Kwa kuwa sheria ya kunyongwa hadi kufa haitekelezwi, kwanini isifutwe?

sem2708

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,604
2,000
Jana mkuu kasema hatatekeleza adhabu ya kunyongwa kwa watu walopewa hukumu hiyo, sasa nashauri sheria hii ifutwe badala ya kila anayekuja kuipotezea... ugumu uko wapi kuifuta sheria hii?
 
Emiir

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
25,656
2,000
Amezuia utekelezaji wa sheria hiyo kwa kipindi chake lakini huenda labda atakaemfuatia akaitumia. Hivyo unaposema ifutwe sio sawa.
 
Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
9,103
2,000
Jana mkuu kasema hatatekeleza adhabu ya kunyongwa kwa watu walopewa hukumu hiyo, sasa nashauri sheria hii ifutwe badala ya kila anayekuja kuipotezea... ugumu uko wapi kuifuta sheria hii?
Mimi hapo nyuma nimewahi kuuliza kuna umuhimu gani wa kuomba ridhaa Ikulu kwa hukumu iliyotolewa na mahakama?! Mahakama ikihukumu mtu kunyongwa kwanini sheria ilazimishe hadi idhini ya rais ndiyo hukumu itekelezwe? Huku si kuingilia uhuru wa mahakama?!

Hawa wahalifu wanaosubiri kunyongwa ni mzigo kwa taifa maana hawafanyi kazi yoyote gerezani. Ni kula na kulala.
 
sem2708

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,604
2,000
Mimi hapo nyuma nimewahi kuuliza kuna umuhimu gani wa kuomba ridhaa Ikulu kwa hukumu iliyotolewa na mahakama?! Mahakama ikihukumu mtu kunyongwa kwanini sheria ilazimishe hadi idhini ya rais ndiyo hukumu itekelezwe? Huku si kuingilia uhuru wa mahakama?!

Hawa wahalifu wanaosubiri kunyongwa ni mzigo kwa taifa maana hawafanyi kazi yoyote gerezani. Ni kula na kulala.
Swali lako ni valid... ngoja wajuzi wa mambo watuelezee
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom