Kwa Hili TECNO Mnastahili PONGEZI

Kwa Hili TECNO Mnastahili PONGEZI

Ndugu wanajamvi,
Nimeona ninene la kwangu kuhusiana na kampuni ya Simu TECNO.
Nimekuwa mtumiaji wa simu za Tecno kwa muda mrefu na hasa kwa hizi Smartphones tangu N3, P3 ........!
Lakini katika matoleo yote nilowahi kutumia leo naomba niwapongeze hadharani kwamba TECNO L6 wameitendea haki kwa suala zima la charge.
Tecno L6 ina uwezo wa kukaa na charge kwa muda mrefu ukilinganisha na matoleo mengine.
Hongera sana TECNO, hongera TECNO L6.

pole Sana kwa kuwa mkereketwa wa tecno mkuu, maana umekuwa mtumwa wa tecno Tena zile za 50000 kama P3.ukipata pesa nunua brand nyingine Kama htc, experia, Samsung nk. utajutia kuipa tecno sifa
 
Ni kweli mkubwa mimi nilikuwa mtumiaji mzuri sana wa simu na vifaa vya apple tatizo kubwa la hizo iPhone ni charge tuu, ilinilazimu kununua hii simu ya Techno L6 kutokana na kukaa na chaji muda mrefu, kwa kweli Tecno kwa hilo nawapa pongezi ingawa nilikuwa naziponda sana hizo simu tokea zilipoanza kuenea
 
Mimi nikiwaambia simu ninayotumia sijui mtanipondaje?
 
Ni kweli mkubwa mimi nilikuwa mtumiaji mzuri sana wa simu na vifaa vya apple tatizo kubwa la hizo iPhone ni charge tuu, ilinilazimu kununua hii simu ya Techno L6 kutokana na kukaa na chaji muda mrefu, kwa kweli Tecno kwa hilo nawapa pongezi ingawa nilikuwa naziponda sana hizo simu tokea zilipoanza kuenea

haijaniingia akilini kuwa unaweza kutoka apple hadi tecno.kauli yako nailinganisha na shetani alivyotupwa toka mbinguni hadi kuzimu.aliona mbinguni hapamfai
 
haijaniingia akilini kuwa unaweza kutoka apple hadi tecno.kauli yako nailinganisha na shetani alivyotupwa toka mbinguni hadi kuzimu.aliona mbinguni hapamfai

Ndio hivyo mkubwa nilikuwa kila mara nachaji hasa nikiingia kwenye net
 
mimi techno sitaki hata kuwasikia. Mwanzoni nilijua labda tatizo ni laini yangu au simu kumbe kuna watu wengi nao wanakabiliwa na TATIZO HILO LA SIMU ZA TECHNO. UKIPIGA AU KUPIGIWA HUA INAKATA YENYEWE HARAFU INAANDIKA RADIO OFF. Nimeenda voda wakaniambia badilisha simu, nimenunua sumsang tatizo limeisha.
 
Mimi nimetumia tecno aina tatu tofauti nimeanzia p3, m5, na sasa h6 na sijakutana na tatizo lolote tatizo wabongo hatuwezi kutengeneza hata tochi ila kwa kuponda hatujambo.
 
haijaniingia akilini kuwa unaweza kutoka apple hadi tecno.kauli yako nailinganisha na shetani alivyotupwa toka mbinguni hadi kuzimu.aliona mbinguni hapamfai

Ni suala la vipaumbele mkuu unaweza ukahama kutoka apple kwenda tecno hakuna shida kwani simu kama simu kwa mtu ambae yupo busy na ujenzi wa taifa anaitumia kidogo sana hivyo kuwa na simu ya laki 9 alafu unaitumia kwa whatsup na facebook labda na kuku-alert kama email imeingia si bora uwe na TECNO ya laki na nusu tu ambayo ina kila kitu na ikiharibika kama haitengenezeki unavuta nyingine tena mpya kiuraini.
 
