Kwa msafara huu wa Rais, bado tuna safari ndefu

Hiyo ndio Athari ya viongozi wetu kushadadia petty issues...Karne hii unambeba Mkuu wa Nchi aende kuzindua Visima au Barabara iliyopakwa Lami kwa juu?... Kuzindua miradi ni Kazi za madiwani , wenyeviti wa Halmashauri na Mameya. Kazi ya Serikali kuu ni kufanya projects na kuwakabidhi local government kupitia viongozi wa wananchi...sasa liproject umelibuni wewe,10%wewe, kulisimamia wewe ata kulizindua unataka wewe, tena kwa gharama kubwa...WHY!?
 
Hivi wale madereva wa Mama wanakula kitu ya Arusha kabla ya Safari?
Maana ule mwendo ni balaa!
 
Na kibaya zaidi hakuna cha maana anachofanya toka arithi uongozi
Alikuta bwawa la umeme rufiji limefika 33%,Sasa lipo70+%,barabara zinajengwa,kinyerezi inaendelea,anaajiri,Katia ruzuku za pembejeo za kilimo ili usilie njaa mwakani,mikopo kwa wanafunzi wote wenye sifa elimu ya juu,anapandisha madaraja watumishi nk,labda wewe ulitaka afanye nini ili uone anafanya kitu!?
 
pikipiki 8, HardTop za kusafisha njia ni 24, zinakuja Hilux 12, zinakuja V8 30, then Hilux 10, zinafunga HardTop 15 mwishoni kabisa
Msafara wa rais unaratibiwa na usalama wa taifa,Kama una utaalam wa mifumo ya usalama wa viongozi kwa gharama nafuu,tafadhali fika makumbusho makao makuu ya usalama wa taifa uwashauri kiundani
 
Alikuta bwawa la umeme rufiji limefika 33%,Sasa lipo70+%,barabara zinajengwa,kinyerezi inaendelea,anaajiri,Katia ruzuku za pembejeo za kilimo ili usilie njaa mwakani,mikopo kwa wanafunzi wote wenye sifa elimu ya juu,anapandisha madaraja watumishi nk,labda wewe ulitaka afanye nini ili uone anafanya kitu!?
Angekuwepo magufuli huo mradi ungekuwa umekamilika
 
Wakuu niko Arusha, mara nyingi huwa naona kwenye TV tu ila awamu hii nimeshuhudia kwa kwa uhalisia kabisa bila chenga.

Nimehesabu magari nikachoka nikaacha ila nikabaki kujiuliza maswali tu.

1. Gharama za huu msafara na afya kwa taifa. Kuna madhara gani magari yakapunguzwa?

2. Kama haiwezekani kwanini Rais asipunguze ziara fulani fulani kupunguza hizi gharama kwa taifa?

3. Kwa hali hii kuna uwezekano Rais akaenda kuzindua mradi wenye gharama ndogo kuliko gharama za ziara yake.

4. Viongozi wetu kuweni na moyo wa huruma kwa taifa nchi hii ni yetu sote na kuna maisha baada ya dunia.
Ulitaka watembee kwa miguu
 
Back
Top Bottom