DIAMOND:MTV HUNISHIRIKISHA KABLA YA KUPITISHA VIDEO YOYOTE YA MSANII WA TANZANIA

KAFA.cOm

JF-Expert Member
Jun 22, 2013
1,301
739
Icon wa Bongo flava Naseeb ‘Diamond’ Abdul, amewashangaa wasanii wanaomtupia maneno kila kukicha kuwa anawabania wasanii wengine ‘connections’ za kung’ara kimataifa.

Akizungumza na TBC juzi, Platnumz amesema anasikitishwa sana na maneno hayo ilhali anafanya juhudi kubwa kujitafutia na kuwatafutia wasanii wengine masoko ya kimataifa.

“Mi nashangaa sana kusikia hayo maneno, wanasema hivyo wakati mi najitahidi kuwasaidia wenzangu tutoboe wote, kila kolabo ya msanii wa nyumbani na msanii wa Nigeria inayofanywa mi ndo huwa nasababisha.” alisema Diamond

“Nikiamua kubana mbona naweza tu, kwa sababu vituo vingi vya nje vinanisikiliza kwa mfano tu MTV wenyewe wakipokea video ya msanii yoyote kutoka hapa (Tanzania) wananipigia wananiuliza kwanza huyu vipi? tuicheze ngoma yake au? mi huwa nasema tu anafanya vizuri huku, basi inapita wanaicheza nikiamua kubana si naweza tu?”

Katika ‘line’ nyingine, baba Tiffah amesema timu yake ya Wasafi ndiyo iliishauri kituo cha tv cha Nigeria Sound City na MTV kuanzisha chati za Afrika Mashariki kwenye vituo hivyo.
 
"MTV wenyewe wakipokea video ya msanii yoyote kutoka hapa (Tanzania) wananipigia wananiuliza kwanza huyu vipi? tuicheze ngoma yake au? mi huwa nasema tu anafanya vizuri huku, basi inapita wanaicheza nikiamua kubana si naweza tu?" Aaaaaaaaawkey!!! Kwamba yeye ndio mwakilishi mkazi wa MTV??o_O
 
ahaaaa!!:eek::eek: nmeshajua, basi ndo mana Balozi video zake hazichezwi uko eeeh!!!...

Acha kutunga weka kitu humu kuonyesha kama hata anajua kuwa watu wanatuma maombi kuonba nyimbo zao zichezww oli wapate pesa

MTV ndio wanamtambua wanamuziki wengi nchini wapo ila hawajawahi kutoboa kama Diamond na habari ndio hiyo.

Hongera kwa Baba Tiffah kwa bidii anayoongoza katika kazi zake na kusaidia wanaotaka kusaidiwa na sio wale wanaofikiri watazeeka wakiimba kama walivyofanya siku ya kwqnza na kutaka kumshusha kitu ambacho wameshindwa.
 
Ndio faida ya kuwa MKUBWA..

Afu watu watachanganya kwenye hili
1. Maoni
2. Kuidhinisha

No vitu viwili tofauti. Hakuna anayefanyiwa figisu figisu, kila Nazi nzuri inapata airplay MTV kama ni ya quality ndogo huwezi kuiona inachezwa huko...
 
ahaaaa!!:eek::eek: nmeshajua, basi ndo mana Balozi video zake hazichezwi uko eeeh!!!...
Kwahiyo unataka kusema kiba anajua kuwa ili nyimbo za kibongo zichezwe ni lazima DIAMOND aulizwe na MTV, na anapoulizwa ndio anasema huyo underground huku wala hajulikani kisha wanaitupia kapuni. SASA KIBA SI ANGEKUWA ANASEMA TU NI JINSI GANI WATU WANAMFANYIA FIGISU FIGISU YEYE ALIKUWA ANAOGOPA KUSEMA ANAONA ATAMPA UJIKO DIAMOND KUWA NDIO MUIDHINISHAJI WA NYIMBO. Nimegundua mambo 2 hapa kuwa 1 -DIAMOND NI MSANII MKUBWA SANA KULIKO HATA SISI MASHABIKI ZAKE TUNAVYOONA 2 - Kiba analijua hili kuwa DIAMOND ni muhidhinishaji wa nyimbo za kibongo ktk vituo vikubwa vya TV.
 
Hahaahahaaaaa,huyu wa kuitwa Mondi namkubali sana,juhudi zake ndizo zimemfikisha hapa alipo,majungi kwake mwiko,yeye kazi tu,kama ronaldo vile,keep it up mzee,mola akuongezee zaidi na zaidi,vizabina zabina vyote kwa uwezo wa allah vishindwe na vilegee
 
Tatizo la Diamond ni uongo mwingi sana MTV wana criteria zao za kufanya video ipigwe au isipigwe video yako ikiwa na criteria wataipiga tuu na pia wana panel inayoreview hio video ambapo inaweza kukaa kwa wiki 3-4 video yako mpya isichezwe lakini kwa wasanii wanaojulikana nadhani hua ni rahisi kupigwa au video zinazotengenezwa na production houses kubwa...MTV Base hawawezi kua wajinga wa kufanya wawe wanamuuliza Diamond hii video vipi? wakati hayupo kwenye hio panel yani sababu tu ni ya msanii anayoka Tanzania maana kwa kufanya hivyo watakua wameenda kinyume na maelekezo yao ya video submission pia watakua wanaweka wazi conflict of interest kati ya Diamond na msanii mwingine yeyote yile toka Tanzania..kama si mtu wa kufatilia vitu kivile ndo unaweza kuamini statement kama hio..
 
Umenena mkuu, hapo Chibu Dangote alituibia kidogo pengine alikuwa anawajibu kiaina yake team coming soon kusema kuwa wanafanyiwa figisu maana mtu hawezi kukufanyia figisu kama hana power hiyo akaona apigilie msumari hahahahah
 
There was no need for that.. So what.?

Kukosa darasa kwa wasanii wetu ni tatizo.
 
Back
Top Bottom