Kwa hili nimeamua kutelekeza mchumba

jembe afrika

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
7,604
3,753
Wakuu nilikuja hapa kuwaeleza nimepata mchumba wa kiganda.

Jamani yaliyonikuta sitaki tena, si kanipeleka kwao kunitambulisha baada ya utambulisho si nikaomba nijue angalau japo kiasi cha mahali,kudadadaddeki oneni jamani,

1. Mahali Ush 8000000 sawa na 6000000 za kibongo.

2. Nguo za mama 600000ug sh.

3. Nguo za baba 500,000 ug sh.

4. Ng'ombe wa bibi 1
5. Ng'ombe wa babu 1
6. Walaji[pombe ya kienyeji] pipa moja

7. Harusi itafanyikia Tanzania niandae tiketi za ndege 30 na sehemu ya kufikia wao, jamani nilitaka kuzimia ilibidi niagize coke angalau nipunguze presha kwani hata soda inanyweka sasa wamenitolea mimacho kinoma mpaka nkashindwa kunywa.

Halafu lichumba lenyewe hata kunitetea hakuna nilikuwa mdogo kama piliton.

Ili niweze kuvilipia vyote inabidi nirudi home labda nikauze kiwanja,nyumba, ngo'mbe mbuzi kuku bata vijiko na baiskeli ya dingi na nikakope hela nyingine ya kujazilizia kudadadadadadeki maisha menyewe ya bongo duu.

Sasa huyu demu atasoma namba tu kesho napanda zangu spider nasepa kimyakimya.

Presha za nini utafikiri nanunua fuso na huyu mchumba anikome kabisa tena akifatafata nabadilisha na laini.

Eti huyu mchumba ananiambia I love you,nyooo kwenda huko wanataka kuniua na presha bora niende zangu Tanzania nikatafute mrembo mweusi kama yeye kwa bei cheee.

Na picha zake nimedelete kwenye simu yangu kudadadadeki,wanataka kumuua jembe afrika niwaacha wana jf hivihivi.

Eti na lenyewe limenisave picha yangu kwenye screensaver yake wataidai hiyo picha mahali kudadadadeki.

Jamani nimepata hasara huyu dada ana mizinga yaani anafikiri mimi ni mtoto wa Mengi.

Mara lunch,saloon,viatu,nguo utaniua eti.Nimeacha viatu kwake sivifuati maana nitakutana na mizinga tu.

Naombeni wabongo wenzangu nipokeeni narudi homu.Nahisi nimepungua kilo 8 hivi.

Nimekoma,bora hata wabongo wanahuruma.

Ni hayo tu wakuu yaliyonikuta mimi jembe afrika.
 
Ndo uanaume huo, kumkuza mtoto wa kike mpaka ukamkuta mzuri na ukampenda mchezo!! Kupambana na minyang'au iliyojaa siku hizi ni kama kupigana vita na makundi ya kigaidi, wana haki we oa mzigo huo utaanza maisha upya bana
mkuu wataniuaeti.....loading error....
 
teh teh teh teh tatizo wameshagundua udhaifu wako...sasa huku bongo utazipata wapi nature black?
 
1.Jembe,wewe sio mmuoaji,mahali ni negotiable wewe wapi unataka binti ndiye akanegotiate? Sasa be responsible not otherwise,unalalamika hata ujaomba kupunguziwa wala hata huku Tz si haba ukikuta familia nzuri zitakutoka tu....

2.Eti nalenyewe limenisave picha yangu kwenye screensaver yake wataidai hiyo picha mahali kudadadadeki.
jamani nimepata hasara huyu dada anamizinga yaani anafikiri mimi ni mtoto wa mengi.


Wewe umeenda Uganda na kuonyesha sifa ,kwanini naye asikuchune......
 
Pole sana. Inaonekana ulimwambia huyo binti unatoka familia bora labda wakati wa kumtongoza..
 
Hahhhha eti walidhani we mtoto wa Mengi
Ndio ukome kuacha vya kwenu na kutamani vya nje oooohhhhhh
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom