Nadhani hujamuelewa. Mleta mada hapa ana maanisha kuwa Tatizo kubwa la waandishi wetu wa habari hawataki kuumiza akili zao kuuliza maswali ambayo yatamfanya mtu anaejibu kuumiza akili katika kufikiria kuyajibu kiusahihi. Kwa kifupi maswali yao mengi ni mepesi sana na 'too direct' hata mjibuji hapati shida ya kuyajibu inakuwa kama kawaandalia maswali kawapa wayajibu. Vile vile suala la waandishi wanapokuwa na nafasi ya kuwauliza wanasiasa wanaenda kama ni wa upande unaowakilisha 'opponent' badala ya kuwa 'neutral' waweze kujenga hoja zaidi na maswali yenye kuumiza kichwa katika kufikiri kuyajibu.
Kwa mfano, katika mkutano wa Mh. Nape jana nilitegemea waandishi wa habari waulize maswali kama hasa tukianzia suala la gharama
1. Bajeti ya TBC kwa mwaka ni kiasi gani?
2. Kama shirika la umma linapewa ruzuku na serikali? Kama ndiyo ni kiasi gani?
3. Kuna upungufu wa kiasi gani wa hela za kuweka kutangaza matangazo live ya Bunge?
4. Bunge ni moja ya Mihimili inayojitegemea, je kwa suala hili limeandaliwa fungu gani kusaidia shirika hili la umma kuonyesha wazi mijadala ya Bunge? Na kama hakuna, kwa nini isiletwe hoja hii kuwezesha kupata fungu litakalokuwa rasmi kusaidia kuwezesha zoezi la utangazwaji live wa vipindi vya bunge?
Haya ni baadhi tu, ilitakiwa Mh. Nape ajikute anarudi kujiandaa tena kuja na facts zenye ushahidi lakini sio anajibu kisiasa
Weledi wataongeza zaidi
wewe jamaa naamini IQ yako ni kubwa sanaaaaaaa