Kwa mtaji huu atufiki

drphone

JF-Expert Member
Sep 29, 2009
3,542
281
wakuu poleni na mapumziko ya wikiendi
jamani jana tulikuwa na mkutano na mwenyekiti na diwani wetu mkutano ulikuwa mzuri uku diwani akijitaidi kujishusha kwa wananchi kwamba wasimwogope kwani ss wananchi ndio mabosi wake akaeleza malengo yake akaomba msaada tufanyeje tuzitokomeze tukahoji kabla atujafikiria tutatengenezaje barabara wakati waliomtangulia walishakula pesa ziliotolewa na wahisani na michango ya wananchi zote wamezila na barabara azipitiki kwa mchanga, wamekula pesa za makalavati zilitolewa na tasafu na wananchi tulichanga zote wamechakachua na wamemaliza mda wao tunao mitaani jibu la diwani ni fupi sana alituliza hayo yametokea wakati yy akiwa madarakani? tukasema no akasema yolopita si ndwele tushirikiane upya tulete maendeleo.

kweli namna hii ya kufukia fukia na kulindana tutajenga nchi kweli au na yy anajiandaa kuchakachua kwa kweli kaniachia maswali mengi yasio na majibu.

wakuu ebu tupeane mawazo tuwafanyeje walochakachua pesa za miradi ya maendele ya kata yetu ikiwa wengi wao hawapo tena madarakani ila wengi wana vyeo ktk ccm kwenye vitongoji
 
Kwa hiyo unataka kumuadhibu diwani mpya kwa makosa yaliyofanyika kipindi kilichopita?
 
Back
Top Bottom