Jumakidogo
R I P
- Jul 16, 2009
- 1,851
- 427
Habari za kazi mheshimiwa Rais, pole sana na majukumu pamoja na visafari vya hapa na pale. Sielewi nikusalimie kwa salamu ipi, lakini bila shaka shikamoo itafaa zaidi. Mimi ninaye kuandikia barua hii ni raia wa kawaida sana. Ni mtu wa mtaani tu kama walivyo watanzania wengine.
Nimekuandikia kupitia hapa kwa sababu sina namna nyingine kufikisha ujumbe wangu kwako. Naamini kwa njia hii, maneno yangu yatakufikia huko uliko.
Mheshimwa, sidhani kama unatambua kuwa, hivi sasa watanzania tuna matatizo makubwa sana. Maisha yamekuwa magumu, ajira hakuna, thamani ya shilingi imeporomoka, maandamano kila kukicha, watu wasio na hatia wanaumizwa bila ya sababu, mfumuko wa bei kila baada ya masaa sita.
Imekuwa afadhali ya Zimbabwe na Somalia. Hata mishahara ya sisi walimu sasa imekuwa kama bahati nasibu. Hayo ni machache tu, lakini kuna mengi zaidi ambayo hayaandikiki. Pamoja na yote hayo, umekuwa kimya sana. Kimya kama kifaranga kilicho ndani ya yai.
Waswali wanasema; kukaa kimya ni namna moja nzuri ya kumpuuza anayekupigia kelele. Lakini kumbuka kuwa, kimya kingi, kina mshindo mkuu.
Moja ya mfano wa mshindo huo, ni kile kilichotokea Mbeya. Hata ukiwa kimya, ni imani yangu kuwa ujumbe na maneno ya watanzani unayasikia kwani hata mabango barabarani hayaongei, lakini watu wakisoma wanaelewa.
Wakati unaingia madarakani, mimi ni mmoja wa watu waliokupigia kura japo itikadi zetu kisiasa ni tofauti. Lakini mpaka sasa sijafaidika na chochote katika utawala wako. Labda cha maana nilichofaidika nacho ni kuacha pombe.
Nimeacha kwa sababu hali imekuwa ngumu na kulazimika kupunguza matumizi yasiyo ya lazima. Unajua kuwa umaarufu wako uliotuka sasa unabalika? Watu wanaona kuwa unawatesa sasa, wengi wanaona kuwa umewageuka.
Vijiweni jina lako limekuwa ndiyo agenda kuu kwa sasa. Naomba ujitokeze utupe japo maneno ya kutufariji tu ili mioyo yetu iburudike na kurejewa na matumaini.
Mengi yametokea, lakini binafsi napenda sana wanyama wa porini. Hivi ni nani aliyeswaga wale twiga kutoka porini na kuwapakia katika ile ndege?
Mpaka sasa waliohusika wamechukuliwa hatu gani? Halafu walikuwa twiga ndama au? Manaake nadhani kumswaga twiga mzee ni kazi kubwa sana.
Mwisho naomba ujue kuwa, wananchi hali zetu ni mbaya sana kwa sasa. Tunahitaji msaada. Nashukuru sana kwa ukarimu wako..Ni mimi raia mwema.
Naishi Mbezi hapa Dar es salaam.