Kuanguka haraka kwa CCM na Hatari inayolikumba Taifa hivi sasa!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Ni asubuhi na mapema, anga likiwa na makunyanzi,huku magimbi yakitanza kwa ukelele na rangi ya kahawia inalitanda anga,

Nyuso za magwiji wa falsafa za mlengo wa kati na hekima ya utawala wa nera zimeshamiri tabasamu mwanana kabisa,

Ndio ni tarehe ileile ya 05/02/1977 siku tukufu kwa wahafidhina wa CCM, nasema ni tukufu kwakuwa wazalendo wa leo hawaamini kuwa ungano lile la saa nne mchana wa 05/02/1977 leo ndilo hili walionalo leo!

Chama cha TANU kikiwa na nguvu thabiti na kikiwa ni miongoni mwa vyama vyenye nguvu barani Afrika, kiliamua kwa kauli moja kuungana na Chama cha Kizalendo/cha weusi ambacho ni kikongwe zaidi barani Afrika cha ASP,

Hilo lilitimia baada ya Muungano wa nchi mbili huru yani Tanganyika iliyopata Uhuru chini ya Shujaa wake Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Zanzibar iliyopata uhuru wake kupitia MAPINDUZI matukufu chini ya Shujaa wake John Okello (Fiel Marshal) lakini kipindi cha muungano Zanzibar ilikuwa chini ya Sheikhe Karume mkubwa,

Ni zama ambazo bara la Afrika lilishuhudia chama cha siasa imara kikizaliwa katika ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara katika ardhi ya Tanzania mpya, chama kilichokuwa na nguvu ya kiushawishi, nguvu ya kiuchumi, na nguvu ya kijasusi!

Chama ambacho kwa msaada wacho kiliyaweka huru mataifa yote ya kusini mwa Afrika, hakuna nchi ya kusini mwa Afrika ambayo haikupita mikono mwacho, laa isingepata uhuru kwa wakati!

Si chama kingine bali ni mvumo wa alama ya kijani na njano, tokezo sahihi la Chama Cha Mapinduzi!

Kwa uimara wake, Tanzania palikuwa mahali pa sauti kuu ya mwafrika, Tanzania ilikuwa na SAUTI mbele ya UNO juu ya mambo mengi hasa UHURU kamili wa Mwafrika,

Kuingia kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa hasa baada ya kupigwa mweleka kwa Azimio la Arusha mwaka 1992 na kuzaliwa Azimio la Zanzibar, kulileta mageuzi mapya ya chama hii,

Sura na hadhi ya chama ilizidi kutia nyongo miongoni mwa wahafidhina hasa baada ya mabaka uchumi kujitwalia sauti na nguvu ya chama,

Lakini magwiji wa siasa zile walipotangulia tu mbele ya haki, mizani ya chama hii imekuwa ikipinda siku hadi siku,

Uchaguzi wa 2010 ulikuwa ni taswira halisi ya chama kubakwa, na wabakaji walidhamiria hasaaa na wamefanikiwa, mabaka uchumi yaliamua kuchota pesa hazina ya serikali (ya wanachi) na kutumbukiza katika uchaguzi huo yakipanda mtu wao wakulinda maslahi yao,

Hakika yalifanikiwa, pesa ilichotwa kupitia mlango uitwao EPA, na yakamuweka mnadhiri wao Ikulu, na hakika maslahi yao yanalindwa kama yalivyo maagano yao!

Hilo liliendelea kuwa angamizo kwa chama adhimu cha CCM, kwa mpasuko ndani yake uliendelea kuongezeka huku chama kikiacha majukumu yake stahiki na kugeuka KAMPUNI la biashara,

Bahati mbaya iliyoje kwa ccm, kwani licha ya kugeuzwa mgodi wa wajanja, bado kiliendelea kukubwa na dhahama ya karne hasa kwa chama kugeuka kuwa NGOs ya familia ya Mwenye Jamuhuri, Baba kashika Jumuiya ya Wazazi, Mama kashika Umoja wa Wanawake, na Mtoto kashika Umoja wa Vijana,

Hakika hapa wahafidhina ndipo walipokamatwa, hakuna pakufurukuta kata kugeuza ukope tu, ukitibuana na The Princess ujue umetibuana na Mwenye Jamuhuri, na ukitibuana na Bimkubwa ujue hulambi unga hata cheme ya haradali,

