Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Mi nadhani hata wabunge na madiwani hatuwahitaji tena.
Tumejaliwa rahis anayeweza kupanga na kupitisha bajeti yeye peke yake, sasa wengine hawa wa kazi gani tena kama siyo kuongeza tu gharama za mikopo ya magari na posho za kukaa.

Kwanza rahis wetu haitaji kikao na mtu ili wagawane posho kwa kufanya maamuzi, huyu ni jembe.
Nadhani tuanze kufikiria hata kufuta mhimili wa mahakama coz tunaye rahis mtenda haki kwa wanadamu wote.

Hata PM haikuwa na haja awe mbunge kwanza, tungeacha tu rahis wetu ateuwe popote sababu ana nia njema sana na wanainji.

Mambo ya uchaguzi ni gharama alafu yanatugawa tu bora tufute ili rahis wetu huyu ATAWALE tu mpaka siku Mungu atakapomuondoa duniani. Mbona babu zetu waliongozwa na kina chifu Mangungo na maisha yalienda vizuri tu.
 
Demokrasia ina-maanisha uchaguzi huru na wa haki lazima viwepo(na mengineyo). Demokrasia hupiganiwa-hivyo ni haki ya watanzania, na mapungufu yatapiganiwa ili yarekebishwe hata kama itachukua miaka mingi-kwa mfano kutokupeleka malalamiko zidi ya mshindi wa uraisi etc. Haijalishi kama alieko madarakani ni mzuri kiasi gani lazima tuwe na checks and balances na uchaguzi ni njia kubwa ya kuwa na checks na balances. Kigezo kimoja kwa uongozi wa JPM ni jinsi atakavyohandle issue ya katiba. Uzalendo na ujasiri wake hapo ndio utaonyesha anataka kulipeleka wapi taifa hili.
 
pro cdm=pro magufuli as long as magufuli ameiacha njia chafu ya ccm kwa sasa ana mass support from cdm ila makada wapiga dili wa ccm watamchukia sana huyu rais
Kweli tupu mfano huyu jamaa anajiita Assadsyria ni mwana CCM ila anampiga vita sana Magufuli nadhani anaisoma namba.
 
Last edited by a moderator:
Swali la kujiuliza ni kuna haja gani ya kuwa hata na chaguzi ilhali tunajua kabisa mwisho wa siku CCM ndo atatangazwa mshindi?
Kumbe wabunge wote wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro nj wa CCM! Kumbe wabunge wote kule Pemba ni CCM! Kumbe wabunge wote Dar es Salaam ni CCM! Kumbe wabunhe wote Lindi, Mtwara, Kigoma ni wa CCM! Sikujua hilo
 
JPM is the special project, Ili kutengeneza msingi imara katika nchi hii JPM apewe muda wa kuongoza usio na kikomo yaani afikishe umri kama wamugabe, taifa limejaa wazembe kwenye ngazi mbalimbali,,, reshuffle ya kudumu inahitajika kuijenga tanzania mpya..
 
Swali hili bado lipo, baada ya kazi nzuri ya Magufuli anayoendelea kufanya ya kutumbua hararais na vijipu uchungu, kuna haja ya kufanya uchaguzi wa rais 2020?!.

Paskali
 
kama 'hapakazi tu' itazalisha kazi na ajira ,
kama tutaona maendeleo ya kweli katika huduma na nyanja nyengine
kama haki na uhuru wa kujieleza utaheshimiwa

haya tutaweza kuongelea baada ya miaka 5 ..au hio 2020 yenyewe kwa sasa kazi kubwa anayo fanya ni kujaribu kuondoa majipu yalopita...awamu zilizo pita ambayo ni za ccm pia.Haya yatampotezea muda kweli kweli kwani ni mengi mnooo
haya madudu ni mengi sana na itafika 2020 bado hayajaisha hivyo ni bora kwa
sasa ashughulike na mambo ya uchumi na kuhimiza uwekezaji na kubuni sera nzuri zaidi za uwekezaji...ili kuvutua wawekezaji wawe wandani au wa nje ili tuongeze ajira na kodi...tunahitaji kukua kwa uzalishaji mara alfu ili ku peleka mbele uchumi wetu....Bila ya kukua uzalishaji kodi itapungua sana hivyo eneo hili ni muhimu sana sana ili tusiyumbe
mambo ya majipu awachie kina makonda na wenzake..yeye asimamie moja kwa moja masuala ya uchumi na maendeleo
hapo baada ya muda kama tumefanikiwa tutampa 5 Pasco
 
Demokrasia ina-maanisha uchaguzi huru na wa haki lazima viwepo(na mengineyo). Demokrasia hupiganiwa-hivyo ni haki ya watanzania, na mapungufu yatapiganiwa ili yarekebishwe hata kama itachukua miaka mingi-kwa mfano kutokupeleka malalamiko zidi ya mshindi wa uraisi etc. Haijalishi kama alieko madarakani ni mzuri kiasi gani lazima tuwe na checks and balances na uchaguzi ni njia kubwa ya kuwa na checks na balances. Kigezo kimoja kwa uongozi wa JPM ni jinsi atakavyohandle issue ya katiba. Uzalendo na ujasiri wake hapo ndio utaonyesha anataka kulipeleka wapi taifa hili.
Ndugu Katiba mpya ndani ya miezi mitano!! Kumbuka mwaka jana uchaguzi+Katiba vilikula hela nyingi sana hebu tumuache aweke mambo sawa kidogo maana hajabadili sheria bali anaweka mambo sawa.
 
