Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,406
- 5,583
Kwa upande wa pili, idadi ya watu wanaokwenda kwenye nyumba za ibada kuutafuta "ufalme wa dunia" - majumba, magari vyeo, kufanikiwa kibiashara, kufaulu mitihani, afya njema ya mwili, kuoa/kuolewa, kupata watoto, n.k. bila kwanza kutaka usafi wa roho, imeongezeka sana. Tena wanataka kupata vitu hivyo haraka sana kwa miujiza ya chapchap. Hii imekuwa kivutio kikubwa kwa "watumishi" kuandaa na kuwasilisha "huduma" zinazokidhi mahitaji ya "wateja" wengi badala ya kuweka msisitizo katika kuutafuta Ufalme wa Mbinguni.