Kwa Kumuondoa Makamba CCM Wamejimaliza

The Prophet

JF-Expert Member
Mar 17, 2011
682
94
Makamba alikuwa anaweza kuitetea CCM kwa maneno yoyote aliyotaka yatoke kinywani mwake pale alipopewa nafasi ya kufanya hivyo. Ilifika wakati msambaa huyu alipinda mdomo kwa sababu ya kuzungumza maneno mengi kuliko mtanzania yeyote, akiitetea CCM.

Sitarajii kama timu hii ya kina Chiligati, Nape na Mukama wataweza muziki wa mtu aliyekuwa na ubavu wa kupakia omba-omba wote kwenye karandinga na kuwarudisha makwao. hakuna anayeweza kumfikia.

Chiligati hawezi kuzungumza bila kusoma notebook.

Nape anaweza kuzungumza bila notebook, lakini hana ushawishi kwa audience. akizungumza sentensi moja au mbili, akiweka nukta ukatafakari, unagundua kuwa hukumbuki ameonge nini.

Mukama ndo hovyo kabisa. Upara wake tu ni tatizo. Yaani mtu akiona ule upara wa Mukama, hata hamu ya kumsikiliza inamtoka. Hata yeye(mukama) anajua kama upara wake ni tatizo maana hawezi kupanda jukwaani bila kofia, na muda mwingi anafanya kazi ya kuficha upara kuliko kutoa hoja.

CCM wana-changamoto moja au mbili:

Ama wamrudishe Makamba kwenye ukatibu-mkuu, vinginevyo wamekwisha.

Ama waunde timu nyengine. Hii timu yao ya sasa inayozunguka mbuyu watu wote wanajua ni timu pandikizi, imepandikizwa kwa ushauri mbovu wa 'waziri mkuu mstaafu', na hakika CCM haitapona!!

take my words. time will tell.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom