Kwa wale wajuzi wa mambo ya Dini, andika jina la Mtume na nchi aliyozaliwa

Mkimuyangu

JF-Expert Member
Oct 5, 2022
1,054
1,929
Nimekuja na hii maada ili watu wapate kujua historia ya Mitume wa Mwenyezi Mungu, inchi walizozaliwa na walikuwa wangapi,

Hapa tunazungumzia Mitume wa Mwenyezi Mungu, siyo wanafunzi wa mitume,Mtume ni yule aliyechaguliwa na Mungu peke, ambaye hata riziki yake anayokula hutoka kwa Mungu, hategemei sadaka

(1) Adamu huyu alizaliwa au aliumbwa peponi, inchi aliyoishi ni Siri lanka
(2)Idrisa, huyu alikuwa mtoto wa Adamu na alizaliwa Iraki
(3)Nuhu alizaliwa Iraki
(4)Hud alizaliwa Yemeni
(5)Salehe alizaliwa Iraki
(6)Ibrahimu alizaliwa Iraki alikuwa rafiki wa Mwenyezi Mungu,na ndiye baba wa Mitume wote waliofuta na ni babu yake Yakobo, na ndiyo Mtume anayekubaliwa na Dini zote, yaani Wayahudi, wakristo na Waisilamu
(7) Luti alizaliwa Iraki, alitumwa kwa watu wa Sodoma na Gomora ambao walikuwa wanatenda zambi za kulawitiana, yaani mapenzi ya jinsia moja mwanaume kwa mwanaume
(8)Ismaili alizaliwa palestina ni mtoto wa Ibrahimu kwa mke wake Hajira alipelekwa kuishi makka pamoja na mama yake, na ndiko anakotokea Mtume Muhammad (S.A.W)
(9)Isahaka au Isaka, alizaliwa palestina ni mtoto wa Ibrahimu kwa mama yake Sala na ni baba yake na Yakubu auYakobo au babu yake Yusufu
(10) Yakubu auYakobo alizaliwa palestina, babe yake alikuwa Isahaka au Isaka ni mtume wa Mwenyezi Mungu, naye akawa Mtume, na mwanaye Yusufu akawa Mtume
(11)Yusufu alizaliwa palestina, alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, na huku akiwa Mfalme wa Misri
(12)Ayubu alizaliwa Saudi arabia, alipata majaribu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, lakini alisimama kwenye Imani yake
(13)Shaibu alizaliwa Syria alitumwa kwa watu wa Madiyani
(14)Musa alizaliwa Misri
(15)Harun alizaliwa Misri ni ndugu wa Musa, huyu aliombewa utume na ndugu yake Musa, sababu Musa alikuwa na matatizo ya kuongea urimi wake ulikuwa mzito, ili akamsaidie katika kazi ya kupambana na Jabali firauni,
(16)Daudi alizaliwa palestina,ni shujaa aliyemuuwa Goriati,
(17)Suleimani alizaliwa palestina, ni mtoto wa kwanza wa Daudi,Mungu alimpa uwezo wa kuongea na wanyama na kuwatawala majini
(18) Eliyasi alizaliwa palestina
(19)Elia alizaliwa palestina
(20)Yunus alizaliwa Iraki ndiye yule aliyemezwa na samaki aina ya chewa halafu akamtema ufukweni mwa bahari
(21) Dhul kafil alizaliwa palestina
(22) Zakaria alizaliwa palestina, ni baba yake na Yahya au Yohana mbatizaji
(23)Yahya au Yohana alizaliwa Syria ni mtoto wa zakaria,Yahya alikuja kutayalisha mapito ya Issa au Yesu
(24) Issa au Yesu alizaliwa Palestina kwa Mama yake Mariamu au Maria
(25) Muhammad (S.A.W) alizaliwa Saudi arabia
 
Gwajiboy Tz
Mwingira
1: BG: Malisa wa kanisa la Ukombozi ministries for all nations.
2: Nabii na Mtume Peter Nyaga wa kanisa la Miracle center,
3: Nabii na mtume Frank Kilawah, wa kanisa la Shiloh Ministries.
4: Nabii na mtume George David Kasambale.(Geordivie) wa kanisa la Geordivie Ministries au Ngurumo ya Upako.
5: Nabii na Mtume Boniface Mwamposa (Buldozer ) wa kanisa la Inuka uangaze.
6: Nabii Frora Peter wa kanisa la Yesu kristo, huduma ya maombezi na uponyaji. Mbezi.

