Kwa hili rais JK umeonyesha udhaifu mkubwa wa kiongozi

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,285
9,922
SIAMINI, tena sitaki kusikia eti Rais Jakaya Kikwete amesikiliza kilio cha wabunge, vyama vya siasa, wananchi wa kawaida na wanaharakati kutaka mawaziri waliohusishwa na kashfa
kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wajiuzulu baada ya
kukubali kulisuka upya baraza lake.

Huu ni uamuzi wake au uamuzi wa CCM? Rais ambaye anaongozwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano, aliyoapa kuilinda kweli anaweza
kufikia uamuzi huo baada ya kushauriwa na viongozi wa CCM? Nani zaidi sasa, CCM au
Katiba ya Jamhuri ya Muungano?
Taarifa ya Rais Kikwete kutaka kubadili upya Baraza la Mawaziri inatangazwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye. Huyu ni nani katika serikali yetu? Katibu Mkuu
Kiongozi hayupo au amekwenda likizo? Kazi za Katibu Mkuu Kiongozi ni zipi? Waziri
Mkuu kazi yake ni nini? Taarifa za mambo ya serikalini siku hizi zinatolewa na Nape?
Tunaelekea wapi? Taaarifa ya kubadili Baraza la Mawaziri inatolewa na Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM.

Bado najiuliza Rais Kikwete alifikiri nini mpaka akaamua kupeleka suala la mabadiliko ya
baraza la mawaziri kwenye kikao cha Kamati Kuu ya CCM? Hili naona halihitaji mwekezaji
kuelewa kuwa mamb yametendwa ndivyo sivyo.
“Hivyo CC tumaridhia na kutaka uamuzi huo uchukuliwe mara moja, tuna imani kuwa rais
atafanya mabadiliko haraka iwezekanavyo maana alikuwa amebanwa na majukumu kidogo
ya safari nje ya nchi, mazishi ya Rais Bingu wa Mutharika na sherehe za Muungano.

Ila sasa wakati wowote atafanya,” hii ni nukuu ya Nape.
Ndugu zangu tangu lini Nape amekuwa msemaji wa Ikulu? Tangu lini Nape amekuwa
msemaji wa safari za rais na ratiba zake za utendaji wa kila siku? Salva Rweyemamu analipwa kwa ajili ya kazi ipi? Au hawajui mipaka ya kazi zao?
Hii kauli ilipaswa kusemwa sirini na watu wenye akili, si kuita mkutano wa waandishi wa
habari kwenda kuzungumzia kitu ambacho kwanza si wajibu wake, na wasemaji wa mambo hayo wapo? Kikwete aliruhusu vipi shughuli za Ikulu kuzungumziwa na Nape wakati Salva Rweyemamu na Balozi Sifuni Sefue wapo? Kwa mantiki hii, Kamati Kuu ya CCM ina nguvu
ya kimaamuzi ya nchi kuliko Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bunge linapoamua mambo fulani hayatekelezwi isipokuwa mpakayapitie kwanza kwa viongozi wa CC ndipo yafanyiwe utekelezaji katika nchi. Aibu gani hii? Tunaipeleka wapi nchi yetu? Tunahangaika sasa
kwa kesi za uchaguzi kuwasumbua Watanzania
na majaji kulipwa kwa pesa kubwa huu ulikuwa ni uamuzi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba, kuwashauri wagombea wote
wa chama hicho walioshindwa wakate rufaa na CCM ingelipia gharama za kuendesha kesi.
Tunahangaika kila kukicha kwa sababu ya maamuzi mabaya ya CCM, bado na Kikwete
tuliyempa madaraka, anasumbuliwa kutokuwa thabiti kwa masuala muhimu yanayogusa masilahi ya taifa.
Kiongozi wetu wa nchi anahitaji kwenda katika CC ya CCM ili kuomba ushauri wa kubadili
baraza la mawaziri au la? Hii pengine inatokana na kuwaogopa mawaziri wachafu, ama kwa uswahiba, au kwa matakwa mengine ambayo
anashindwa kubeba lawama, badala yake anatafuta sehemu ya kujiegemeza ili lawama zisimkute yeye.