Mungu wangu!, huenda ndio kifo kiliita ccm yangu,

Kibaya zaidi mwenye kiti wa chama aliamua kupanga safu yake ya Uongozi baada ya Uchaguzi wa 2010 kwa kumpiga chini Yusufu Makamba na kuleta sura azitakazo ambazo kimsingi zingemsikiliza matakwa yake, naaam aliingia bingwa wa falsafa za kale za Kingwanamalundi, huyu kwa asili ni mtaalamu wa njama za siri na ni jasusi muhitimu mikononi mwa Julius Nyerere kama aliyo Yusufu Makamba, tofauti yao ni moja tu, Mkama ni mtaalamu wa mikakati ya siri aliyefuzu mafunzo ya kijasusi ipasavyo, Yusufu Makamba ni mtaalamu wa ujasusi wa kipropaganda aliyebobea na kuiva ipasavyo kutoka Mosco,

Katika siasa za leo huku chama kikizidi kutoweka mioni mwa Watanzania, Chama kilihitaji mtaalamu wa propaganda aliyebobea ipasavyo, na kilihitaji mtaalamu wa njama za siri mwenye kutembea katika lengo mahususi,

Lakini kumtoa Makamba na kumuweka Mkama lilikuwa kosa la karne, kwakuwa chama kilikuwa kwenye mfumo wa Analogi na kilihitaji kuingia katika mfumo wa Digitali ambamo vyama makaini vya mageuzi ya pili vimo,

Kama vile mungu ameandika kifo kwa ccm mikononi mwa Jakaya Kikwete kabla ya 2015, chama kilifanya mabadiliko tena ya uongozi na kurudisha "makapi" ya kale na si mwingine ni Abdulahiman Kinana mtanzania mwenye ASILI ya "KIGENI" RAIA wa Somalia,

Malengo ya mwenyekiti ni kutumia taaluma ya Kijasusi ya Kinana katika siasa mpya, lakini akisahau kuwa filosofia ya Kinana na Mkama ni moja kasolo hulka zao tu,

Kinana amekuja na aina mpya ya siasa za Tanzania, hasa kwa kuruhusu na kushinikiza vyombo vya Dola kutawala siasa za CCM, leo mwanaccm hawezi kuzungumza chochote bungeni bila kupewa maelekezo na Idara za Usalama za nchi,

Lakini hilo tisa, kumi ni pale chama kilipowaingiza vijana ambao hawajapevuka kiakili katika uongozi wa juu wa chama, lengo la CCM lilikuwa zuri sana kama lingelenga watu sahihi katika nafasi hizo kwakuwa hawa wangekuwa ni kiungo kati ya kundi la vijana nchini ambalo ndilo linalotawala karibu 98% ya wahanga na waamuzi wa siasa za nchi hii, Watu hao si wengine bali ni Mwigulu Nchema na Ndugu Nape Nnauye,

Hawa kwa political meker wa ccm alilenga kuwa wawe kiunganishi cha vijana wa Kitanzania, lakini matakwa na chaguo la Mwenye Jamuhuri ni ANGAMIZO kwa CCM na kwa NCHI kwa ujumla,

Wamegeuka kuwa ni maadui wa vijana wa kitanzania, hata wale vijana ambao hawakuwa na uamuzi wa haraka wa kuamua waende chama gani cha siasa wamejikuta wanaichukia CCM hata kabla hawajaamua pakwenda,

Leo taifa limesimama wima linastaajabu kuona ccm imeamua kutawala kwa damu dhahiri shahiri, siasa za majukwani na vitendo vya vijana hawa Mwigulu na Nape vinaliyumbisha taifa, wamekuwa na mamlaka makuu kuliko hata mwenye Jamhuri, wanaamrisha vyombo vya dola watakavyo,

Mauaji yametabakaa kila kona ya nchi, na yote chanzo ni siasa za nchi hii, manyanyaso kwa vyama vya upinzini yamekomaa kiasi cha kutishia usalama wa taifa hili hivi sasa, lakini yote haya ni ni siasa za majukwani za ccm kushindwa kushawishi Watanzania na sasa Watanzania wanalazimishwa kwa mtutu wa bunduki kuikubali ccm na maovu yake yote!

Bahati nzuri watanzania wanasema wazi hapanaaaaa! Hawataki siasa za damu, hawataki kumpenda mtu kwa lazima, hataki kudanganywa tena, hawataki raslimali zao kuibwa tena,

Wataka huduma bora na maisha bora huku raslimali zao kikilinufaisha taifa na vizazi vyao vya kesho!


