Kwanini Mungu hazungumzi tena na watu wa leo?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
344
1,007
KWA NINI MUNGU HAZUNGUMZI TENA NA WATU WA LEO?

Leo 14:45hra 27/11/2022

Je unaweza kuitambua sauti ya Mungu!? Je ukipata ndoto au maono utaweza kutambua huyu azungumzae nami ni nabii Musa, ama Nabii Elia ama ni Yesu Kristu? Unapaswa kuwajua awa kwa kuwasoma kwenye maandiko jinsi walivyo ili uwaonapo ndotoni,ujue pasipo na shaka kwamba huyu, ni Nabii Elia ama huyu ni Nabii Musa,ama huyu ni Malaika Gabriel,sasa basi lugha ya kimaono na kiishara ni kama picha za kuchora za katuni moyoni mwako na katika ufahamu wako,kutafsiri ni sawa na kuwasha umeme kwenye socket ukifika kwenye balbu unakuwa mwanga,kuna kiwango cha kiroho ambacho kitakupeleka karibu zaidi na Mungu nawe utaweza kutafsiri,utasikia atakachosema Mungu moyoni mwako kwa maana upo karibu nae.

Kuna ngazi nne za mawasiliano ya kiroho, ngazi ya lugha, ngazi ya mwonaji, ngazi ya tafakuri, ngazi ya kiishara, hivi ni viwango ya kiroho vitakavyokufanya uweze kusikia sauti ya Mungu. Je, wewe ni mcha Mungu kiasi gani, kiasi chako cha ucha Mungu ndio kitakusogeza karibu na Mungu na atakacho kisema utakisikia, sali kwa uaminifu na unyenyekevu, soma na kupekua maandiko ya Mungu kila siku,ishi sheria ya mfungo. Je, una uzoefu wa hisia za upendo, shangwe, amani, subira, unyenyekevu, upole, imani matumaini na faraja moyoni mwako? Je! Mawazo yameshawahi kukujia akilini mwako au hisia moyoni mwako, ambazo unajua zinatoka kwa Bwana, na sio hisia za kawaida kutoka kwako? Je, Umewahi kusikia sauti yako ikiongea ukweli bila kupanga kile utakachosema?Je umeshawahi kutambua dhambi katika maisha yako na ukapata hamu ya kurekebisha?Je umeshawahi kuhisi Roho akitukuza na kushuhudia juu ya Mungu Baba na Yesu Kristo?

-Namna ya kuitika na kujibu sauti ya Mungu.

1Sam 3:4 Kisha Bwana akamwita Samweli,Samweli akajibu, “Mimi hapa.”Naye akakimbia kwa Eli na kumwambia, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.”Lakini Eli akasema, “Sikukuita; rudi ukalale.” Hivyo akaenda kulala,Bwana akaita tena,“Samweli!” naye Samweli akaamka, kwenda kwa Eli na kusema, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.”Eli akasema, “Mwanangu, sikukuita, rudi ukalale.”Wakati huu Samweli alikuwa bado hajamjua Bwana,Neno la Bwana lilikuwa bado halijafunuliwa kwake,Bwana akamwita Samweli mara ya tatu, naye Samweli akaamka kwenda kwa Eli na kusema, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.” Ndipo Eli akatambua kuwa Bwana alikuwa akimwita kijana, hivyo Eli akamwambia Samweli, “ nenda ukalale, na kama akikuita, sema, ‘Nena Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza.’ ” Hivyo Samweli akaenda na kulala mahali pake,Bwana akaja akasimama hapo, akiita kama mara zile nyingine, “Samweli! Samweli!” kisha Samweli akasema, “Nena Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza.”

Kufikia hapa tunaelewa sasa,ya kwamba,Bwana Mungu anazungumza na kila mtu, ananena lakini hatusikii, anaita lakini sisi ndio hatuitiki, tatizo linakuja ni hatujui jinsi ya kuielewa sauti yake, tunataka Mungu azungumze kwa njia zetu sisi kama vile mtu anaongea na rafiki yake, lakini hatutaki yeye azungumze katika njia zake na hapo ndipo tunapomkosa.Isaya 65: 12 “……..Nilipoita hamkuitika; niliponena,hamkusikia; bali mlitenda yaliyo mabaya machoni pangu, mlichagua mambo nisiyoyafurahia”. Ni dhahiri usipokuwa na Neno la Mungu ndani yako, ni ngumu kuielewa sauti ya Mungu, kwani ni kweli atazungumza na wewe lakini hautamwelewa hata kidogo..Imekuwa ni ngumu kwa watu wengi kuisikia sauti ya Mungu ikizungumza maishani mwao, hii ni kutokana na kwamba hawamjui wanayemwomba, sasa utamjuaje unayemuomba,nenda katika njia zake kwa kuongozwa na neno lake,yakupasa kusoma neno lake ili umjue,utakapomjua na kuenenda kwa uaminifu katika njia,utakuwa umefikia kiwango Fulani cha kiroho kitakachokuwezesha kuisikia sauti ya Mungu,kupata maono na kuyafafsiri.