Nakumbuka Rais Kikwete alishawahi kusema kuwa urais wake hauna ubia, lakini kwa hali ya mambo inavyokwenda jambo hilo linaonekana kuwa tofauti, je, amesahau kauli hii?
Mawaziri waliobainika kuwa ni wabadhirifu wa mali za umma wametajwa na ripoti ya Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Akataja bila woga kuwa Waziri wa Nishati na
Madini, William Ngeleja; Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu; Waziri wa Fedha; Mustafa Mkulo
na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi, George Mkuchika. Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda na Waziri wa Viwanda na Biashara; Dk Cyril Chami. Je, orodha ya wazi namna hii ilihitaji kweli kuitisha Kamati Kuu ya CCM kuomba ushauri kufikia maamuzi?
Kwanza Waziri Mkuu angekuwa makini kwa hili, angekuwa haogopi uswahiba wa mawaziri hawa na Kikwete, angetoa tamko akiwa anaahirisha Bunge mjini Dodoma, Nape anatamba bila aibu kuwa Kamati Kuu iliyokutana juzi ilipokea taarifa mbili ikiwemo uamuzi huo wa rais kulisuka upya baraza la mawaziri kutokana na ripoti ya CAG. “Kamati Kuu imepokea taarifa kubwa mbili, taarifa ya Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa CCM na Kamati ya Wabunge wa CCM kwa upande mmoja na taarifa ya Kamati ya Uongozi
ya Wawakilishi wa CCM kwa Bara na Zanzibar,” alisema.

Haya ya kwenye kamati za CCM yameingiliaje maamuzi ya Katiba ya nchi na mamlaka ya Rais Kikatiba? Na Kikwete kwanini aliamua kuuchezea urais wake kwa kuwapa CCM
waufanyie majaribio?
Najisikia aibu nchi yetu inavyoongozwa, lakini
kwa kuwa tunaongozwa na familia ya kambale;
baba ana ndevu, mama ana ndevu, bibi ana ndevu, vijana wake kwa waume wana ndevu,
basi kila mmoja ni msemaji katika taifa letu kwa jambo lolote.

Aibu kubwa sana kwa uongozi wa nci kuchukuliwa kiurahisi kiasi hicho.
 
SIAMINI, tena sitaki kusikia eti Rais Jakaya Kikwete amesikiliza kilio cha wabunge, vyama vya siasa, wananchi wa kawaida na wanaharakati kutaka mawaziri waliohusishwa na kashfa
kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wajiuzulu baada ya
kukubali kulisuka upya baraza lake.

Huu ni uamuzi wake au uamuzi wa CCM? Rais ambaye anaongozwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano, aliyoapa kuilinda kweli anaweza
kufikia uamuzi huo baada ya kushauriwa na viongozi wa CCM? Nani zaidi sasa, CCM au
Katiba ya Jamhuri ya Muungano?
Taarifa ya Rais Kikwete kutaka kubadili upya Baraza la Mawaziri inatangazwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye. Huyu ni nani katika serikali yetu? Katibu Mkuu
Kiongozi hayupo au amekwenda likizo? Kazi za Katibu Mkuu Kiongozi ni zipi? Waziri
Mkuu kazi yake ni nini? Taarifa za mambo ya serikalini siku hizi zinatolewa na Nape?
Tunaelekea wapi? Taaarifa ya kubadili Baraza la Mawaziri inatolewa na Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM.

Bado najiuliza Rais Kikwete alifikiri nini mpaka akaamua kupeleka suala la mabadiliko ya
baraza la mawaziri kwenye kikao cha Kamati Kuu ya CCM? Hili naona halihitaji mwekezaji
kuelewa kuwa mamb yametendwa ndivyo sivyo.
"Hivyo CC tumaridhia na kutaka uamuzi huo uchukuliwe mara moja, tuna imani kuwa rais
atafanya mabadiliko haraka iwezekanavyo maana alikuwa amebanwa na majukumu kidogo
ya safari nje ya nchi, mazishi ya Rais Bingu wa Mutharika na sherehe za Muungano.

Ila sasa wakati wowote atafanya," hii ni nukuu ya Nape.
Ndugu zangu tangu lini Nape amekuwa msemaji wa Ikulu? Tangu lini Nape amekuwa
msemaji wa safari za rais na ratiba zake za utendaji wa kila siku? Salva Rweyemamu analipwa kwa ajili ya kazi ipi? Au hawajui mipaka ya kazi zao?
Hii kauli ilipaswa kusemwa sirini na watu wenye akili, si kuita mkutano wa waandishi wa
habari kwenda kuzungumzia kitu ambacho kwanza si wajibu wake, na wasemaji wa mambo hayo wapo? Kikwete aliruhusu vipi shughuli za Ikulu kuzungumziwa na Nape wakati Salva Rweyemamu na Balozi Sifuni Sefue wapo? Kwa mantiki hii, Kamati Kuu ya CCM ina nguvu
ya kimaamuzi ya nchi kuliko Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bunge linapoamua mambo fulani hayatekelezwi isipokuwa mpakayapitie kwanza kwa viongozi wa CC ndipo yafanyiwe utekelezaji katika nchi. Aibu gani hii? Tunaipeleka wapi nchi yetu? Tunahangaika sasa
kwa kesi za uchaguzi kuwasumbua Watanzania
na majaji kulipwa kwa pesa kubwa huu ulikuwa ni uamuzi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba, kuwashauri wagombea wote
wa chama hicho walioshindwa wakate rufaa na CCM ingelipia gharama za kuendesha kesi.
Tunahangaika kila kukicha kwa sababu ya maamuzi mabaya ya CCM, bado na Kikwete
tuliyempa madaraka, anasumbuliwa kutokuwa thabiti kwa masuala muhimu yanayogusa masilahi ya taifa.
Kiongozi wetu wa nchi anahitaji kwenda katika CC ya CCM ili kuomba ushauri wa kubadili
baraza la mawaziri au la? Hii pengine inatokana na kuwaogopa mawaziri wachafu, ama kwa uswahiba, au kwa matakwa mengine ambayo
anashindwa kubeba lawama, badala yake anatafuta sehemu ya kujiegemeza ili lawama zisimkute yeye.

