Kwa mara ya kwanza watazania wala ugali sikukuu ya iddi

kula kulala hawawezi kuelewa fasihi mpaka uwatafunie kila kitu,hali ni mbaya sikukuu utadhani msiba
kwani una miaka mingapi?....maana hayo mambo ni kawaida sana labda kama wewe ni wa "kishua" na hujawahi kutembea ndio utaona ajabu.
 
Chakula ni sehemu ya utamaduni,ndio maana ukienda china unaweza kukuta wanakula konokono,nyoka kenge mamba nk ndio utamaduni wao
tangu nazaliwa miaka kadhaa baada ya yesu kuzaliwa huku kwetu uswahilini Tandika,Mbagala,Manzese ,Mwananyamala Tandale.siku za sikukuu za kidini iwe iddi,pasaka ,au krismasi lazima pilau lipikwe .ndio utamaduni wetu hauzuiwi kula pilau siku ambazo sio za sikukuu ila sikukuu kukosa pilau ni nje ya utamaduni wetu
Kwa mara ya kwanza kuna jirani zangu tena waislamu ambapo leo ndio sikukuu yao ila leo wamekula ugali kwa mara ya kwanza ,watoto wakambana baba akatoa sababu kuwa iddi imekuja ghafla mno walitarajia iwe kesho so watakula pilau keshosie watu wazima tukawa tumeshaelewa anamaanisha nini ,masikini watoto wamekula ugali na kesho huenda wakala tena ugali, kusema ukweli maisha yamekuwa magumu wafanya biashara wa kariakoo nao wanashangaa mauzo ya mwaka huu kipindi cha sikukuu yamevuja rekodi kwa kuwa chini
Na wewe uache hiyo tabia ya kuchungulia majiko ya watu eti wamepika nini?
Yanakuhusu nini maisha ya watu? Mbona wewe hujasema ulipika nini?

Siku nyingine ukikosa kitu cha kufanya bora hata uwe unalala tu kuliko kuanza kunusa nusa majiko ya jirani zako.
 
Kwa iyo ni bora yule aliyesema hajui kwa nini waTanzania ni maskini??..
Tuwe na subra,mambo yatakaa sawa pilau izo itakua historia,mambo itakua ni biriani kwa kwenda mbele!
 
e1b9d004bdea4b6b5764fd8da44f8652.jpg
Nini hiyo mkuu ?
 
Hata cc tumekula ugali hata mm nashangaa maana mm ni mfanya biashara wateja wanqnunua soda ndoga za sh 500 na kuziona za sh 700 ni garama. Mchele na mafuta hayajatoka. Nipo Songea
 
Chakula ni sehemu ya utamaduni,ndio maana ukienda china unaweza kukuta wanakula konokono,nyoka kenge mamba nk ndio utamaduni wao
tangu nazaliwa miaka kadhaa baada ya yesu kuzaliwa huku kwetu uswahilini Tandika,Mbagala,Manzese ,Mwananyamala Tandale.siku za sikukuu za kidini iwe iddi,pasaka ,au krismasi lazima pilau lipikwe .ndio utamaduni wetu hauzuiwi kula pilau siku ambazo sio za sikukuu ila sikukuu kukosa pilau ni nje ya utamaduni wetu
Kwa mara ya kwanza kuna jirani zangu tena waislamu ambapo leo ndio sikukuu yao ila leo wamekula ugali kwa mara ya kwanza ,watoto wakambana baba akatoa sababu kuwa iddi imekuja ghafla mno walitarajia iwe kesho so watakula pilau keshosie watu wazima tukawa tumeshaelewa anamaanisha nini ,masikini watoto wamekula ugali na kesho huenda wakala tena ugali, kusema ukweli maisha yamekuwa magumu wafanya biashara wa kariakoo nao wanashangaa mauzo ya mwaka huu kipindi cha sikukuu yamevuja rekodi kwa kuwa chini
Inasikitisha sana !
 
Tulizoea kuletewa chakula chekwa chekwaa na majirani kama zawadi ya Idd, leo loooooo!!!!!, majanga. Hakuna kitu , hali ngumu! Kweli Magu amefunga mirija na njia zote!
Dah...ndiyo mkome kuzoea vya kunyonga bila jasho. Sasa acheni pereteperete ili mfanye kazi kwa bidii mtaona matunda yake :)

fb_img_1467814943308-jpg.363558
 
Safi sana ugali ndio chakula yetu ya asili .. Mtanyooka tu awamu hii.. Hapa kazi tu.
 
Back
Top Bottom