Kwa hili!!! : Nicolas mgaya,gratian mkoba na tucta nakosa imani na nyinyi.................

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
...........Tangu bunge la bajeti lilipoanza nilikuwa nasubiri kwa hamu bajeti ya wizara ya utumishi wa umma,na jana bila kusita wala kuona aibu waziri wetu ambaye natilia shaka uwezo wake wa kuwa kiongozi kutokana na namana anavyowasilisha mada pamoja na kuongea kama waziri Ndugu Hawa Ghasia aliwasilisha bajeti hiyo.Kilichoniuma na kinachoniuma ni kutosikia ongezeko la mishahara kwa sisi wapiga nyundo.Wakati wenzetu wanakula posho mpaka za nguo,sisi wapiga nyundo tunaendelea kuumia kwa viela vichache.Na kilichoniumiza zaidi ni pale alipoulizwa kuhusu ongezeko la mishahara,akadai hilo ni siri kati yao na wawakilishi wa wafanyakazi.............Jamani mimi ni mtumishi wa umma lakini sijawai pata taarifa kuwa tunaongezewa shs ngapi,sasa Je,Mgaya,Mkoba na TUCTA mnawawakilisha akina nani wakati mimi mtumishi wa umma sina taarifa hiyo? Na Je,hapa hakuna ajenda ya siri kati yenu TUCTA na serikali ya JK? Na naanza kupata maana ya yale maneno aliyosema JK wakati wa mei mosi namnukuu "Ndugu wakipatana wewe kashike jembe ukalime" na "waliokuwa wanawaombea mabaya wajue kuwa tumepatana" Jamani watumishi wenzangu ndugu wamepatana tushike majembe tukalime tuendelee kupigwa na jua kwa mwaka mwingine...Huku tukianza na mafuta ya taa bei juu lol!!!!
 
Hapa ndipo tuliposalitiwa mkuu lakini anyway tutajua cha kufanya

jk-wafanyakazi-1.jpg
 
.......... "Ndugu wakipatana wewe kashike jembe ukalime" na "waliokuwa wanawaombea mabaya wajue kuwa tumepatana" !

Hakuna kitu kilinikera siku hiyo kama kauli hiyo ya kinafiki na tangu wakati huo nilijua "hamna kitu hapo!"
 
poleni sana wajameni, hata sisi tunaingia sokoni kusaka ajira nadhani tunakuja kupambana wote!

Mgaya na Mkoba wameshapata mgao wao hawana haja ya kuwasemea wengine!
 
Hapo ninapokosa imani na watanzania. Maana huwa sielewi kama huwa wanafumba macho wakati wa kupiga kura au huwa kinatokea nini. Kwenye kampeni utawakuta na tshirt na bendera za CCM. uchaguzi ukiisha tu wanaanza malalamiko. Kwa taarifa yenu, JK keshapewa kura yake anajua hamuwezi kumfanya chochote, anasubiri mitano yake iishe aondoke zake. Hatakaa afirikirie matatizo yenu ****** yule.
 
Tanzania ni nchi ya wendawazimu; utategemea nini kutoka kwao. Ndiyo maana nchi hii infaidiwa zaidi na watu wakutoka nje.
 
Wehu naangalia marudio ya bunge star tv ndo nazidi kuchanganyikiwa. CCM kuna vichaa, halafu kwa nini kuna vyama vingi vya wafanyakazi. Kwa nini kisiwe kimoja?
 
Hapo ninapokosa imani na watanzania. Maana huwa sielewi kama huwa wanafumba macho wakati wa kupiga kura au huwa kinatokea nini. Kwenye kampeni utawakuta na tshirt na bendera za CCM. uchaguzi ukiisha tu wanaanza malalamiko. Kwa taarifa yenu, JK keshapewa kura yake anajua hamuwezi kumfanya chochote, anasubiri mitano yake iishe aondoke zake. Hatakaa afirikirie matatizo yenu ****** yule.

Kwa hiyo mkuu unatuambia kuwa tuna miaka mitano ya mateso sisi wapiga nyundo wa umma................?
 
Back
Top Bottom