Kwa mfano kila mwana JamiiForums mwakani ( 2025 ) wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu akipewa nafasi ya Kumuuliza Swali Rais Samia Wewe utauliza lipi?

Mamlaka ya rais wa Tanzania ni yetu sote sio ya samia peke yake Ila tukimvunjia Mh Rais Samia heshima tunaweka alama mbaya Sana.
 
Mbona kashakata pumzi za kuongoza jahazi, kwa nini mwakani asipumzike tu akalee wajukuu Kizimkazi
 
La Kwangu GENTAMYCINE nitaliweka mwishoni kabisa mwa Kurasa ya mwisho zitakazotokana na huu Uzi wangu hapa Ok?
Mhe Rais Dr Samia Suluhu Hassan, hongera sana kuwa Rais wa kwanza mwanamke kwa Afrika Mashariki.

1. Ulikuwa ni Makamu Mw/kiti wa Bunge la katiba iliyokuwa inapendekezwa na mchakato wake uligharimu taifa hela nyingi sana za walipa kodi, je kwa nini hadi sasa hujataka kuruhusu mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya, ambayo Watanzania wengi wanaitamani?

2. Wakati unaingia madarakani kama Rais rushwa ilikuwa kwa kiasi gani na kwa sasa umepambana nayo kwa kiasi gani?

3. Ulitumia vingezo vipi kukubali uwekezaji wa DPW kwenye bandari zetu huku wakiwa na changamoto na nchi km Somaliland, Djibouti nk?

4. Wakati unapokea uongozi deni la taifa lilikuwa kiasi gani na kwa sasa lipo kiasi gani?

5. Pamoja na kuendeleza miradi ya ya mtangulizi wako, wewe umeanzisha miradi ipi mikubwa mikubwa na umefikia wapi?

6. Ukiondoka leo madarakani watanzania watakukumbuka kwa yapi mazuri uliyowafanyia hasa wale wa vijijini?
 
Mhe Rais Dr Samia Suluhu Hassan, hongera sana kuwa Rais wa kwanza mwanamke kwa Afrika Mashariki.
1. Ulikuwa ni Makamu Mw/kiti wa Bunge la katiba inayopendekezwa na mchakato wake ulitumia hela nyingi sana za walipa kodi, je kwa nini hadi sasa hujataka kuruhusu mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya ambayo Watanzania wengi wanaitamani?
2. Wakati unaingia madarakani kama Rais rushwa ilikuwa kwa kiasi gani na kwa sasa umepambana, ana nayo kwa kiasi gani?
3. Ulitumia vingezo vipi kukubali uwekezaji wa DPW kwenye bandari zetu huku wakiwa na changamoto na nchi km Somaliland, Djibouti?
4. Wakati unapokea uongozi deni la taifa lilikuwa kiasi gani na kwa sasa lipo kiasi gani?
5. Pamoja na kuendeleza miradi ya ya mtangulizi wako, wewe umeanzisha miradi ipi mikubwa mikubwa na umefikia wapi?
6. Ukiondoa leo madarakani watanzania watakukumbuka kwa yapi mazuri uliyowafanyia hasa wale wa vijijini?
Kwa hilo Swali lako #4 naona kama vile unajitafutia tu matatizo nae.
 
Mimi nipo ndani ndani huku kwahiyo ningemuuliza kwenye huu uongozi wake amefanya lipi ambalo ni jipya kwa ajili ya wananchi wake? Nafahamu tu kuwa amejitahidi kukopa lakini sifahamu nitaomba kufahamishwa.

Hayati Magufuli yeye alibana matumizi kuendeleza secta mbalimbali

Ila ugali bado naupenda jamani 🥲
 
Nitamuuliza anajisikiaje kuongoza wananchi ambao hawamwelewi ??

Hivi bila wasanii unaweza kujaza hata nangwanda au gwambina stadium ??

Kwann mei mosi alijifungia chumbani akamtuma vice prsd..??
 
Back
Top Bottom