GE2025 Imfikie Rais ayafanye ili kuondoa kinachoendelea kwa wananchi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Ninja

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2010
Posts
361
Reaction score
726
Mheshimiwa rais,

Nakusalimu kwa unyenyekevu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Mheshimiwa rais, nafupisha sana nisikupotezee muda wako adhimu.

Mheshimiwa rais, yafuatayo ni mambo niliyoyatafiti na hivyo nimeona vema kukushirikisha kwa njia hii:

1. Nchi haijakushinda kama baadhi ya watu wanavyodai. Hata hivyo kuna 'machawa' wanaokuzunguka wana lengo hilo, kukufanya ufeli, hata hivyo umewaamini sana kwa sababu ya tabasamu lao usoni, maneno yao ya kukusifu na hata yale mliyoyarekodi kwa siri, walijua kuwa wanarekodiwa. Pima matokeo 'output' na athari 'outcome' ya mapendekezo na ushauri wao kwako na sio mashamsham 'vibe' za kipambe wanazokupa. NI WATU HATARI SANA KWAKO.

2. Tunafanya kazi kwa ajili ya vizazi vyetu vya baadaye. Hakuna haja ya kuwaachia watoto wetu matatizo tunapoondoka madarakani au hata duniani. Kwenye 'deals' zenye utata hakuna mtu huiweka familia yake kuja kujibu baadaye na hasa katika mazingira ya kutokuwa na kinga ya kutokushtakiwa.

3. Tanzania mpya sio njema kabisa kwa CCM japo inaweza kuwa njema kwa taifa 'in a long run'. Tanzania mpya itazaliwa endapo (i) kesi ya TAL itaendelea (ii) Humphrey Pole Pole hatopatikana akiwa na hali njema (iii) Maswali ya wananchi kuhusu watekaji hayatojibiwa kwa vitendo (iv) Vita haramu dhidi ya vyama vya upinzani havitakomeshwa.

4. Yuko adui mkubwa na mwenye nguvu nyuma ya haya yanayotokea. Kwako amejifanya rafiki. Lengo lake ilikuwa uchafuke wewe, akutoe aweke watu wake. Humphrey Polepole akagundua na kukusaidia. Leo hii taifa limejua kuwa kumbe shetani sio wewe, bali kuna namna umekuwa 'captured', na kwa maslahi ya taifa inabidi ucheze mziki wao. TUTAKUOKOA.

Mama nakuomba ufanye yafuatayo ASAP (kwa unyenyekevu nakusihi):

1. Tuma watu wako (wale 'first class E1) washirikiane na vijana wa Nkunda mkamwokoe Humprey huko aliko. Humphrey hakuwa anakushambulia kama ulivyodhani bali alikuwa anakuokoa wewe, kwa mujibu wa viapo vyetu, wewe ndiye alama ya taifa. Haya ni mambo ya Cuba mama. Kama sio Humprey kutuonyesha adui namba moja wa dola yako ni nani leo hii wangeshakumeza. Ilikuwa usifike Oktoba. Ukichelewa, sijui kitakachojiri.

2) Kesi ya Tundu Lissu, DPP aipige chini fasta. Huyo Tundu Lissu hana madhara akiwa uraiani kuliko akiwa kwenye hali hii ya sasa. Taifa linachafuka sana. Tumieni watu wenye akili watakusaidieni, sio hao wenye kujua kuua tu bila kujua namna ya kulinda mustakabali wa taifa. I can also help.

3) Mtumie Humprey kukusaidia kabla ya 29/10. Ana uwezo na ana watu wenye uwezo, wa rika mbalimbali kuzima matatizo ambayo yanaweza kutokea kwa taifa. TISS wakikupa 'intel analysis' ya kweli utagundua kuwa anayeyasukuma haya yote anaendelea kufanikiwa kwa kukudanganya. Kumbuka walivyomdanganya JPM.

