Huyo sio mzazi bora hafai kuwa tegemeo, inamaana sikukuu ingekuwa kesho, ndiyo ndiyo leo angeandaa hela ya mchele na hela ya viongo vya pilau, ninavyojua mimi ramadhani huchukua siku 30, 29 hivi na mwisho wake huja sikukuu, maandalizi ya sikuu ni lazma uanze nayo mapema. Wazizi wenzangu tujiandae mapema, inamaana huyo angepata dharula majuzi akasafiri mkoa, familia iingelala njaa kabisa, ndio maana watu huchukuliwa wake zao kwa uzembe. Kwa wenye watoto ambao huvarishwa nguo mpya kila sikukuu, baada ya sikukuu hii, anza maandalizi ya kununua nguo moja moja hivi sasa ili kukwepa kutumia hela nyingi kwa wakati mmoja kwa ajili ya sikukuu, hali inayopelekea mambo mengine huushindikana.