Taifa linayumba kwa siasa CHAFU za CCM, tumekuwa kituko mbele ya uso wa dunia, taifa linanuka DAMU ya binadamu, taifa linaomboleza kila uchao,

Lakini waratibu na wauaji tunao mitaani, serikali haichukui hatua, na zaidi inabariki kwakusema "wapigini tu tumechoka"


Kwa muktadha huo chama cha cha siasa chenye mlengo wa fikra za mageuzi ni Chadema, na kimefanikiwa kubeba tumaini la Watanzania karibu wote, labda tu wale wahafidhina vipofu wa ccm!


Watanzania wanao uchaguzi wao wenyewe, wakuamua ama kuishi katika damu ama kuishi katika ukombozi mpya,

Mwenye macho haambiwi tazama!
 
Ebu upitie tena huu uzi na uufanyie marekebisho maneno mengi hayako sawa,kwa mfano "mawingu" unaita "Magimbi"
 
Mkuu umenena vema,kikubwa tujiandae kisaikolojia kwa haya ambayo ccm wanayotutendea tena kasi ya ajabu.wacha wtupige,wacha watubambikizie kesi,wacha watuue lakini amini amini nawaambieni ukombozi lazima utapatikana tu,watake wasitake mabadiliko yanakuja tu.najua watatufunga sana lakini ni suala la wakati tu na watufunge tu.
 
Hilo lilitimia baada ya Muungano wa nchi mbili huru yani Tanganyika iliyopata Uhuru chini ya Shujaa wake Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Zanzibar iliyopata uhuru wake chini ya Shujaa wake John Okello (Fiel Marshal) lakini kipindi cha muungano Zanzibar ilikuwa chini ya Sheikhe Karume mkubwa,
Zanzibar ipi ilipata uhuru wake chini ya Okello? Unatakiwa kuisoma upya historia ya visiwa hivi.....
 
Mkuu umenena vema,kikubwa tujiandae kisaikolojia kwa haya ambayo ccm wanayotutendea tena kasi ya ajabu.wacha wtupige,wacha watubambikizie kesi,wacha watuue lakini amini amini nawaambieni ukombozi lazima utapatikana tu,watake wasitake mabadiliko yanakuja tu.najua watatufunga sana lakini ni suala la wakati tu na watufunge tu.

Hilo ndilo linalotupa nguvu zaidi sisi wahafidhina wa ukombozi
 
Oooho karibu sana dada, ukiona nimenyanyua kalamu na kuandika hayo ujue nimeandika kilichosahihi,

Omba msaada nikujuze ujue zaidi historia ya Zanzibar
Ina uhakika mimi ni dada au unakurupuka tu kama ulivyokurupuka na kusema uhuru wa Zanzibar ilkuja chini ya Okello?! Ni usahihi gani ulionao wakti umeanika uongo?! Ukweli uliopo ni kwamba uhuru wa Zanzibar haukuja chini ya Okello bali Okello alihusika kwenye mapinduzi ya Zanzibar April 1964 wakati uhuru ulipatikana December 1963!! Watu wasioijuwa historia huwa wanachanganya kati ya mapinduzi ya zanzibar na uhuru wa Zanzibar......haya sasa, umejitapa kwamba unachoandika unakuwa na uhakika nacho, sema hapa Uhuru huo wa Zanzibar chini ya Okello ulipatikana lini!!!!
 
Marekebisho Kidogo maana Zanzibar imepata uhuru tarehe 10 Disemba, 1963 chini ya Baba wa Taifa la Zanzibar Marehemu Mohammed Shamte na baadae kufuatiwa na Mapinduzi ya tarehe 12 January, 1964
 
Zanzibar ipi ilipata uhuru wake chini ya Okello? Unatakiwa kuisoma upya historia ya visiwa hivi.....

Makosa madogo, sasa tu-deal na content ya makala yake...yuko sahihi kabisa...change is a non reversible process, CCM wakubali mabadiliko na waheshim mawazo ya watanzania,serikali haipaswi kuwalazimisha watanzania kuipenda ccm na iheshimu siasa za vyama vingi,vinginevyo wananchi tutaichukia ccm kuliko sasa na amani itapotea, hata hivo ccm haina hati miliki ya taifa hili. TUTABAKI KUWEKA WASIWASI JUU YA NGUVU KUBWA INAYOTUMIWA NA CCM KU-supress nguvu ya vyama vya upinzani na demokrasia in general...
 