Wanabodi.

Kwa Kasi Hii ya Rais Wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli na Falsafa yake ya "Hapa Kazi Tuu", na kama hiki tunachokiona sio nguvu ya soda tuu, yaani ataendelea kwa kasi hii hii hadi 2020,
  1. Hivi Kweli Tanzania, Tuna Haja tena ya Kufanya Uchaguzi Wa Rais kwa mwaka 2020?.
  2. Hatuwezi kufanya uchaguzi wa wabunge tuu na madiwani, na badala yake , ili kuokoa pesa na muda, Magufuli apewe a walkover ya kuendelea hadi 2025?!.
  3. Au kwa vile Uchaguzi wa Rais ni takwa la kikatiba, hivyo uchaguzi huo lazima tuu ufanyike hata kama ni wastage of time and money?!,
  4. Na hiyo 2025 tukimuona bado anaweza, na anatufaa, kuna ubaya kuibadili katiba yetu tumpatie extension ya kutosha kuinyoosha Tanzania?!.
  5. Kwani katiba ni nini?,si ni kipande tuu cha karatasi?!, nini muhimu kati ya kipande cha karatasi na Magufuli?!.
  6. Na Katiba ni ya nani?!, ni yetu?!, na iko kwa manufaa ya nani?!, si ipo kwa manufaa yetu?!, hivyo sisi ndio muhimu kuliko katiba, tukimtaka Magufuli, si tunaweza kuiweka tuu katiba pembeni?!.
  7. Sasa kama Magufuli anatufaa sana, na katiba haitamruhusu kuendelea baada ya 2025, kuna ubaya gani kuibadili katiba kwa manufaa yetu?!,
  8. Au kwani Katiba ni Msahafu kusema haiwezi kubadilishwa?!.
  9. Na jee ubaya wowote wapinzani wa Tanzania mkiamua kwa kauli moja msisimamishe tena mgombea urais, na badala yake CCM ndio iwe inatoa rais siku zote kufuatia long eksipirience ya uzoefu wa muda mefu kwenye urais?.
  10. Na kufuatia somo la urais wa Zanzibar, na kilichofanyika kwenye urais wa JMT, kweli wapinzani makini bado watahitaji kweli kusimamisha mgombea kushindana na Magufuli?!, kutakuwa ni kugombea au kujifuahisha tuu?!, au hata ikitokea ameshinda atatangazwa?!.

Hayo ni maswali tuu nimeanza kujiuliza aloud?!.
Jee wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?!.

Pasco
Hivi kumbe na wewe huwa unaandika upuuzi kama huu
 
Wanabodi.

Kwa Kasi Hii ya Rais Wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli na Falsafa yake ya "Hapa Kazi Tuu", na kama hiki tunachokiona sio nguvu ya soda tuu, yaani ataendelea kwa kasi hii hii hadi 2020,



    • Hivi Kweli Tanzania, Tuna Haja tena ya Kufanya Uchaguzi Wa Rais kwa mwaka 2020?.
    • Hatuwezi kufanya uchaguzi wa wabunge tuu na madiwani, na badala yake , ili kuokoa pesa na muda, Magufuli apewe a walkover ya kuendelea hadi 2025?!.
    • Au kwa vile Uchaguzi wa Rais ni takwa la kikatiba, hivyo uchaguzi huo lazima tuu ufanyike hata kama ni wastage of time and money?!,
    • Na hiyo 2025 tukimuona bado anaweza, na anatufaa, kuna ubaya kuibadili katiba yetu tumpatie extension ya kutosha kuinyoosha Tanzania?!.
    • Kwani katiba ni nini?,si ni kipande tuu cha karatasi?!, nini muhimu kati ya kipande cha karatasi na Magufuli?!.
    • Na Katiba ni ya nani?!, ni yetu?!, na iko kwa manufaa ya nani?!, si ipo kwa manufaa yetu?!, hivyo sisi ndio muhimu kuliko katiba, tukimtaka Magufuli, si tunaweza kuiweka tuu katiba pembeni?!.
    • Sasa kama Magufuli anatufaa sana, na katiba haitamruhusu kuendelea baada ya 2025, kuna ubaya gani kuibadili katiba kwa manufaa yetu?!,
    • Au kwani Katiba ni Msahafu kusema haiwezi kubadilishwa?!.
    • Na jee ubaya wowote wapinzani wa Tanzania mkiamua kwa kauli moja msisimamishe tena mgombea urais, na badala yake CCM ndio iwe inatoa rais siku zote kufuatia long eksipirience ya uzoefu wa muda mefu kwenye urais?.
    • Na kufuatia somo la urais wa Zanzibar, na kilichofanyika kwenye urais wa JMT, kweli wapinzani makini bado watahitaji kweli kusimamisha mgombea kushindana na Magufuli?!, kutakuwa ni kugombea au kujifuahisha tuu?!, au hata ikitokea ameshinda atatangazwa?!.

Hayo ni maswali tuu nimeanza kujiuliza aloud?!.
Jee wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?!.

Pasco
Adi na wewe unahandika Pumba,kweli Njaa mbaya kaka
 
Back
Top Bottom