victormztz
JF-Expert Member
- Apr 6, 2015
- 1,111
- 614
Sababu kuu ni kuwa na wanajeshi wetu Congo yanayowapiga waasi wanafadhiliwa na Rwanda wakati huo huo tunajifanya marafiki wa Rwanda
Ni jambo lipi lilifanywa na Congo, likiashilia kuutilia mashaka uhusiano wa Tz na Rwanda? Hili ndio lilikuwa swali langu kwako, kwa mujibu wa post yako ya hapo awali, mkuu.
Pili, kama tatizo lilikuwa ni Kagame, mbona bado tuna uhusiano naye, sababu zilizomfanya Joseph Kabila aamue kurudisha ushilikiano na nasi ni nini, ikiwa hapo mwanzo ulidai ni Kagame?
Mimi siamini kama kutangulia kwa Kagame kuja Tz baada ya awamu ya 5 kuingia madarakani kuliashilia au kulilenga kutothamini mahusiano yetu na Congo.
Na hii dhana kwamba eti Congo ni muhimu zaidi kuliko Rwanda kwakuwa ina population kubwa sio sahihi kwani hata kile kidogo walichonacho Rwanda, bado tunakihitaji kwa maendeleo ya nchi yetu, kumbuka sio Tz pekee inayozifukuzia hizo fulsa kutoka Congo,ushindani ni mkubwa hivyo huwezi kujihakikishia kuwa nao miaka yote. Wote tunawahitaji kama ambavyo wanatuhitaji sisi.