Zanzibar ipi ilipata uhuru wake chini ya Okello? Unatakiwa kuisoma upya historia ya visiwa hivi.....
Kitu kama hukijui omba wenye uelewa wakuelimishe wala si vibaya, hata mimi miaka ya nyuma niliamini kabisa Mapinduzi yaliongozwa na Karume kumbe si kweli.

Kaa karibu au wasiliana nao hata kwa Email waandishi wa makala wenye weledi mkubwa kama Joseph Mihangwa watakuelimisha na utaijuwa kweli.
 
Makosa madogo, sasa tu-deal na content ya makala yake...yuko sahihi kabisa...change is a non reversible process, CCM wakubali mabadiliko na waheshim mawazo ya watanzania,serikali haipaswi kuwalazimisha watanzania kuipenda ccm na iheshimu siasa za vyama vingi,vinginevyo wananchi tutaichukia ccm kuliko sasa na amani itapotea, hata hivo ccm haina hati miliki ya taifa hili. TUTABAKI KUWEKA WASIWASI JUU YA NGUVU KUBWA INAYOTUMIWA NA CCM KU-supress nguvu ya vyama vya upinzani na demokrasia in general...
Tuendelee na mjadala, ilikuwa ni point of correction kwani mwenyewe bado anaamini alichokaindika ni sahihi,,,,lazika tusahihishane yanapotokea makosa ya kiufundi; maandiko yanasomwa na wengi! In fact, hata kama angeendelea kunga'ang'ania nilishapanga kuachana nae ili mada isije kuwa diverted lakiini ni muhimu kwetu kuwa na uhakika kwa kila tunachokiandika!
 
Marekebisho Kidogo maana Zanzibar imepata uhuru tarehe 10 Disemba, 1963 chini ya Baba wa Taifa la Zanzibar Marehemu Mohammed Shamte na baadae kufuatiwa na Mapinduzi ya tarehe 12 January, 1964


Jibu kwa NasDaz

Nikweli hujakosea nimekuta dada kutokana na ninavyokufahamu kupitia hapa jf hasa katika mada ambazo mimi nimewahi kujadiliana na wewe,

Yap kile unachoamini ulikuwa ni uhuri wa Zanzibar hakikuwa kwa Wazanzibar bali kwa Sultan Jamushd,

Uhuru kamili wa Zanziba uliletwa kwa mapinduzi matakatifu chini ya Field Marshal John Okello akiongoza jeshi la wazalendo weusi!

Usidanganyike na propaganda zilizofanywa baada ya Okello kukabidhi madaraka kwa Karume, zilikuwa na lengo la kufuta kile wao walichokiita aibu, lakini historia huwa haibadilishwi hata kwa chembe ya haradari!

Okello anabaki kuwa ndie baba wa taifa la Zanzibar,

Abdulahman Babu alipewa kazi ya propaganda za kufuta ukweli lakini ilishindikana!
 
mkuu Yericko, hapo umenena vyema... umeanza kama historia na matatizo ya ccm mpaka kufikia kuchokwa na wananchi.

halafu mwishoni haukuacha watu wana hang ukaja na suluhisho, ukatoa solution kipi kifanyike, ni watu kujiunga kwenye ukombozi...

ccm kwa sasa haina inshu, lakini sidhani watu kama zomba wanalielewa hilo...
 
Last edited by a moderator:
Kitu kama hukijui omba wenye uelewa wakuelimishe wala si vibaya, hata mimi miaka ya nyuma niliamini kabisa Mapinduzi yaliongozwa na Karume kumbe si kweli.

Kaa karibu au wasiliana nao hata kwa Email waandishi wa makala wenye weledi mkubwa kama Joseph Mihangwa watakuelimisha na utaijuwa kweli.
Mkuu Matola, tuiache hii mada ili tusije tukabadilisha mjadala! Hata hivyo, kabla hatujaacha naomba nikuambie umejichanganya kama alivyojichanganya mleta mada! Okello alihusika kwenye mapinduzi na sio uhuru....wengi wanachanganya kati ya uhuru wa zanzibar na mapinduzi ya zanzibar...hivi ni vitu viweli tofauti! Uhuru wa zanzibar ulipatikana December 1963 kutoka kwa Waingereza wakati a,bacho alihusika Okeelo ni Mapinduzi ya Zanzibar April 1964, mapinduzi ambayo yaliiangusha serikali iliyokuwa inaongozwa kwa pamoja kati ya ZNP na ZPPP, maarufu kama serikali ya Sultani!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom