Kwa nini Tanzania kutakua na maandamano makubwa huu mwaka.

Tall Guy fam

JF-Expert Member
Jan 16, 2017
917
1,089
Habari wakuu
Mpaka sasa ipo wazi kuwa taarifa za ishu ya maandamano zimesambaa sana nchini, especially baada ya kupewa kiki na magazeti pamoja na polisi wao wenyewe katika press zao. Swala la kwamba yatafanyika na kufanikiwa au hayatafanyika ndio ishu ambayo watu wengi wanajadili kwa sasa.

Muamko ni mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram na Telegram ambapo watu wengi wanaonyesha kuunga mkono. Hizi ni, kwa maoni yangu, sababu kuu 3 kwa nini huu mwaka tutashuhudia watanzania wakiandamana kwa amani.

1. Mateso
Mpaka sasa, asilimia kubwa ya wananchi wameshaisoma namba. Magufuli alipoingia madarakani alijenga dhana ya kwamba yeye ni rais wa wawanyonge, na watu pekee ambao watapata shida ni mafisadi, viongozi wanaotumia vibaya madaraka , wakwepa kodi, wahalifu n.k huku akiwaacha wananchi wanyonge wakiifurahia keki ya nchi yao. Matokeo yake ikawa kinyume na matarajio ya wengi.

Katika kipindi cha miaka miwili+, amefanya maisha yawe magumu zaidi kwa wanyonge, mfano hai ni kubomoa nyumba bila fidia, kutofikisha michango ya rambirambi, wanafunzi kukosa mikopo, kupunguza wafanyakazi, kutokupandisha madaraja wafanyakazi wa uma wala mishahara yao, just to name a few. Watu hawa wana kinyongo na ni rahisi kuandamana ili kumuondoa rais kwani wanajisikia kusalitiwa. Na wanajua, maisha yatazidi kuwa magumu endapo ataendelea kubaki.

2. Hayaongozwi na upinzani

Hii ishu ya maandamano ilianza kiutani utani mnamo tarehe 18 Februari 2018, katika account ya instagram ya Mange Kimambi. Jinsi siku zinavyoenda ndivyo inavyozidi kupata muamko na uungwaji mkono wa watanzania wengi, hii ni kutokana na sababu zilizoainishwa hapo juu (1).

Baada ya kuona vitendo vya kinyama walivyofanyiwa CHADEMA katika uchaguzi wa ubunge kinondoni na Siha tarehe 17, pamoja na kifo cha Akwelina jana yake na kile cha diwani wa chadema morogoro, watanzania wengi, akiwemo Mange Kimambi, walitarajia chama kitafanya press conference na kuja na ajenda mpya ya maandamano ya amani kupinga kubanwa kwa uhuru, uonevu pamoja na kuvunjwa kwa demokraisia nchini. Hawakufanya hivyo, badala yake kwenye mkutano wao waliendelea kulalamika tu kama kawaida.

Hicho kitu kilimkera Mange ndipo akaamua kuhamasisha wananchi wajikomboe wenyewe. According to her, mwanasiasa yoyote anaruhusiwa kuunga mkono jitihada lakini haruhusiwi kushika usukani. Faida kubwa ya hii approach ni kwamba serikali itakosa sababu za msingi za kuwashitaki viongozi wa upinzani kwa sababu hawahusiki. Lakini pia, inaondoa risk ya kukwamishwa na hao viongozi wa upinzani kwa kuyaahirisha Kama walivyofanya kwa UKUTA mwaka 2016. Faida nyingine ni kujenga hofu kwa Rais ajaye ya kuheshimu matakwa ya wananchi wake.

3. Ndani ya mwezi wa 3 na 4 zitakuja sababu zaidi
Kuna matukio ambayo yatatokea katika hiki kipindi ambayo yatazidi kuwaudhi wananchi na kuwapa hasira na mzuka wa kuandamana. Kwa jinsi awamu hii inavyokwenda, sitashangaa polisi wakimpiga risasi mwananchi mwingine asiye na hatia, kiongozi mkubwa wa upinzani kufungwa jela, kutekwa na/au kuuawa kwa mkosoaji maarufu wa serikali, nakadhalika. Tumeshaona tayari uongo wa kichwa cha treni ulivyozidi kuwakera wananchi, tutarajie ishu kubwa zaidi.
 
Back
Top Bottom