Uchaguzi 2020 Kwa mambo haya 10, mimi kama Mtumishi wa Umma (mwalimu), John Pombe Magufuli sikupi kura yangu asilani

Najilaum sana kuipigia kura fisiemu 2015 saizi kura yangu inaenda chadema awe diwani simjui ,awe mbunge mdee rais ni lisu hii ndio kura yangu mmetutesa sana Ila muda wetu wa kuwatesa ni 28/10 saizi Niko tayari kufa sina Ila nitetee kura yangu
👏👏👏👏👏✌️✌️✌️🙏🙏🙏🙏
 
Siyo mwalimu huyo dalali tu, annual increment kila mwaka imekuwa ikiingia. Madaraja walimu tunaostahili tumepandishwa wale waliostahili kupandishwa halafu hawakupandishwa pasipo sababu walipolalamika maafisa utumishi waliwajibishwa.

Acha kudandia taaluma za watu mimi ni mwalimu niko pamoja na Magufuli.Jikite kwenye siasa zako siyo kuwasemea waalimu.
Wewe ni mwalimu au ni UVCCM tu uliyejivika koti la ualimu? Kama kweli wewe ni mwalimu, tuwekee check namba yako hapa ili tukuamini.
 
Nikuwekee check number yangu ya nini kama huamini endelea kuamini falsafa za kinyumbu kwamba ujenzi wa miundombinu, ununuzi wa ndege, ujenzi wa hospitali, vituo vya afya na zahati havina manufaa kwa watu.
 
Mimi naunga mkono hoja yako, maana katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria, lakini mambo yanavyokwenda hakuna haja ya kuuliza kuwa eti kuna mtu yupo juu ya sheria, maana kutomuongezea mtumishi mshahara hii tayari ni majibu tosha kuwa katiba ya nchi watu wameikalia.
 
siyo walimu tu. wakulima wa korosho, pamba, kahawa, wote wanalia. dawa ni moja.................... Wafanya biashara, wanafunzi waliomaliza vyuo bila ajira......
Wakulima wa korosho wamefanywa nini na wafanyabiashara na kikao kikaitishwa na Rais alafu ikawaje. Nasubiri Jibu.
 
Pamoja na kujipitisha mashuleni kutuomba kura za huruma, mie nimeamua kura yangu sitampa mgombea wa ccm kama nilivyofanya 2015 hii ni kutokana na mambo 10 niliyoyaona kipindi hiki cha miaka mitano

1. Makato ya bodi ya mikopo toka 8% hadi 15% bila sababu maalum tena kwa ubabe.

2. kutunyima nyongeza ya mshahara (annual increment) kwa miaka takribani mitano wakati ni haki ya msingi ya mtumishi.

3. Kutopandishwa daraja mwaka wa 6 huu unakwenda wa 7. Mie nimeajiriwa mwaka 2014 mwezi Aprili, mpaka leo Oktoba 2020 takribani miaka sita imepita huku nikilipwa mshahara wa TGTS D ambao ndio nilioanza nao mwaka 2014 na hata anayeajiriwa leo naye atalipwa hivyohivyo. Halafu wasanii wa bongo fleva wanatanua na kuchezea hela ya serikali kwenye kampeni zako.

4. Kutolipa hela ya likizo kwa wakati. Mfano mie likizo ya malipo nimeenda juni 2017 na juni 2019 JPM ukiwa madarakini, likizo zote nimesafiri toka Lindi hadi Mwanza bila kulipwa hata senti, mwaka huu ndio nimepewa hela ya likizo ya mwaka 2017 tena nusu tu.

5. Hela ya usimamizi wa mitihani ya Taifa kidato cha 4, 2 na 6 kutolipwa yote ya mwaka 2018 na 2019 huku siku za usimamizi (za malipo) kwa wataalamu wa maabala zikishushwa kuanzia mwaka huu toka siku 6 hadi moja.

6. Sheria mpya ya wastaafu ambayo umejifanya Kuibatilisha hadi 2022 ni geresha tu kupisha uchaguzi mkuu huu ufanyike na baada ya hapo kikokotoo kipya kianze kazi. malipo ya mkupuo kwa wastaafu (Lumpsum) kwa Kikokotoo kipya kinataka mstaafu apewe 25% ya mafao yake yote, na 75% zinazobaki apewe kidogokidogo hadi kufa kwake mfano milioni 100 upewe milioni 25 halafu milioni 75 nilipwe kidogokidogo. Mie kama mtumishi hii kwangu haiingii akilini na ili isiniumize ni kukunyima tu kura yangu.

7. Ulituahidi Laptop kila mwalimu 2015 lakini muda wako wa awamu ya kwanza unaenda mwishoni bila dalili yoyote ya kupewa hiyo Laptop.

