Kwa ilivyo hali ya kisiasa Tanzania , je ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali inaweza kuaminika?

Kuna dawa za maumivu zinalevya ndio,na kama mtu atazi'abuse nae itahesabika ni mtumiaji wa dawa za kulevya.
NB: Mkemia mkuu atajua tu ni kilevi cha aina gani kimetumika kwahiyo hakuna wasiwasi hapo.
Kila mtu aende na mkemia wake,,,alaaaaaa
 
Wakuu natanguliza salamu.

JF ndio sehemu pekee wanapokutana wale wanaofikiria "NJE YA BOX" Sasa naomba kufahamu imani yenu kwa Taasisi hii ambayo inatumika kubaini wanaotumia Madawa ya kulevya .

Je haiwezi kupokea " MAAGIZO KUTOKA JUU " ?
Mkuu, kama vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya na kutekeleza maagizo kutoka juu, hivyo utarajie pia Mkemia mkuu lazima atapokea na kutekeleza maagizo hayo kutoka juu.
 
wakawa sasa wamegeuka na kuwa watetezi wa wahalifu.. sasa wameenda mbali hata kuzarau professional za watu walioko sector nyeti kama mkemia mkuu.. prof wangu manyele hajawahi kuwa mtu wa namna hiyo. na kama waliopimwa hawajaridhika wanaweza kukata rufaa na kwenda kupima lab nyingine, kwa usimamizi wa serikali na mtuhumiwa.
Acha utani weweeeeeeee,wakimchoma sindano ya sum........
 
Porojo za UKAWA science is a Science ikionesha kuwa Damu au Mkojo wa Mbowe una Heroine sidhani kama Mkemia mkuu wa Kenya atakua na kipimo kitakachopima tofauti.
Acha unafiki wako. Ni mambo mangapi yamekwenda ndivyo sivyo hapa njini kwetu. Hivi mnadhani hatuoni au hatujui?
 
Kwanini walioshutumiwa hawajakata rufaa kuwa sample zao zipelekwe sehemu nyingine wewe ndo unaonekana siyo Great thinker kwa kujaribu hata kuingilia elimu usiyokua Nayo na vipimo vya kisayansi.
Wapeleke wapi?
 
Chadema mitandaoni mmetisha lakini kwenye box la mpiga kura huwa wananchi wanawapa ile inaitwa suprise...
Hongereni wana mtandao
 
mbona hawaonyeshwi matokeo ya vipimo hapohapo kama ilivyo kwa HIV,full politics mkuu
ubabaishaji mwingine ndo huu sasa.. kabla ya kulaumu onesha kwanza medhod inayotumika kupima HIV na uwepo wa madawa ya kulevya katika mkojo. onesha pia muda unaotumika katika kila test alaf ndo uje kulaumu hapa kwa nini wanachelewesha majibu ya vipimo vya madawa ya kulevya, wakati ya HIV vinatoka papo hapo.

usipende kulaumu vitu usivyovijua..
 
Wakuu natanguliza salamu.

JF ndio sehemu pekee wanapokutana wale wanaofikiria "NJE YA BOX" Sasa naomba kufahamu imani yenu kwa Taasisi hii ambayo inatumika kubaini wanaotumia Madawa ya kulevya .

Je haiwezi kupokea " MAAGIZO KUTOKA JUU " ?
Msiwe na wasiwasi waungwana na tuziamini mahakama zetu tu na zinatenda haki. Otherwise, ushahidi wa Daktari kuhusu vipimo uwa ni kama OPINION tu na Judge au Hakimu hafungwi na vipimo vya Daktari. Kinachomtia mtu hatiani ni DIRECT EVIDENCE ila wa Kitabibu is Just a mere opinion.
 
Wakuu natanguliza salamu.

JF ndio sehemu pekee wanapokutana wale wanaofikiria "NJE YA BOX" Sasa naomba kufahamu imani yenu kwa Taasisi hii ambayo inatumika kubaini wanaotumia Madawa ya kulevya .

Je haiwezi kupokea " MAAGIZO KUTOKA JUU " ?

Siku zote unatakiwa kutilia mashaka Serikali & Wanasiasa. Siku ukiacha (au ukibweteka) na kuwaamini umekwisha.
 
Wakuu natanguliza salamu.

JF ndio sehemu pekee wanapokutana wale wanaofikiria "NJE YA BOX" Sasa naomba kufahamu imani yenu kwa Taasisi hii ambayo inatumika kubaini wanaotumia Madawa ya kulevya .

Je haiwezi kupokea " MAAGIZO KUTOKA JUU " ?
Jibu la swali lako mkuu lipo katika matamko ya kamanda Sirro, it seems hakuna chombo kinacho zingatia taaluma na ueledi tena katika awamu hii.Hiyo ofisi ya mkemia mkuu itatumika kupiga rubber stamp kwa maamuzi yaliyofanyika katika jengo jeupe.
 
Porojo za UKAWA science is a Science ikionesha kuwa Damu au Mkojo wa Mbowe una Heroine sidhani kama Mkemia mkuu wa Kenya atakua na kipimo kitakachopima tofauti.
Inawezekana ikapimwa sampuli ya TID iliyobandikwa jina la Mbowe, na majibu yakatangazwa kuwa ni ya Mbowe. Hivyo ndivyo inavyoweza kufanyika IKIWA kuna maagizo kutoka juu. Kwani kuna mtu anasimamia mchakato wa kuhakikisha kuwa kweli sampuli iliyochukuliwa toka kwa mtuhumiwa ndiyo iliyopimwa, au kama imepimwa kwa usahihi na majibu sahihi ndiyo yaliyotangazwa kuhusu mtuhumiwa huyo? Hapa namaanisha mtu ambaye ana maslahi na mtuhumiwa, mtu ambaye katika hali ya kawaida hawezi ku-conspire au hata kutishwa na wale waishio "juu"!!

Nina hakika unaelewa kuwa ukweli ni mpana zaidi kuliko hicho ulichoongea.
 
Hata nusu kaputi pia.Ila Makonda na Sirro wanacheza mchezo mchafu sana,watakuja kut=jutia sana baadaye
Hili kweli na haswa madereva huyo ndio atakuja kujuta. Maana ataangukiwa na kesi za kutosha hadi atajuta
 
Back
Top Bottom