Julias Vimvinyira
Senior Member
- Jun 2, 2025
- 155
- 205
KAMPUNI ya kimataifa ya Fitch Rating inayojihusisha kufanya tathmini ya nchi kukopesheka katika masoko ya mitaji ya kimataifa, imeithibitisha Tanzania kuwa na uchumi thabiti wenye uwezo wa kukopesheka katika masoko ya mitaji kimataifa.
Kupitia taarifa ya kampuni hiyo iliyochapisha hivi karibuni, ilieleza uthibitisho huo umechangiwa na ukuaji imara wa Pato la Taifa (GDP), mfumuko mdogo wa bei, usimamizi mzuri wa sera za uchumi na kuimarisha ushirikiano na taasisi za kimataifa.
Taarfa hiyo ilieleza kuwa uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.9 mwaka 2025, ukichochewa na sekta za kilimo, madini, utalii, uwekezaji katika miundombinu kama mradi wa reli ya kisasa (SGR) na mradi wa umeme wa Mwalimu Nyerere.
Vilevile, ilieleza kuwa Tanzania imepongezwa kwa kudhibiti mfumuko wa bei ambao umebaki ndani ya lengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) la asilimia tatu hadi tano, kuboresha usimamizi wa fedha za umma ambapo madeni yaliyokuwa yakisubiri kulipwa kwa wazabuni na marejesho ya VAT yamepungua kutoka asilimia 1.2 ya GDP mwaka 2022 hadi asilimia 0.4 kufikia Machi mwaka huu.
Fitch ilieleza kupitia matokeo hayo kwamba wanatarajia mwelekeo wa sera kuendelea kuwa thabiti chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, jambo litakaloendelea kuwavutia washirika wa maendeleo na wawekezaji nchini.
Ripoti hiyo ilieleza kuwa, Tanzania imeweza kudumisha akiba ya fedha za kigeni ambapo hadi Machi mwaka huu ilifikia dola bilioni 5.7 sawa na uwezo wa kulipia uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa miezi 4.2.
Kadhalika, Fitch ilieleza kuwa kuongezeka kwa akiba ya fedha za kigeni, kuendeleza utekelezaji mzuri wa sera za uchumi na kuendelea kuvutia wawekezaji wa sekta binafsi kunaweza kuiwezesha Tanzania kupandishwa daraja zaidi.