Mimi namwamini Mungu tu mambo ya sijui Gamanywa, Kakobe, Mwingira mara sijui Mzee wa Upako nawaachia wenye akili zao mi na ujinga wangu ntabaki na Mungu wangu tu.. Biblia inanitosha sina mwongozo mwingine.
Kama maisha yamekushinda jifunze uchungaji,halafu jitahidi uende Mbeya,Congo au Nigeria ukapikwe fresh,ukirudi lazima utoke kimaisha ndani ya mwezi tu.Kama wewe ni msanii na unataka mafanikio ya faster,jipodoe vizuri,rekebisha hips,kisha imba injili.
Mkuu, wewe umewaza kama mimi.... nimechoka kwa kweli... naamini MUNGU ni mwaminifu na anaweza kunifanyia mimi kama Neno lake linavyosema...Mimi namwamini Mungu tu mambo ya sijui Gamanywa, Kakobe, Mwingira mara sijui Mzee wa Upako nawaachia wenye akili zao mi na ujinga wangu ntabaki na Mungu wangu tu.. Biblia inanitosha sina mwongozo mwingine.
nakupa 100% me too kaka nitabak na bibilia yangu tu,Mimi namwamini Mungu tu mambo ya sijui Gamanywa, Kakobe, Mwingira mara sijui Mzee wa Upako nawaachia wenye akili zao mi na ujinga wangu ntabaki na Mungu wangu tu.. Biblia inanitosha sina mwongozo mwingine.
Mimi namwamini Mungu tu mambo ya sijui Gamanywa, Kakobe, Mwingira mara sijui Mzee wa Upako nawaachia wenye akili zao mi na ujinga wangu ntabaki na Mungu wangu tu.. Biblia inanitosha sina mwongozo mwingine.
Mkuu Mossad Jaribu basi na kur-an nao ni muongozo mwingine wa Mungu.
Jumamosi mchana nillisikiliza radio Wapo fm inayomilikiwa na Mchungaji Gamanywa wa wa Wapo internatinal
Siku hiyo mchana wote manabii, mitume na wachungaji wanaomiliki makanisa na vituo binafsi vya maombi na maombezi walikuwa wamepanga Foleni redioni wakinadi misa zao za Siku iliyofuata yaani Jumapili.yaani ilikuwa bandika bandua mpaka Usiku
Maneno yao yalifanana woote, Yani ilikuwa ni kama copy n paste, kuwa ibada itakuwa na miujiza ambayo hujawahi kuiona popote, watakaohudhuria wataombewa watoe nuksi,wapate mali,vyeo utajiri nk nk, lakini mwishoni walitaja namba zao za mpesa na tigopesa kwa ajili ya kuchangia huduma
Nikajiuliza mbona Wapo fm inatumika namna hii, lakini nikajua ni biashara hivyo wanapokea matangazo wanalipwa basi life goes on
Jumapili asubuhi kwenye kipindi cha Patapata Mchungaji gamanywa naye akarushwa hewani akaaza kuwaonya wasikilizaji kuwa wawe makini na watu watoao matangazo ya kuvutia watu waende kwenye makanisa yao, akasema wengi ni waongo na hawaaminiki. Kumbuka naye Siku hiyo alikuwa na ibada kwenye kanisa lake hivyo akawa anavutia kwake huku akikandia wenzake
Hii si nzuri; jana yake kachukua pesa ya wenzake, kawarusha hewani wakajinadi, Siku inayofuata kawakejeli huku akijifagilia mwenyewe
Mungu huyu anaona mengi...!
Injili imegeuka kuwa biashara, na makanisa yameteka umma mkubwa wa wakiristo kwa kuamini yanayohubiriwa humo ni KWELI katika kumwinua Kristo. Ukweli ulio kweli ni kwamba wanaasimama kuhubiri wanapewa nguvu hiyo na mwovu shetani ambapo hii ni kufuru kubwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Kwa muono wangu ambao naamini ni ushuhuda alionijalia Mungu Mwenyezi, zaidi ya asilimia 90 ya wanaoijiita Wachungaji, manabii, mitume, wapakwa mafuta wamepikwa kwa nguvu za giza huko Nigeria, Kongo, Mbeya nk ili kuja kuanzisha makanisa wanayoyaita ya kiroho na ambayo yanawavutia wengi kujiunga. mahubiri yai ni kutafuta mali za hii dunia.