4) Msigwa angejitahidi kukutenganisha na udhalimu wa 'shetani wa pwani'. Huyo anayempa 'script' zinakuchafua wewe na kumpamba 'swp'. Alipaswa katika kila 'script', akutenge na kashfa zote: utekaji, kuuzwa bandari, Kiziga, Rostam, JK, mauaji n.k. kuna namna ya kuja na script zinazojenga taswira njema kuhusu rais, serikali n.k na sio hizo za kuwatisha Gen Z na za majigambo.

5) Tunaojua ukweli, tunajua rais wetu huhusiki na kashfa yeyote, isipokuwa UMETEKWA. Tunataka tukuokoe mama yetu, kutoka mikononi mwao 'before it's too late'.

6) Tuko kambini hapa, fanya upande wako na sisi tutakulinda, wasikudanganye walamba damu, hutaingia Ikulu kwa njia zao, acha sisi wananchi tukuthibitishe. Mbaya wetu tushamjua. Aliyetaka kutuchonganisha na wewe mama yetu tushamjua. Picha mbaya waliyotengeneza tutaiondosha.

Tusikilize sisi wananchi wako tulio na mapenzi thabiti kwako. Achana na machawa na huyo shetani wa Pwani WATAKUPOTEZA mama.

Nimetimiza wajibu wangu mama. Nimekwambia ukweli.

Nina mengi ya kukuambia, lakini nimejaribu kukupa hayo machache bila kumpa adui faida.

Nawasilisha kwako kwa unyenyekevu mkubwa, mheshimiwa rais.

Asante!

Ninja.
 
Tanzania Tatizo Halipo Kwa Mtu Kwahiyo Hataaje Malaika Hapewe Nafas Kuongoza Kwenye Mfumo Huu Bado Hataonekana Ni Wale Wale Tu Hamna Jipya Litakao Unekana

Tatizo Lipo Kwenye Mfumo Wenyewe Wa Uendeshaji Katika Uongozi Kuwepo Mitandao Mingi Inayo Ulinda Mfumo Huu

Njia Pekee Ni Kuutoa Mfumo Huu Wasasa Kuleta Mpya Wenye Tumaini Bora Kwa Taifa Letu
 
Kwa kweli ndg umeongea kwa hekima kubwa sana na kwa upendo mkubwa sana. Mama tu hapa anatakiwa kuelewa picha nzima ilivyo.

Mie siongezi ila umemaliza mkuu, kitu cha ajabu watu wengi wanahisi wanatekwa raia tu kumbe hata mama naye ametekwa mateka.😥 Na anatakiwa kuokolewa, shetani wa Pwani ni kama limzimu hivi la kunywa damu.

29 inakuja kwa kasi sana kuanzia sasa
 
Mheshimiwa rais,

Nakusalimu kwa unyenyekevu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Mheshimiwa rais, nafupisha sana nisikupotezee muda wako adhimu.

Mheshimiwa rais, yafuatayo ni mambo niliyoyatafiti na hivyo nimeona vema kukushirikisha kwa njia hii:

1. Nchi haijakushinda kama baadhi ya watu wanavyodai. Hata hivyo kuna 'machawa' wanaokuzunguka wana lengo hilo, kukufanya ufeli, hata hivyo umewaamini sana kwa sababu ya tabasamu lao usoni, maneno yao ya kukusifu na hata yale mliyoyarekodi kwa siri, walijua kuwa wanarekodiwa. Pima matokeo 'output' na athari 'outcome' ya mapendekezo na ushauri wao kwako na sio mashamsham 'vibe' za kipambe wanazokupa. NI WATU HATARI SANA KWAKO.

2. Tunafanya kazi kwa ajili ya vizazi vyetu vya baadaye. Hakuna haja ya kuwaachia watoto wetu matatizo tunapoondoka madarakani au hata duniani. Kwenye 'deals' zenye utata hakuna mtu huiweka familia yake kuja kujibu baadaye na hasa katika mazingira ya kutokuwa na kinga ya kutokushtakiwa.

3. Tanzania mpya sio njema kabisa kwa CCM japo inaweza kuwa njema kwa taifa 'in a long run'. Tanzania mpya itazaliwa endapo (i) kesi ya TAL itaendelea (ii) Humphrey Pole Pole hatopatikana akiwa na hali njema (iii) Maswali ya wananchi kuhusu watekaji hayatojibiwa kwa vitendo (iv) Vita haramu dhidi ya vyama vya upinzani havitakomeshwa.

4. Yuko adui mkubwa na mwenye nguvu nyuma ya haya yanayotokea. Kwako amejifanya rafiki. Lengo lake ilikuwa uchafuke wewe, akutoe aweke watu wake. Humphrey Polepole akagundua na kukusaidia. Leo hii taifa limejua kuwa kumbe shetani sio wewe, bali kuna namna umekuwa 'captured', na kwa maslahi ya taifa inabidi ucheze mziki wao. TUTAKUOKOA.

Mama nakuomba ufanye yafuatayo ASAP (kwa unyenyekevu nakusihi):

1. Tuma watu wako (wale 'first class E1) washirikiane na vijana wa Nkunda mkamwokoe Humprey huko aliko. Humphrey hakuwa anakushambulia kama ulivyodhani bali alikuwa anakuokoa wewe, kwa mujibu wa viapo vyetu, wewe ndiye alama ya taifa. Haya ni mambo ya Cuba mama. Kama sio Humprey kutuonyesha adui namba moja wa dola yako ni nani leo hii wangeshakumeza. Ilikuwa usifike Oktoba. Ukichelewa, sijui kitakachojiri.

2) Kesi ya Tundu Lissu, DPP aipige chini fasta. Huyo Tundu Lissu hana madhara akiwa uraiani kuliko akiwa kwenye hali hii ya sasa. Taifa linachafuka sana. Tumieni watu wenye akili watakusaidieni, sio hao wenye kujua kuua tu bila kujua namna ya kulinda mustakabali wa taifa. I can also help.

3) Mtumie Humprey kukusaidia kabla ya 29/10. Ana uwezo na ana watu wenye uwezo, wa rika mbalimbali kuzima matatizo ambayo yanaweza kutokea kwa taifa. TISS wakikupa 'intel analysis' ya kweli utagundua kuwa anayeyasukuma haya yote anaendelea kufanikiwa kwa kukudanganya. Kumbuka walivyomdanganya JPM.

4) Msigwa angejitahidi kukutenganisha na udhalimu wa 'shetani wa pwani'. Huyo anayempa 'script' zinakuchafua wewe na kumpamba 'swp'. Alipaswa katika kila 'script', akutenge na kashfa zote: utekaji, kuuzwa bandari, Kiziga, Rostam, JK, mauaji n.k. kuna namna ya kuja na script zinazojenga taswira njema kuhusu rais, serikali n.k na sio hizo za kuwatisha Gen Z na za majigambo.

5) Tunaojua ukweli, tunajua rais wetu huhusiki na kashfa yeyote, isipokuwa UMETEKWA. Tunataka tukuokoe mama yetu, kutoka mikononi mwao 'before it's too late'.

6) Tuko kambini hapa, fanya upande wako na sisi tutakulinda, wasikudanganye walamba damu, hutaingia Ikulu kwa njia zao, acha sisi wananchi tukuthibitishe. Mbaya wetu tushamjua. Aliyetaka kutuchonganisha na wewe mama yetu tushamjua. Picha mbaya waliyotengeneza tutaiondosha.

Tusikilize sisi wananchi wako tulio na mapenzi thabiti kwako. Achana na machawa na huyo shetani wa Pwani WATAKUPOTEZA mama.

Nimetimiza wajibu wangu mama. Nimekwambia ukweli.

Nina mengi ya kukuambia, lakini nimejaribu kukupa hayo machache bila kumpa adui faida.

Nawasilisha kwako kwa unyenyekevu mkubwa, mheshimiwa rais.

Asante!

Ninja.
Umeongea kama KGB "James bond" Agent 007
 
Back
Top Bottom