Mimi hapo nyuma nimewahi kuuliza kuna umuhimu gani wa kuomba ridhaa Ikulu kwa hukumu iliyotolewa na mahakama?! Mahakama ikihukumu mtu kunyongwa kwanini sheria ilazimishe hadi idhini ya rais ndiyo hukumu itekelezwe? Huku si kuingilia uhuru wa mahakama?!Jana mkuu kasema hatatekeleza adhabu ya kunyongwa kwa watu walopewa hukumu hiyo, sasa nashauri sheria hii ifutwe badala ya kila anayekuja kuipotezea... ugumu uko wapi kuifuta sheria hii?
Swali lako ni valid... ngoja wajuzi wa mambo watuelezeeMimi hapo nyuma nimewahi kuuliza kuna umuhimu gani wa kuomba ridhaa Ikulu kwa hukumu iliyotolewa na mahakama?! Mahakama ikihukumu mtu kunyongwa kwanini sheria ilazimishe hadi idhini ya rais ndiyo hukumu itekelezwe? Huku si kuingilia uhuru wa mahakama?!
Hawa wahalifu wanaosubiri kunyongwa ni mzigo kwa taifa maana hawafanyi kazi yoyote gerezani. Ni kula na kulala.
Lakini hata watangulizi wake wamekuwa wanakwepa. Lakini pia , je kuna mtu ana hiari ya kutekeleza sheria?Amezuia utekelezaji wa sheria hiyo kwa kipindi chake lakini huenda labda atakaemfuatia akaitumia. Hivyo unaposema ifutwe sio sawa.
Kila mmoja anakwepa kuonekana yeye ndio kaua.Lakini hata watangulizi wake wamekuwa wanakwepa. Lakini pia , je kuna mtu ana hiari ya kutekeleza sheria?