Kwa hili! WaTz tuna 'roho mbaya' kweli!

Usedcountrynewpipo

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,636
2,725
Nimejaribu ku reciprocate fadhila tunazopewa na wenzetu weupe kwa kweli nikaishia kuona aibu na huzuni.
Wazungu wanaongoza kwa kutupa mabilioni ya pesa za msaada. Kuanzia bajeti ya maendeleo n.k pesa nyingi ni ya mfadhili. Hata huko kwenye miradi ya ukimwi, haki ya nani isingekuwa Wazungu nusu yetu tungekuwa ni wangonjwa au marehemu ila misaada yao ndio imesaidia kupunguza maambukizi. Huko Africa ya magharibi isingekuwa msaada wa Markeani kuingilia kati, Ebola ingekuwa imewafagia wooote.
Wachina nao walitujengea reli ya TAZARA bureee kabisa kama msaada.
Sasa nikajaribu kusema embu tuseme asante kwa kuwapa ka Twiga kamoja hawa wazungu kama shukrani nikaona Weeee!
Yani ukipandisha Twiga mmoja ndege ukawape wazungu Wabongo watapiga kelele kuanzia January mpaka January nyingine. Watatokwa povu na kuongea kila aina ya maneno kwa mnyama ambaye value yake hata haizidi ten million.
Basi nikaona kumbe hii ndio sababu wabongo hatusogei kimaendeleo kwa sababu hatuna roho za kusaidiana na kusaidia wenzetu, yani chetu chetu na kakitu kadogo kanaweza kumtoa roho mbongo....
Ili wabongo kusogea hapa tulipo, hatuhitaji tu kuwa open minded, tunapaswa pia kuwa open hearted...
 
Mwongo mkubwa wewe! mzungu gani kapewa twiga? Na ni zawadi gani inayotolewa kwa kufichwa fichwa? Wazungu wanaishi Arabuni?
Si hao twiga wangekabidhiwa hadharani TBC ikionyesha live? Na kwa nini wahusika walipwe kisirisiri? Ngumburu wewe!!
 
Wendi wetu wakiwemo viongozi hatuwaelewi Wachina vizuri; wachina walifundishwa na babu zao waliowatangulia miaka mingi iliyopita kuwa "TOA KWANZA ILI UPATE KUCHUKUA."
Tunaamini kuwa wachina walijenga reli ya TAZARA bure, hiyo si kweli kwani hawa wachina walisomba madini mengi sana wakati wa uchimbaji wa ile reli na thamani ya hayo madini ilikuwa zaidi ya thamani ya kujenga hiyo reli!!

Hivi sasa viongozi wengi wa Afrika wameingia kwenye mtego huo huo wa kupata misaada kutoka China na kufikiri ni ya bure; hivyo sivyo kwani China inawapa misaada mingi Afrika ili kuweza kukomba maliasili zinazopatikana toka katika kontinenti hili. Kumbuka waingereza wanamsemo kuwa "THERE IS NO FREE LUNCH."
 
Mwongo mkubwa wewe! mzungu gani kapewa twiga? Na ni zawadi gani inayotolewa kwa kufichwa fichwa? Wazungu wanaishi Arabuni?
Si hao twiga wangekabidhiwa hadharani TBC ikionyesha live? Na kwa nini wahusika walipwe kisirisiri? Ngumburu wewe!!
Nani atalipia ikionyeshwa TBC?
 
Nimejaribu ku reciprocate fadhila tunazopewa na wenzetu weupe kwa kweli nikaishia kuona aibu na huzuni.
Wazungu wanaongoza kwa kutupa mabilioni ya pesa za msaada. Kuanzia bajeti ya maendeleo n.k pesa nyingi ni ya mfadhili. Hata huko kwenye miradi ya ukimwi, haki ya nani isingekuwa Wazungu nusu yetu tungekuwa ni wangonjwa au marehemu ila misaada yao ndio imesaidia kupunguza maambukizi. Huko Africa ya magharibi isingekuwa msaada wa Markeani kuingilia kati, Ebola ingekuwa imewafagia wooote.
Wachina nao walitujengea reli ya TAZARA bureee kabisa kama msaada.
Sasa nikajaribu kusema embu tuseme asante kwa kuwapa ka Twiga kamoja hawa wazungu kama shukrani nikaona Weeee!
Yani ukipandisha Twiga mmoja ndege ukawape wazungu Wabongo watapiga kelele kuanzia January mpaka January nyingine. Watatokwa povu na kuongea kila aina ya maneno kwa mnyama ambaye value yake hata haizidi ten million.
Basi nikaona kumbe hii ndio sababu wabongo hatusogei kimaendeleo kwa sababu hatuna roho za kusaidiana na kusaidia wenzetu, yani chetu chetu na kakitu kadogo kanaweza kumtoa roho mbongo....
Ili wabongo kusogea hapa tulipo, hatuhitaji tu kuwa open minded, tunapaswa pia kuwa open hearted...
Duh! Nimecheka na kusikitika hapohapo! Twiga waliuzwa hawakutolewa msaada bro!!
 
Back
Top Bottom