8. Uzalilishaji unaofanywa na wateule wako kama Ma-RC na ma-DC mbele ya wanafunzi wetu na wewe umekuwa kimya. Mfano kutulazimisha kulala kwenye mwenge tena kwa kuitwa majina kama watoto.

9. Ninachangia bima ya afya (3%) kila mwezi halafu dawa za muhimu zimeondolewa na unapoenda hospitali tunalazimika kujinunulia kwa hela yetu.

10. Sababu za Kutoa kufundisha walimu wa masomo ya sanaa wa sekondari kwenda shule za msingi ni za ajabu sana.
hahahaaa ndio umejitahidiiii kuorodhesha...kwani kama hizo zote ni kero sasa si uache hiyo kazi uje huku kitaa uone kama hujarudi faster? Wewe ukiona kazi mbaya na haina maslahi kwako achana nayo. Hivi unajua kuna kina mama mtaani wanatembeza mboga na mtoto mgongoni na jua kali na faida kwa siku haifiki hata buku 3? Leo wewe nyau unalilia hela ya likizo kwani ulipoomba kazi kazi hukujua utatakiwa kurudi kwenu? Acha kazi kama mbaya.
 
ndio maana hatampa kura magu
 
Pamoja na kujipitisha mashuleni kutuomba kura za huruma, mie nimeamua kura yangu sitampa mgombea wa ccm kama nilivyofanya 2015 hii ni kutokana na mambo 10 niliyoyaona kipindi hiki cha miaka mitano

1. Makato ya bodi ya mikopo toka 8% hadi 15% bila sababu maalum tena kwa ubabe.

2. kutunyima nyongeza ya mshahara (annual increment) kwa miaka takribani mitano wakati ni haki ya msingi ya mtumishi.

3. Kutopandishwa daraja mwaka wa 6 huu unakwenda wa 7. Mie nimeajiriwa mwaka 2014 mwezi Aprili, mpaka leo Oktoba 2020 takribani miaka sita imepita huku nikilipwa mshahara wa TGTS D ambao ndio nilioanza nao mwaka 2014 na hata anayeajiriwa leo naye atalipwa hivyohivyo. Halafu wasanii wa bongo fleva wanatanua na kuchezea hela ya serikali kwenye kampeni zako.

4. Kutolipa hela ya likizo kwa wakati. Mfano mie likizo ya malipo nimeenda juni 2017 na juni 2019 JPM ukiwa madarakini, likizo zote nimesafiri toka Lindi hadi Mwanza bila kulipwa hata senti, mwaka huu ndio nimepewa hela ya likizo ya mwaka 2017 tena nusu tu.

5. Hela ya usimamizi wa mitihani ya Taifa kidato cha 4, 2 na 6 kutolipwa yote ya mwaka 2018 na 2019 huku siku za usimamizi (za malipo) kwa wataalamu wa maabala zikishushwa kuanzia mwaka huu toka siku 6 hadi moja.

6. Sheria mpya ya wastaafu ambayo umejifanya Kuibatilisha hadi 2022 ni geresha tu kupisha uchaguzi mkuu huu ufanyike na baada ya hapo kikokotoo kipya kianze kazi. malipo ya mkupuo kwa wastaafu (Lumpsum) kwa Kikokotoo kipya kinataka mstaafu apewe 25% ya mafao yake yote, na 75% zinazobaki apewe kidogokidogo hadi kufa kwake mfano milioni 100 upewe milioni 25 halafu milioni 75 nilipwe kidogokidogo. Mie kama mtumishi hii kwangu haiingii akilini na ili isiniumize ni kukunyima tu kura yangu.

7. Ulituahidi Laptop kila mwalimu 2015 lakini muda wako wa awamu ya kwanza unaenda mwishoni bila dalili yoyote ya kupewa hiyo Laptop.

8. Uzalilishaji unaofanywa na wateule wako kama Ma-RC na ma-DC mbele ya wanafunzi wetu na wewe umekuwa kimya. Mfano kutulazimisha kulala kwenye mwenge tena kwa kuitwa majina kama watoto.

9. Ninachangia bima ya afya (3%) kila mwezi halafu dawa za muhimu zimeondolewa na unapoenda hospitali tunalazimika kujinunulia kwa hela yetu.

10. Sababu za Kutoa kufundisha walimu wa masomo ya sanaa wa sekondari kwenda shule za msingi ni za ajabu sana.
Kama kweli we ni mwalimu,hakika wanetu wana hasara.
Mwalimu usiejua tofauti ya
Dhalilisha na zalilisha!!

Sent from my TECNO-C7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom