Kwa mwaka 2023 Tanzania pekee ndiyo nchi ya SADC na EAC yenye records kubwa za kuweka wapinzani mahabusu, unadhani kwanini tumekaa kileleni?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
879
4,123
Nchi za SADC na EAC zina mfumo wa kidemokrasia na zinatumia katiba somehow inayoendana na Tanzania. Zina sheria na kuna wapinzani ambao baadhi yao wameweza hadi kuongoza nchi mfano Zambia.

Lakini upo ustaarabu flan wa dola ambao umejengeka.; Ni aidha mpinzani kwenye nchi nyingine upo dhaifu kuliko upinzani wa Tanzania au mataifa hayo yamestaarabika.

Mfano, Tundu Lisu amefanya mikutano kanda ya ziwa hakuna mwananchi aliyechubuliwa....lakini amekwenda kwa Wamasai huko kaskazini tayari imekuwa Bingwa....Je ndio kusema watu wa huko kanda ya kaskazini hawana uhuru kama walivyo watu wa kanda ya ziwa? Kwanini tunarudia kosa lilelile la kuwabagua kama walivyofanya S gang?

Hii siyo sifa nzuri kwa nchi; ningependa tujadili kwanini tunaongoza kwa sifa hii isiyo ya Kiutu? Au wingi wa nyumba za ibada na matumizi makubwa ya vitabu vitakatifu katika maeneo mbalimbali kunatutenga na hofu ya Mungu?

Kwanini na nini kifanyike?
 
Hakuna uongozi uliojipambanua kusimamia misingi ya Haki na demokrasia kama hii ya Mh Dr. Samia, wenyewe wapinzani wanakiri hilo mioyoni mwao
 
Back
Top Bottom