Nakumbuka Rais Kikwete alishawahi kusema kuwa urais wake hauna ubia, lakini kwa hali ya mambo inavyokwenda jambo hilo linaonekana kuwa tofauti, je, amesahau kauli hii?
Mawaziri waliobainika kuwa ni wabadhirifu wa mali za umma wametajwa na ripoti ya Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Akataja bila woga kuwa Waziri wa Nishati na
Madini, William Ngeleja; Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu; Waziri wa Fedha; Mustafa Mkulo
na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi, George Mkuchika. Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda na Waziri wa Viwanda na Biashara; Dk Cyril Chami. Je, orodha ya wazi namna hii ilihitaji kweli kuitisha Kamati Kuu ya CCM kuomba ushauri kufikia maamuzi?
Kwanza Waziri Mkuu angekuwa makini kwa hili, angekuwa haogopi uswahiba wa mawaziri hawa na Kikwete, angetoa tamko akiwa anaahirisha Bunge mjini Dodoma, Nape anatamba bila aibu kuwa Kamati Kuu iliyokutana juzi ilipokea taarifa mbili ikiwemo uamuzi huo wa rais kulisuka upya baraza la mawaziri kutokana na ripoti ya CAG. "Kamati Kuu imepokea taarifa kubwa mbili, taarifa ya Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa CCM na Kamati ya Wabunge wa CCM kwa upande mmoja na taarifa ya Kamati ya Uongozi
ya Wawakilishi wa CCM kwa Bara na Zanzibar," alisema.

Haya ya kwenye kamati za CCM yameingiliaje maamuzi ya Katiba ya nchi na mamlaka ya Rais Kikatiba? Na Kikwete kwanini aliamua kuuchezea urais wake kwa kuwapa CCM
waufanyie majaribio?
Najisikia aibu nchi yetu inavyoongozwa, lakini
kwa kuwa tunaongozwa na familia ya kambale;
baba ana ndevu, mama ana ndevu, bibi ana ndevu, vijana wake kwa waume wana ndevu,
basi kila mmoja ni msemaji katika taifa letu kwa jambo lolote.

Aibu kubwa sana kwa uongozi wa nci kuchukuliwa kiurahisi kiasi hicho.
Mkapa aliwahi kunukuliwa akiuliza hivi " kwani Kikwete ni robbot"?
 
Hongera sana Mkuu KURUNZI kwa kumpasulia JK. Maelezo yako yana mantiki kubwa sana. Hiyo hali ya Mambo ya serikali kusemewa na akina Nape, ni uthibitisho mwingine mkubwa kuwa JK ni dhaifu sana kwa vigezo vyovyote vya uongozi. Tangu aingie madarakani nchi yetu ilianza kukabiliwa na Ombwe kubwa la uongozi wa ngazi ya juu. Hata Lowassa aliwahi kusema bungeni kuwa serikali ya JK haiwezi kufanya maamuzi magumu. Yeye JK akabaki anachekacheka tu kama kawaida yake. Hakuna kitu pale Ikulu. Kwa hiyo hata akibadili baraza la mawaziri mara 1000, hakuna kitakachobadilika maana hata hao wapya wanaujua udhaifu wake, nao watafanya wanavyotaka. Tatizo kubwa kama wadau wengi walivyosema ni JK mwenyewe. Nchi hii kubadilika labda yeye mwenyewe awajibike kwa kujihudhuru urais. Dk Bilal yupo atamalizia kipande kilichobaki. Hii inaweza kumrejeshea heshima JK. Zaidi ya hapo ni kuchemka tu na kujidharaulisha mwenyewe.
 
Unashindwa kuelewa kuwa hiyo sheria iliyowapa CAG meno na wabunge mdomo kaileta Kikwete kwa makusudi kabisa na ilikuwa haipo kabla ya yeye kuingia madarakani.