Nimalizie kwa neno muhimu kabisa,Ishi sheria ya mfungo,Ili kuongeza uwezo wetu wa kusikia sauti ya Roho, sisi sote tutaweza kufanya vyema kufunga kwa masaa 24 siku ya jumapili ya kwanza au ya mwisho wa mwezi na kutoa toleo letu la ukarimu la mfungo ili kusaidia wale walio na mahitaji, “Bwana alisema kwa Isaya, kwamba wale wanafunga na kutoa mkate kwa wenye njaa,wanaweza kumwita na Bwana atajibu, wanaweza kulia na Bwana atasema, ‘Mimi hapa’ Isaya 58:6–9.hii ni njia moja ya kuendelea katika masharti ya kuongea na Bwana,tunapokwenda kumaliza Mwaka, yajaribu mwaka huu,na mwakani fanya hivyo Mwaka mzima na kila Mwaka, Ishi sheria ya mfungo kikamilifu, tukifanikiwa hilo tutaweza kuliombea taifa letu dhidi ya roho ya umasikini, ujinga na maradhi,roho ya rushwa na ufisadi, roho ya kupeleka kusipo pesa za serikali, roho ya kurudi nyuma kimaendeleo, roho ya maisha magumu, yote haya tutaweza kuyaondoa kwa kufunga na kuomba.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 

smaki

JF-Expert Member
Jan 23, 2019
4,980
2,929
Mungu hawezi kuzungumza na watu wajinga kama wewe.
Ni kweli uko sahihi! mungu wako hawezi fanya ivo, km unavowaza!! lkn Mungu wangu anaweza yote!...hata akitaka sasa ivi anakupiga kigugumizi cha mikono, hutaandika hapa tena!! unabishaaa??
 

Demi

JF-Expert Member
Nov 22, 2016
31,297
60,320
Ni kweli uko sahihi! mungu wako hawezi fanya ivo, km unavowaza!! lkn Mungu wangu anaweza yote!...hata akitaka sasa ivi anakupiga kigugumizi cha mikono, hutaandika hapa tena!! unabishaaa??
Acha vitisho ndugu
 

smaki

JF-Expert Member
Jan 23, 2019
4,980
2,929
Wewe ndo unatakiwa kuamini sio mimi. Inakuaje hujiamini?
wewe kibibi vepi?? nakwambia kesho huamki unasema tena mara mimi heee!!! una vurugu ya maono wewe?? au! ...ntakushukia hapooo usiku... heee!...kwanza ngoja Mungu apumuzike naanza ku deal na wewe

subiri tu unatanitafuta... kwanza

weye ni kademu? ....au kidume mbusi?? sasa sikia.......nakuja kwanza.......
 

She Quoted you

JF-Expert Member
Oct 19, 2020
555
753
Anazungumza na kina Geordavie mkuu.

Tofauti binadamu wa sikuizi washajanjaruka, akitokea mhuni kama Mwampisa akasema ameongea na mungu jana hamna anayemuamini (wachache sana watamuamini)
ila enzi za kale enzi za mawe, Akitokea Jamaa kama Muhamad au Paulo anakusanya kijiji anaanzisha na dini kabisa
 

smaki

JF-Expert Member
Jan 23, 2019
4,980
2,929
WA NINI MUNGU HAZUNGUMZI TENA NA WATU WA LEO?
Wanadamu mna maudhi sana bana! km Nyerere tu kajitolea weee! mzee watu kulikomboa Bara la Africa/tanzania /zanzbar lkn mpaka sasa kuna watu wanambeza!!

kumbuka tumeumbwa kwa mfano wake!! yamkini hata yupo anapita pita humu! km mtu tu! makazini humo! tena anaweza kuwa ombaomba tu! ila utamdharau!

anaongea sana ndotoni lkn sababu una dhambi unasahau lkn wenzako sie tunaamshwaga tunapiga swaga sana na MUNGU! Msimuzoeee Mungu sanaaaaa
 

smaki

JF-Expert Member
Jan 23, 2019
4,980
2,929
Nia yako tukufate inbox🙄. Subiri hapo
Afu weee Demi wewe? ?........ heee! mnifuate in box! kwani mko wangapi?....njo mwenywe banaaa! nimesubiri weeee! hata sijakuona asaaa niondoke au nivumilie kwanza!
 

Demi

JF-Expert Member
Nov 22, 2016
31,297
60,320
Afu weee Demi wewe? ?........ heee! mnifuate in box! kwani mko wangapi?....njo mwenywe banaaa! nimesubiri weeee! hata sijakuona asaaa niondoke au nivumilie kwanza!
Nimeamka salama hata sijafa 🤣😀
 

Norshad

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
5,121
11,850
Mungu yumo ndani mwako kama huisikii sauti yake maana yake wewe ni mfu
 

Norshad

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
5,121
11,850
Mungu yumo ndani mwako kama huisikii sauti yake maana yake wewe ni mfu
 
3 Reactions
Reply
Top Bottom