GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,554
- 108,896
Kuna Watu mmenishangaza kweli kweli kwa Hoja yenu kwamba inawezekana vipi Yanga SC kutaka Kuhonga Tsh Milioni 40 wakati hata Kombe lenyewe halina Kiasi kikubwa cha Pesa?
Kitu pekee ambacho wengi wenu ( hasa Wanafiki ambao ni wana Yanga SC ) ni kwamba tayari Yanga SC imeshajua kuwa katika Ligi Kuu ya VPL mbele ya Simba SC hawana chao tena.
Hivyo basi ili Uongozi wa Yanga SC na hasa hasa Wadhamini wao GSM kupitia Injinia Hersi ( ambaye aliwaaminisha wana Yanga ) kuwa iwe isiwe mwaka huu Yanga SC ni Bingwa wa VPL na isipokuwa basi aulizwe Yeye.
Katika hali ya Kutuliza Presha wanachokifanya sasa GSM kupitia Injinia Hersi ni kutumia Gharama yoyote ( hasa ya Rushwa ) ili angalau Yanga SC iweze kufika mbali katika Kombe la ASFC ( FA ) na ikiwezekana ichukue Ubingwa ili wawe na Kitu cha Kujitetea na Kutuliza Presha za Mashabiki wao ambao wameshakata tamaa sasa.
Na kingine kinachowatesa Yanga SC sasa na ndiyo maana hata wanahangaika Kuhonga hivi ni kwamba wameshajua kuwa Msimu ujao Tanzania inaingiza Timu Nne ( 4 ) hivyo kwa kutokutaka Aibu hiyo ya Kubebwa na Mafanikio ya Simba SC na Namungo FC wanahaha ( wanahangaika ) mno wabebe Kombe la ASFC ili wawe wamejibeba wenyewe Kimataifa na isiwe wamebebwa na Mtani wao wa Jadi Simba SC.
Nikiwa kama Mdau mkubwa tu wa Michezo ( hasa Soka la Tanzania ) sijakubaliana na Kauli ya Kihuni na isiyo ya Kiungwana na Uanamichezo iliyotolewa na Nahodha wa Prisons FC Benjamin Asukile na ningemshauri Yeye binafsi pamoja na Uongozi wa Prisons FC upesi sana utuombe Radhi ( Msamaha ) Sisi Wadau wa Michezo na hata Watanzania wote kwa Ujumla.
Kuhusu Tuhuma aliyoitoa ya Wao ( Wachezaji ) wa Prisons FC kutaka Kuhongwa na Yanga Tsh Milioni 40 hizo GENTAMYCINE nakubaliana nae tena kwa 100% kutokana na kwamba nipo katika Mpira wa Tanzania ( Bongo ) na Michezo hii ya Hatari nimeshawahi Kuishuhudia binafsi na hata baadhi ya Wachezaji Waandamizi wa Vilabu Vikubwa nchini ambao ni Marafiki zangu wameshawahi kuniambia hili.
Tatizo lenu wengi wenu hapa JamiiForums hamtunzi Kumbukumbu ila mwaka Jana nakumbuka GENTAMYCINE niliwahi Kuandika Uzi kuwa Mchezaji Swedi aliyekuwa akichezea Klabu yake ya Kagera Sugar ( Kocha akiwa Rafiki yangu Mecky Maxime ) iliyocheza na Yanga SC katika Ligi Kuu Kipindi cha Kwanza waliibania Yanga SC vilivyo.
Walipoenda Mapumziko waliambiwa na Mmoja wa Kiongozi wao kuwa Miamala yao imesoma tayari hivyo wakiingia wasibane ( wasikaze ) tena na kweli wao hawakufanya hivyo na kweli Yanga SC ikashinda Mechi hiyo.
Baada ya Mechi hiyo Kumalizika na Yanga SC kushinda Mchezaji Swedi alipowasha Simu yake ili aangalie Salio la Hela waliyoahidiwa na Yanga SC akakuta Yeye hajawekewa ndipo kwa Hasira Kesho yake akapanda Basi na kuja Dar es Salaam na hadi Kuamua kuachana pia na Soka la Tanzania.
Nina Mwamuzi Mmoja Rafiki yangu ( anatokea Jeshini ) Wiki Mbili tu zimepita aliwahi kuniambia kuwa amewasikia Waamuzi kadhaa wa Ligi Kuu wakisema kuwa TFF watawafungia sana tu ila Wao wakipewa Hongo ( Rushwa ) kutoka Azam, Simba na Yanga kuanzia Tsh Milioni 20 mpaka 30 ili wawabebe ( wawapendelee ) hawatoziacha kwani hata wao pia wana Shida na Familia zao pia.
Na mwisho naomba bila Unafiki katika hili GENTAMYCINE nisiiseme tu Yanga SC na niseme tu ukweli ( japo najua kuna Watu nitawakera kwakuwa ni Mwenzao ) kuwa hata Sisi Simba SC ( Timu yangu pendwa ) Michezo hii tunaifanya ( tunaicheza ) sana hivyo Simba na Yanga ni tatizo kubwa la Maendeleo ya Soka la Tanzania.
Na kama kuna Mtu ambaye nawaombeni mkipata muda nendeni mkamuulize juu ya Upangaji wa Matokeo na kusumbuliwa na Vilabu vya Azam, Simba na Yanga ni aliyekuwa Kocha wa Kagera Sugar ( zamani Mtibwa Sugar ) Kocha Mecky Maxime kwani kwa hili Yeye ni Mhanga sana.
Rushwa katika Soka la Tanzania ipo tu.