Mimi nimetumia tecno aina tatu tofauti nimeanzia p3, m5, na sasa h6 na sijakutana na tatizo lolote tatizo wabongo hatuwezi kutengeneza hata tochi ila kwa kuponda hatujambo.
Uzuri wa hizi unahakika kuwa ni brand new na si fake wakati hizo zingine mkuu unaweza ukapigwa kwa kuuziwa fake wa bei original, by the way tuishi kulingana na uwezo yaani ukibarikiwa kuwa na fungu la kutosha nunua Samsung au Apple n.k lakini kama vipi hata TECNO si mbaya sana kwani simu unataka ukae nayo miaka 5 imekuwa scania hiyo au fuso
 
Wengi unakuta hatujui matumizi ya vitu vinavyohusiana na computer unakuta for the first time ndio amegusa smart phone kama ndio kifaa kinachohusina na computer hivyo kunapokuwa na system failure kwa kuwa ni mashikolomageni anajifanya kuing'ang'aniza kuzima na mwisho wa siku anahiharibu (sasa hapa ndio simu zimetofautiana maana kuna ambazo zinavumilia unashangaa inadunda na kuna zingine zitakuzingua though hata zile sizizozingia wakati mwingine zinaweza kuroga kama ukiilazimisha). Kikubwa na matumizi sahihi ya vifaa vya ectronics itapelekea simu yako kudumu hata kama simu yako itaitwa sijui Wugh Wangh
 
Ni kweli mkubwa mimi nilikuwa mtumiaji mzuri sana wa simu na vifaa vya apple tatizo kubwa la hizo iPhone ni charge tuu, ilinilazimu kununua hii simu ya Techno L6 kutokana na kukaa na chaji muda mrefu, kwa kweli Tecno kwa hilo nawapa pongezi ingawa nilikuwa naziponda sana hizo simu tokea zilipoanza kuenea

Kukaa au kutokaa na chaji ni aina ya matumizi...
Wengi tunataka kufanya kazi za pc kwenye simu...
Zaidi ya kupiga na kupokea simu, smartphone zimekuwa designed kufanya kazi nyepesi ambazo unaweza kuzifanya ukiwa hauna pc au tablet...
 
pole Sana kwa kuwa mkereketwa wa tecno mkuu, maana umekuwa mtumwa wa tecno Tena zile za 50000 kama P3.ukipata pesa nunua brand nyingine Kama htc, experia, Samsung nk. utajutia kuipa tecno sifa

Yap. Jana nilikuwa nasoma makala moja kuhusu IQ za weusi dhidi ya weupe. Kiufupi ni masikitiko makubwa sana. Jamaa anasema wanabuni product nyingi kwa ajili ya weusi ambao hawajui uchumi wala hawafikirii kukuza uchumi wao zaidi ya kununua flashy things. Perfect fit
 
Nikiangalia screenshots zako natathimini kuwa simu yako haikai na chaji hata kwa 24 hours!!!
 
Nikiangalia screenshots zako natathimini kuwa simu yako haikai na chaji hata kwa 24 hours!!!

Then kitu kinachokula charge kuliko vyote Ni standby.

Wakati standby inamaanisha kioo kimezima na simu imetulia. Simu ambayo mda mwingi IPO standby na haifikishi hata masaa 24 inasifiwa inakaa chaji?

attachment.php

Mfano windows phone standby inaweza kaa masaa hata 8 ikadrop asilimia moja au mbili tu.
 
pole Sana kwa kuwa mkereketwa wa tecno mkuu, maana umekuwa mtumwa wa tecno Tena zile za 50000 kama P3.ukipata pesa nunua brand nyingine Kama htc, experia, Samsung nk. utajutia kuipa tecno sifa
Kila imburi hula kwa urefu wa kamba yake mura Ilisorokobwe. Akipata fweza atakuwa na vipaombele vingine, siyo simu. Techno yatosha.
 
Back
Top Bottom