Kwa hili Serikali inachemsha.

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,737
405
Asubuhi ya leo katika taarifa ya habari ya Clouds FM nimesikia kuwa serikali imeshatoa uraia kwa wakimbizi wa Kisomali zaidi ya 4000 na kuna wengine takribani 1500 hasa wale walio maeneo ya Handeni Tanga nao wapo katika mchakato wa kupewa uraia kwa kuwa serikali imeridhika kuwa hawa ni KIZAZI CHA NNE CHA WAZIGUA waliohamishwa enzi za ukoloni na kupelekwa mashariki ya mbali na somalia. MY TAKE Sipingi hawa jamaa kupewa uraia lakini serikali imetumia vigezo gani kujiridhisha kwa hilo?...na nyie ndg zangu WAZIGUA kumbe wengi wenu ni wasomali.,sikujua hilo.
 
Mbongo, kwa hili, serikali did the right thing!. Hao wasomali walikuja nchini 1973, wazazi waliokuja wengi wamefia hapo, wanaopewa uraia ni watoto ambao wamezaliwa Tanzaniam hawaongei tena Kisomali bali Kizigua na Kiswahili.

Wanachofanyiwa ni kupewa tuu birth right ya kuzaliwa nchini hao watoto, hivyo lazima uwape uraia na watoto wao.

Hatua hii ni moja ya masuluhisho matatu makuu ya tatozo la wakimbizi duniani kote, inaitwa Intergration, mengine ni Repatriation, kuwajesha kwao na Resettlment into a 3rd Country, yaani kuwapeleka nchi nyingine. Kwa hao wakimbizi wa Kisomali, intergration is the best option.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom