mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 20,015
- 49,153
Chakula ni sehemu ya utamaduni,ndio maana ukienda china unaweza kukuta wanakula konokono,nyoka kenge mamba nk ndio utamaduni wao
tangu nazaliwa miaka kadhaa baada ya yesu kuzaliwa huku kwetu uswahilini Tandika,Mbagala,Manzese ,Mwananyamala Tandale.siku za sikukuu za kidini iwe iddi,pasaka ,au krismasi lazima pilau lipikwe .ndio utamaduni wetu hauzuiwi kula pilau siku ambazo sio za sikukuu ila sikukuu kukosa pilau ni nje ya utamaduni wetu
Kwa mara ya kwanza kuna jirani zangu tena waislamu ambapo leo ndio sikukuu yao ila leo wamekula ugali kwa mara ya kwanza ,watoto wakambana baba akatoa sababu kuwa iddi imekuja ghafla mno walitarajia iwe kesho so watakula pilau keshosie watu wazima tukawa tumeshaelewa anamaanisha nini ,masikini watoto wamekula ugali na kesho huenda wakala tena ugali, kusema ukweli maisha yamekuwa magumu wafanya biashara wa kariakoo nao wanashangaa mauzo ya mwaka huu kipindi cha sikukuu yamevuja rekodi kwa kuwa chini