Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Pasco ni mapema mno kuwaza haya.

Tumpongeze kwa kiasi fulani lakini pia tusisahau kuweka akiba ya maneno.

Ni wabongo tu hawana kumbukumbu na rahisi kudanganyika. Mrema alitisha kuliko Magufuli mara kumi. Watu mpaka walibandika vibao vilivyoandikwa ''usitupe taka taka hapa kwa amri ya Mrema''. Kila mahali ilikuwa ni Mrema Mrema! Katu uongozi wa namna hii hauwezi kuleta mabadiliko! Kinachotakiwa na Magufuli kuweka mfumo mzuri wa uongozi!
 
#Pasco Leo umeboronga,sidhani mtu mwelewa kama wewe unaweza kujiuliza maswali kama hayo!
Je,ni nani atakayepima kuwa kufanya uchaguzi ni wastage of time?Ni kwa utaratibu upi unadhani utatumika kujua wananchi wanamtaka aendelee?Au wachache watawasemea wengi?Ni akina nani hao?Labda tuseme wabunge,je atajuaje kuwa wananchi wanataka hivyo?
Yakifanyika hayo,huoni kama tunalea jipu ambapo Rais yeyote hata kama hafai miaka ya mbeleni anaweza jiamulia tu kuwa wananchi wengi wanamtaka hivyo no uchaguzi!
Tunamuunga mkono Magufuli ila mahaba yako kwake yasikutie upofu!Uzi huu naona ni kama umeanzisha kwa lengo la kumsifia na si hilo linaloonekana moja kwa moja kwenye uzi!
Mambo haya zungumza humu humu JF,usijeongea kwenye media kama radio na tv,watu watakuona mwehu!
 
Hakuna haja ya kufanya uchaguzi sababu chama kilichoshika dola akitak achilia na wanatangaza rais wanaomtaka wao sio alochaguliwa na watanzania,so no need ya ku waste time ktk kufanya uchaguzi but inabd system yao iwe waz tu.
 
Pasco,

Umeandika katika lugha ngumu kwa kiasi flani hoja zako zinajirudia kimantiki.

Nikirejea hapo umesema "Nguvu ya Soda" Ambyo kimsingi ni mfano hai kwa Watangulizi wake,Hvyo bdo hoja yako inakosa uhalisia inabaki kutegemea uhalisia wake kwa Jinsi alivyoanza na aina ya Mrejesho wake kwa Wananchi.

Umezungumzia hoja ya Upinzani kushiriki uchaguzi wa Urais,Ukirejea Mifano ya Znz na ukiomweka Jamaa hapo alipo kwa kujikita katika Upinzani kutangazwa endapo watashinda nadhani hoja ya Muhimu ipo kwenye kutangazwa Mshindi na si Vinginevyo.
 
Last edited by a moderator:
Huwa nikiona comment za kuibiwa kura huwa nacheka sana...maana nakumbuka Lowasa aliwambia wapige kura kazi ya kulinda amwachie...!
Haikutosha makamanda walimsajili mtu aliye wadanganya kuwa yeye ni mtaalam wa kuiba kura lakini wapi...!

Umemaliza kufikiri vp hujaenda kwa bibi yako msoga?
 
Mbona wewe ni Member siku nyingi tu humu ndani? Umeshindwa kabisa kumsoma Pasco katikati ya mistari?

Kumezuka kikasumba cha kutuaminisha kuwa Magufuli ni Musa wa Tanzania atakayetuvusha Baharini na Jangwani.

Ila wengine wanataka kumfanya tayari ni Mfalme. Utadhani walioweka miaka 10 mwisho hawakuwa na akili.

Kama akiwashughulikia Mafisadi, kuleta nidhamu nchini na mwisho wakati anaondoka atuache katiba ya Warioba, basi itatosha kwani atakuwa kashajenga msingi na kuwaachia wengine waendeleze.

Pasco kataka watu tuanze kufikiri huko wengine wanatupeleka kwani kuzaliwa kwa Dikteta huanza kama lelemama.

