Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wananchi ndio wenye nchi na wana nguvu na mamlaka (kikatiba) kukataa maamuzi ya serikali

Morning_star

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
4,167
11,490
Ukisoma katiba yetu mwanzo mwisho inaongelea wananchi ndio wanaiweka serikali madarakani. Wananchi ndio wanachagua wabunge.

Chama kikuu (CCM) ukisoma ilani yake imejengwa kimamlaka kwa wananchi! Katiba inatoa ruksa uhuru wa kuongea, kupaza sauti kupinga unyonyaji na ukandamizaji wa aina yoyote! Hivyo vyombo vya habari na wana habari hawatanyamaza!

Hata dini zetu kama jambo lina maslahi mapana ya kitaifa zinaruhusiwa (kikatiba) kukataa. Kwahiyo, kwa hili la DP world kuuziwa bandari zetu kihunihuni na wahuni! HAKIKUBARIKI!!

Kila mwananchi mwenye mapenzi mema na nchi yake anapinga kwa nguvu zote mkataba kandamizi wa uwekezaji uliosainiwa kwa rushwa na Rais na kupitishwa kwa njia za rushwa na bunge!

Tutapiga kelele mpaka uondolewe na kama ni lazima, basi majadiliano ya uwazi yaanze upya!
 
Back
Top Bottom