Kwa kauli hii, yamkini JWTZ hakupo shwari

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,109
18,326
Nadhani jeshini kumepata mabadiliko sana , enzi za Mwamunyange huwezi sikia kauli kama hizi kwa askari wetu. Hizi ni kauli za wanasiasa na sio kwa wanajeshi kama JWTZ.

Huyu Mkuu wa Jeshi anasema yupo Tayari kuwafuta kazi wanajeshi. Jeshi letu ni jeshi lililofundishwa kuwa na nidhamu, yamkini kuna malalamiko ambayo hayajatelelezwa.

Mabeyo unafeli wapi mkuu.

20200605_145929.jpeg
 
Mkuu mbona kaongea kawaida sana au kulikuwa na kitu kichwani kwako ulipenda aongee hajaongea? Au ww upo uko ungependa utoe kilio chako bila kupata sehem sahihi na kuamua kutafuta huruma ya watu huku? Anyway nisamehe Kama nimekukwaza kwa mtazamo wangu.
 
Nukuu ya taarifa hii ya kinidhamu ilipaswa kubaki huko huko jeshini, na wala isifike huku uraiani. Ni kama vile tu kauli ya kinidhamu ya mkuu wa shule kwa wanafunzi wake, ama kauli ya kiongozi wa dini kwa watendaji wake wa chini n.k.
 
Kwanini sare za makamanda wa Tanzania ziko local na wako kwenye event wala sio field. Tazama mavazi na kofia kama vya fundi cherehani. Mbona sioni wakivaa golden star au hata silver, wana star za kushona. Mkuu wa majeshi nchi zingine wanavaa kitu kama suti hivi, sasa hawa kila nikiona picha zao wanavaa kawaida mno. Mbona kina IGP Mwema na Gen. Mwamunyange at least walivaa smart.

Kuhusu kuongea, huyu Gen. alishawahi kusema neno kuhusu kambi Fulani mpya akaleta mkanganyiko. Naamini si msemaji mzuri bali mtendaji.
 
Kuhusu hii picha mimi ningeuliza alama yetu kama taifa ni JWTZ au TPDF sababu hapo kuna Kiingereza na Kiswahili jee tunalitambua jeshi letu kwa kizungu au kiswahili. Ni vema tuwe na alama moja tu utakuta wanajeshi wengine wamevaa JWTZ
 
Kuna watu mnajua kuthamanisha!
Wengine tukiangaliaga hayo mapicha, hata kutofautisha hatuwezi.
Ni sawa na mtoto mdogo akipewa uji uliowekew chumvi ama sukari yeye anakunywa tu, dah!
 
Nukuu ya taarifa hii ya kinidhamu ilipaswa kubaki huko huko jeshini, na wala isifike huku uraiani. Ni kama vile tu kauli ya kinidhamu ya mkuu wa shule kwa wanafunzi wake, ama kauli ya kiongozi wa dini kwa watendaji wake wa chini n.k.
sawa kabisa
 
Kuhusu hii picha mimi ningeuliza alama yetu kama taifa ni JWTZ au TPDF sababu hapo kuna Kiingereza na Kiswahili jee tunalitambua jeshi letu kwa kizungu au kiswahili. Ni vema tuwe na alama moja tu utakuta wanajeshi wengine wamevaa JWTZ
Ni 3D inategemea upo engo ipi lakini maana ni ile ile
 
Sasa kipi kibaya alichosema General hapo?

Soma mpaka mwisho anasema askari wafanye kazi kwa kuzingatia viapo vyao, we unavijua viapo vya askari?
Askari anaapa na atafanya kazi kwa kulinda kiapo chake, kama hujui viapo vyao vinasema nini nenda kapige stori zingine haya mengine huyajui
 
Hatuoni maana ya hayo matamshi ya kisiasa na kutishana.. jeshini hatutishani..

Bwana E. V. Mapigano, CR bora kuwahi kutokea pale SUA, course ya agribusiness sina cha kuongeza kwenye uzi huu.
 
Hatuoni maana ya hayo matamshi ya kisiasa na kutishana.. jeshini hatutishani..
hata wanajeshi wanafukuzwa mkuu.

haya ndio mnalilia kila siku ili kulinda haki za watumikiwa(wanchi) yaani nidhamu na uwajibikaji.
hao wengine walifnya jeshi kuwa taasisi ya wavuta bangi.
 
Kunafitinika ukiona hivyo... Ila ni hatari sana kumfuta kazi askari mwanajeshi mwenye mafunzo kamili

Jr
 
Back
Top Bottom