Ghadaffi, Kagame, Mugabe nk walikuwa viongozi wazuri sana mwanzoni ila mwishoni wote tunaona wanavyouwa watu ili tu kubaki madarakani. Uganda na Museven ndiyo kabisa. Kajaza Mizee inayoitwa UGANDA DREAM TEAM.



Pasco,
Kwanza nikiri wazi kwamba huwa naheshimu sana maoni ya watu. Pili huwa nafuatilia na kuvutiwa na hoja zako nyingi hapa jukwaani! Ila niseme ukweli leo umeongea kijinga sana kwenye hii hoja! Nasema kijinga kwa sababu bado unaweza kujielimisha,kuelimishwa na ujinga wako ukaondoka!
Tanzania hatufanyi uchaguzi eti kwa sababu Nchi haina uongozi mzuri ama kwa sababu hakuna kiongozi shupavu. Mpaka sasa anachokifanya magufuli sio kitu kigeni,kiliwahi kufanywa huko nyuma na waliomtangulia lkn bado tulilazimika kuingia ktk uchaguzi! Tulikuwa tunafanya uchaguzi tukiwa na mfumo wa chama kimoja, leo tunao mfumo wa vyama vingi unakuja na mawazo ya kijinga namna hii?
 
Last edited by a moderator:
Wenzio tayari wamepigiwa Push-up na Mkafiri wa Kisukuma. Unaona Mziki wa wala Nguruwe?

Nina imani hivyo vibiashara vyako ulilipa kodi kwani vinginevyo, wewe na mumeo, MtaiSOMA NAMBA.

UDA tayari kimenuka. Bakhresa wako tayari maji shingoni. Nadhani atakwenda na Wahindi/Waarabu kadhaa wa Kariakoo.

Yaani huwezi kuamini eti nchi ilikuwa na Rais na watu kama wewe mlishinda hapa mnamtetea.

Halafu Mkapa na UFISADI wake anaita watu wanaolalamika eti Wapumbavu na Malofa. AnBen wataisoma namba.

Ushamtema mamvi?

Sikushangai, nnaona umesalim amri kama wapumbavu na malofa wenzako wengi tu.
 
KAMA atafanya vizuri mimi sina shida kuiunga mkono CCM! Mimi sina chama ila ninataka uongozi mzuri! Naona mnatumia nguvu nyingi sana kumsifu Magufuli japo bado hajafanya chochote kipya. Mtaweza kucheza na bongo za wabongolala ambao hawana kumbukumbu. Alikuwepo Mrema na alitingisha kuliko Magufuli mara kumi... lakini uongozi wa kutegemea mtu badala ya mfumo haudumu na haubadilishi chochote!

Nakubaliana na wewe asilimia zote mtu mmoja hawezi kutenda yote. Nchi yetu imekosa taasisi zinazoweza kujitegemea zenyewe na kufanya kazi kwa uweledi mkubwa na ndio maana hatupigi hatua. Tukijenga taasisi imara zisizoingilika na kutumika na wanasiasa wakubwa na kuheshimu professionalism tutapiga hatua. Bila hivo tutakua tunapaka upepo rangi.
Magufuli anataka Ku progress ahakikishe taasisi zote zinafanya mambo kwa usmart.
 
Swali la kujiuliza ni kuna haja gani ya kuwa hata na chaguzi ilhali tunajua kabisa mwisho wa siku CCM ndo atatangazwa mshindi?

No need bila kuwa na tume huru nothing will change na watu wamejikatia tamaa ya kupiga kura. Nchi hii hamna uchaguzi huru na haki sasa upinzani unapambana na dola yenye kila kitu hapo itachomozaje kutangazwa tu matokeo ya upinzani Mpaka mabomu yapigwe. Tuna safari ndefu ka taifa
 
Huu ni ukima na ukinyanyiko...raisi hajakutana hata na gumu lolote tumpime iq yake na maamuzi, hajamaliza hata mwaka tupime utendaji wake watamani atawale milele! Weka akiba ya maneno safari ni ndeeeeefu sana...japokuwa mwanzo sio mbaya wala sio mzuri kivile..
 
Back
Top Bottom