Icon wa Bongo flava Naseeb ‘Diamond’ Abdul, amewashangaa wasanii wanaomtupia maneno kila kukicha kuwa anawabania wasanii wengine ‘connections’ za kung’ara kimataifa.
Akizungumza na TBC juzi, Platnumz amesema anasikitishwa sana na maneno hayo ilhali anafanya juhudi kubwa kujitafutia na kuwatafutia wasanii wengine masoko ya kimataifa.
“Mi nashangaa sana kusikia hayo maneno, wanasema hivyo wakati mi najitahidi kuwasaidia wenzangu tutoboe wote, kila kolabo ya msanii wa nyumbani na msanii wa Nigeria inayofanywa mi ndo huwa nasababisha.” alisema Diamond
“Nikiamua kubana mbona naweza tu, kwa sababu vituo vingi vya nje vinanisikiliza kwa mfano tu MTV wenyewe wakipokea video ya msanii yoyote kutoka hapa (Tanzania) wananipigia wananiuliza kwanza huyu vipi? tuicheze ngoma yake au? mi huwa nasema tu anafanya vizuri huku, basi inapita wanaicheza nikiamua kubana si naweza tu?”
Katika ‘line’ nyingine, baba Tiffah amesema timu yake ya Wasafi ndiyo iliishauri kituo cha tv cha Nigeria Sound City na MTV kuanzisha chati za Afrika Mashariki kwenye vituo hivyo.
Chanzo: Timesfm