Inaonesha una fikra dhaifu, finyu na fupi.
 
Hivi kwenu hakuna choo ili uwe unapeleka huko hicho kiny... chako!?
 
Unashindwa kuelewa kuwa hiyo sheria iliyowapa CAG meno na wabunge mdomo kaileta Kikwete kwa makusudi kabisa na ilikuwa haipo kabla ya yeye kuingia madarakani.

Inaonesha una fikra dhaifu, finyu na fupi.
Hivi, Rais ndiye anayetunga sheria kweli!
 
Unashindwa kuelewa kuwa hiyo sheria iliyowapa CAG meno na wabunge mdomo kaileta Kikwete kwa makusudi kabisa na ilikuwa haipo kabla ya yeye kuingia madarakani.

Inaonesha una fikra dhaifu, finyu na fupi.

Hajui maana na madhara ya sheria aliyopitisha. Tumeshudia mara nyingi akitia sahihi miswada yenye mapungufu mengi kuwa sheria, na ikirudishwa tena bungeni kwa masahihisho.
 
Unashindwa kuelewa kuwa hiyo sheria iliyowapa CAG meno na wabunge mdomo kaileta Kikwete kwa makusudi kabisa na ilikuwa haipo kabla ya yeye kuingia madarakani.

Inaonesha una fikra dhaifu, finyu na fupi.

Kweli wewe ni mpuuzi. Huwa situmii hili neno lakini kwa uharo ulioandika sifa ya upumbavu nakupatia. Sheria ya kuwepo CAG sio matakwa ya JK. Ameikalia ripoti akawa Waziri wa mambo ya nje ni fedheha kubwa. Kuomba msaada wa Dola milioni nne kutoka Korea sawa na pesa zilizoliwa Kishapu and you think we have a president? Nilikwishasema na Narudia . Jakaya Mrisho Kikwete na CCM plus his Government is not serious come rain come sun. It's just daylight between The persona JK and presidency . Nilishatoa Shingo yangu sadaka if JK can make a single manly decision! Endeleeni kumsifu huyu Juha wenu
 
Amakweli ni Janga la Taifa aliwahi kutaadharisha Dr. Slaa kwenye kampeni zake mwaka 2010?
 
Nimesoma michango ya wadau wengi, kwa kweli Kikwete ni janga, hivi huyu uwezo wake kweli alifikiria nini kuwa rais, kuna mtu niliwahi kumwambia nafasi aliyopaswa kuitumikia nchi ni mjumbe wa nyumba kumi. Labda niwaulize ndugu zangu hivi kuwa na rais kama kikwete na nchi kutokuwa na rais lipi ni bora?
 
ni wachache sana hawajui kuwa kikwete ndo tatizo la nchi hii. anagawa vyeo kama sadaka unategemea nini? Mpaka anadiliki kusema kwenye siasa kazi haziishi bila kujua hao atakaowaweka wataathiri vipi utendaji wa serikali.Na kibaya zaidi yeye anajijua kuwa yeye kama yeye ni kilaza kwa sababu kitu kidogo kinachohitaji kufikiri bila kutumia akili nyingi yeye anasema hata m sijui kwanini nchi yetu maskini, kwani mi Mungu nilete mvua? Nchi za afrika zitaendelea endapo wafadhili watakuwa wanatoa misaada waliyoahidi kwa wakati nk hii ni mifani tu kuonyesha Rais wetu kilaza Hata College mate wake Lipumba alisema. The man he didn't bother himself to think at all. kwa hiyo ****** akistep down akamwachia makamu wake(ingawa naye hajui kuongea kabisa) tuone then 2015 CDM tuwatoe kabisa kiutawala ndo dawa
 
Jamaa ni kilaza wa kutupwa. Lakini labda kwa upande mwingine mi nahisi anawaogopa huenda anakula nao hivyo anajua akitamka mwenyewe kuwatosa watatoboa siri km enzi za Richmond alivyomwogopa Edward Hoseah kwa kuwa alikuwa anajua A to Z madudu yao.
 
Kwa jinsi nilivyomuelewa NAPE ni kwamba aliiwasilisha ile taarifa yake kwa vyombo vya habari na watanzania wote kwa ujumla kama msemaji wa Chama kuhusiana na yalojili CC ikiwa ni agenda kuu ya kikao kile na sio kama msemaji wa IKULU.
 
Atafute ushauri kutoka kwenye katiba kwani katiba inaongea?

Ikiwa ameza kuvunja katiba kwa kukasimu majukuu ya urais kwa CC unategemea anaweza akaifuata hata hiyo katiba itakayoaandikwa huenda akaipitisha bila hatakujua anapitisha nini.
 
Back
Top Bottom