Hao ni wachache kutoka Ndani ya Bongo.
Kwa ufupi tumebarikiwa MA upako Ya kutosha
 
Naomba mods mnibadilishie kichwa cha habari kisomeke majina 25 ya Mitume wa Mwenyezi Mungu
 
Halafu ukiwa mchawi wa hesabu,utaona kwamba pale mahali anapozaliwa nabii wa Kiislamu kuna uhusiano na Mecca,kuna harmonic somewhere katika latitude na longitude.
Likewise,geographic location anapozaliwa nabii wa Kikristu ina mahusiano na Vatican. Inakuwepo harmonic,katika degrees,na minutes,na arcs. Watu wa geo
graphy labda wanaweza kuelewa.
 
Hao wote mitume uliowaorodhesha hawajawai kuwepo, hizo ni White supremacy za mzungu na mwarabu zilitungwa kumtishia mtu mweusi.

Yaan Adamu aumbwe ktk eden alafu nyie wahuni mje mseme kijiografia aliishi ktk hizo nchi ambazo hazina hata sifa ya uoto wa asili wala uwepo wa shahidi za mabaki ya wanyama, mimea na vitu vilivyokuwepo hapo edeni?.

Kiufupi tu manabii wote hao waliishi hapa hapa afrika isipokuwa huyo mtume wa waarabu.

Haya mambo yanachanganya sana na kutuharibia akili za watoto na vizazi vyetu , mnapowafunza uongo ambao babu zetu walidanganywa na ninyi mnaendelea kudanganya.

Afrika ndio ilikuwa Eden na mitume wote waliishi Africa ambako ndiko kuna ushahidi wa uwepo wa maziwa na asali, madini yote, ushahidi wa bustan ya eden, ushahidi wa kibiblia wote upo Africa, why wasomi hamuamki na kuwafunza watu haya mambo, mnabaki kudanganya danganya tu haya mambo?.

Eti edeni ilikuwa iraq huo uongo ni mjinga ndie huamini, yaan jangwa ligeuke rutuba na supporting area kwa mimea? tangu lin? Ushahidi tu wameshindwa kuuthibitisha kuwa huko iraq ilikuwepo eden mnabaki kusingizia mabadiliko ya dunia na upuuzi mwngi, mbona afrika haibadiriki?

Tujitahidi kusoma wajamen tulidanganywa lkn tusikubali huo uongo uendelee kutawala fikra za vizazi vyetu.
 
Halafu ukiwa mchawi wa hesabu,utaona kwamba pale mahali anapozaliwa nabii wa Kiislamu kuna uhusiano na Mecca,kuna harmonic somewhere katika latitude na longitude.
Likewise,geographic location anapozaliwa nabii wa Kikristu ina mahusiano na Vatican. Inakuwepo harmonic,katika degrees,na minutes,na arcs. Watu wa geo
graphy labda wanaweza kuelewa.
Shida ni makao ama hizo sehemu zilikuwa mahala pa matambiko na ibada za mashetan, hizo dini zote hizo sehem zao takatifu zinamilikiwa na Miungu wao wa asili za jamii hizo ambao hawa Miungu ndio wanatawala dini hizi mpka leo hii, sehemu hizo lazma ziwe na nguvu inayoathiri maisha ya kimwili maana bado hao miungu(mashetan) wanashikilia hizo sehemu.

Tafuta mashekhe waliobobea ktk elimu za kidini achana na hawa mapimbi wanaokalili dini huko madrasa hao akina faizafoxy na mapimbi wengine, pia tafuta , wale wasomi wa dini ya kikatoric haswa wale makadinali watakueleza kilichopo nyuma ya haya mambo.

Dunia hii tunaishi basi tu ni vile kuna watu wametaka tusiyajue mambo,
 
Back
Top Bottom