Kwa mtazamo wangu ilikuwa ni lazima aondoke kwa sababu kama hizi:

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,912
Kushindwa kukabiliana na Matukio ambayo yameichafua Idara kwa muda mfupi aliokuwepo.
Kushindwa kukamilisha baadhi ya Maagizo ya Kimkakati dhidi ya Maadui wa nchi na Bosi wake.
Kushindwa Kuwaunganisha Watendaji wake ambao wamegawanyika na wanasalitiana sana.
Kuhisiwa Kwake kuwa na Yeye pia ni Mmoja wa Wasaliti wakuu wa Idara kwa Jina la Kigogo.
Kushindwa kutumia Utaalam wake mkubwa wa IT kuweza Kumjua Mtu anayeonekana ni tishio.
Kushindwa kudhibiti Uvujaji wa Siri nzito na kubwa za Idara hatimaye Kuichafua Idara.
Ripoti zake za Kiutendaji Kukinzana na za Mtu ( Kivuli ) aliyewekwa ambaye Yeye hakumjua.

Nasisitiza tena kwamba huu ni mtizamo wangu Mimi kama Mimi na sikulazimishi ama uukubali au uukatae.

Pole sana Mchungaji Njagu na kwa hali iliyopo najua kwa sasa utateseka na Kuathiriwa mno Kisaikolojia. Vumilia kwani najua kwa Heshima yako na hasa kwa kuwa Kwako DG basi lazima tu utapewa Zawadi ya Kutulizwa Moyo hasa ya Ubalozi katika moja ya nchi Kubwa na Rafiki kwa Tanzania iliyopo ama Bara la Ulaya au Asia muda si mrefu baada ya Wewe kumaliza Kutoa Ushahidi wako juu ya yale ambayo umehisiwa nayo na yamekugharimu leo.
 
Kushindwa Kuwaunganisha Watendaji wake ambao wamegawanyika na wanasalitiana sana.Kuhisiwa Kwake kuwa na Yeye pia ni Mmoja wa Wasaliti wakuu wa Idara kwa Jina la Kigogo.Kushindwa kutumia Utaalam wake mkubwa wa IT kuweza Kumjua Mtu anayeonekana ni tishio.

Hivi ndivyo vilivyomuondoa hapo, Kigogo na Membe wamemgharimu Mkubwa...
 
wacha athumani atuonyeshe maujuzi aliyotoa huko polisi.

ila mimi binafsi ningekuwa idarani ningekuwa mwoga sana,maana hukawiii kuumbuka.
 
Ile ni taaluma tu kama uliyonayo mkuu, Sema hii position inaamua kifo na uhai wa watu kutokana na maamuzi mbali mbali ambayo mtu huyo kafanya.
wacha athumani atuonyeshe maujuzi aliyotoa huko polisi.

ila mimi binafsi ningekuwa idarani ningekuwa mwoga sana,maana hukawiii kuumbuka.
 
Yote kheri, muhimu ni nchi, serikali na RAIA kuendelea kuwa salama, yenye amani, utulivu na maendeleo. Taifa kwanza, MTU baadae
 
Ina maana hapo ni mtu aombe Mungu Kigogo aendelee kutrend..?

Vinginevyo itahisiwa Kigogo ni mkono wake?
 
Back
Top Bottom