Hongera Diamond kwa mtazamo mwema juu ya Kiba na Harmonize. Huu ndio uungwana

Kibumbula

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2018
Messages
3,462
Points
2,000

Kibumbula

JF-Expert Member
Joined Mar 26, 2018
3,462 2,000
Hakika umeonesha utu,hata kama una mapungufu yako.Sisi sote tunayo mapungufu.

---
Diamond Platnumz amezungumzia kilichoandikwa na msanii mwenzake, Ali Kiba katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram saa chache baada ya kumualika kushiriki tamasha la Wasafi litakalofanyika Novemba 9, 2019.

Akizungumza jana Ijumaa Novemba Mosi, 2019 katika televisheni ya Wasafi nyota huyo wa kibao cha “Number One” amesema hakujua Ali Kiba alilenga nini, akibainisha kuwa hawezi kuwa na chuki naye.

Diamond alikuwa akizungumzia sintofahamu iliyoibuka Oktoba 30, 2019 kati yake na Ali Kiba.

Siku hiyo aliulizwa swali katika mkutano wake na waandishi wa habari kama Ali Kiba na Harmonize watashiriki katika tamasha la Wasafi.

Alijibu kuwa ameuandikia uongozi wa Ali Kiba kuomba ushiriki wa mtunzi huyo wa wimbo maarufu wa “Aje”.

Pia, Diamond ambaye jina lake halisi ni Nassib Abdul, alisema hakuna haja ya kuendeleza “bifu (mzozo) ambao hakuutaja, baina yake na Ali Kiba.

Lakini kauli yake kwa waandishi wa habari haikumfurahisha Ali Kiba na katika akaunti ya mtandao wa kijamii ya officialalikiba, alitoa maneno makali bila ya kumtaja anayemshambulia.

“Usiniletee mambo ya darasa la pili, unaniibia penseli halafu unanisaidia kutafuta,” ameandika bosi huyo wa Kings Record Label.

“(UNIKOME). Mwanaume huwa anaongeaga mara moja tu, sasa ukitaka nikuweke uchi watu wajue unayonifanyia hata kwenye hilo tamasha hatokuja mtu. Sasa tuishie hapo, nakutakia tamasha jema.”

Juu ya ujumbe huo kuna picha ya Ali Kiba akiwa amekaa kwenye kiti, amevalia suruali aina ya jeans na shati la mikono mirefu bila ya kufunga vifungo.

Jana katika mahojiano hayo Diamond amesema, “nilibahatika kuona post kama watu wengine, na sikujua alilenga kitu gani, lakini Alikiba ni kaka yangu amenizidi umri alianza muziki kabla yangu.”

“Kwenye muziki kuna mambo ya ukitoa wimbo ni kama Simba na Yanga (timu za soka zenye upinzani nchini Tanzania) lakini haiwezi kutia chuki kati yangu na yeye,” amesema Diamond.

Diamond ambaye wimbo wake wa “Number One” (remix) ulitamba Afrika baada ya kumshirikisha Davido wa Nigeria amesema, “japo sijajua sababu, mimi ni mtu ninayeheshimu sanaa naamini ni miongoni mwa watu tunaochangia kuleta sifa katika tasnia ya muziki nchini.”

Kuhusu tuzo za Afrimma zilizofanyika Marekani ambazo alikuwa miongoni mwa wasanii waliotakiwa kupanda jukwaani, Diamond amesema alishindwa kutumbuiza, akibainisha kuwa suala hilo linaihusu menejimenti yake.

Diamond pia alizungumzia kuhusu Harmonize ambaye ametangaza kujiondoa kampuni ya WCB, “Nimempush Harmonize kufika hapo alipo, nafikiri sasa ni wakati sahihi wengine kuwasapoti, tamanio letu ni kuona tunafanikiwa, naomba watu wamsapoti lengo letu ni kusapoti vijana.”

Chanzo: Mwananchi
 

Msukuma wa dar

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2016
Messages
871
Points
1,000

Msukuma wa dar

JF-Expert Member
Joined Jul 14, 2016
871 1,000
Bwana mdogo kajua kucheza akili za wadanganyika..

Katoka kumtoza mil500 mmakonde wa watu km ada ya kuvunja mkataba, lakni leo anajidai kumtaka kijana ashiriki tamashani..
Diamond bana, mbele ya camera anajifanya mtu mwema, nyuma ya pazia anawafitini na kuwaroga, huyu jamaa ni snitch
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Messages
12,043
Points
2,000

Mkaruka

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2013
12,043 2,000
Ili wasanii wa bongo wafikie malengo hawanabudi kuungana.
Kama kweli anataka kuwasaidia wasanii wenzake na siyo kuwatumia kwanini hafanyi collabo nao mpaka aone faida kwanza.

Hata Kumshirikisha Msanii Kutoka Wasafi Chai Jaba Hataki Ila Yeye Akiwataka Wasanii Wengine Anafanya

Na Wasanii Wasiposhtuka Watatumika Sana
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Messages
12,043
Points
2,000

Mkaruka

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2013
12,043 2,000
Tokea amdhalilishe mwanamke aliyemzalia watoto, simpendi huyu mtoto. Mungu anisamehe tu.
Kamtangaza Mpaka Penny Katoa Mimba Yake Kwenye Media, Alipoona Haitoshi Akamtangaza Mpaka Kwenye Wimbo.

Yaani Itakumbukwa Vizazi Kuwa Penny Alitoa Mimba Ya Domo.

Sijui Kwanini Penny Hakumpeleka Mahakamani Kwa Kumfanyia Defamation Ya Hali Ya Juu.
 

Kibumbula

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2018
Messages
3,462
Points
2,000

Kibumbula

JF-Expert Member
Joined Mar 26, 2018
3,462 2,000
Kama kweli anataka kuwasaidia wasanii wenzake na siyo kuwatumia kwanini hafanyi collabo nao mpaka aone faida kwanza.

Hata Kumshirikisha Msanii Kutoka Wasafi Chai Jaba Hataki Ila Yeye Akiwataka Wasanii Wengine Anafanya

Na Wasanii Wasiposhtuka Watatumika Sana
Fafanua vizuri hapo kiongozi
 

Forum statistics

Threads 1,390,273
Members 528,139
Posts 34,047,949
Top