Kwa Hili Nawapongeza Wababa/Wanaume

Mary Chuwa

Senior Member
Feb 24, 2011
177
40
Imekuwa ni kawaida kusikia ugomvi baina ya wamama na wake za watoto wao wa kiume(wakwe zao)
Hii ni kutokana na wamama wengi kutotambua nafasi yao pindi watoto wao wanapopata wake.
Kwani kabla ya kuoa nafasi hiyo hushikiliwa na mama,na pindi mwanaume anapooa huwa ni ya mke.

Lakini wamama wengi hawaridhiki na kuiacha nafasi hiyo,bali huwa ni kama mashindano kuonesha ubora,
Mfano:mama huona kama mtoto wake wa kiume haudumiwi vizuri,nguo hazifuliwi zikatakata,hapikiwi chakula kama alichokuwa anakiandaa yeye na mengineyo.
Anaona haudumiwi yeye bali ni mkwewe hivyo kujenga wivu na chuki.

Kwa wababa nafasi ya mume hushikiliwa na baba na baada ya binti kuolewa ni nafasi ya mume,
Nawapongeza wababa kwa kutambua kuwa sasa nafasi hiyo si yao tena na kupunguza mgogoro baina yao na wakwe zao,kwa hili nawapongeza sana na ni vyema mkasaidiana ili wakina mama watambue nafasi hiyo si yao tena na kupunguza mgogoro wa kugombana baina yao na wakwe zao.
 
Kwa wana harakati unapoongelea kurelax kwa baba baada ya binti yake kuondoka kwenda kwa mume. Wanaita huu ni mwendelezo wa mfume dume, kwani mzazi wa kiume akisha kabidhi binti yake kwa mume anaona sasa amemaliza kazi ya ulinzi wa binti yake na amekabidhi kwa mlinzi mwingine imara ambaye ni mume...!
 
Nata wala siyo mfumo dume kama wanaharakati wanavyotaka tuamini,ni kuwa hiyo nafasi si yao kwa minajili kwamba mume anapaswa kwajibika kwa vyote na avile ambavyo baba hakufanya kwa wakati huo sababu yeye ni mzazi kwa binti lakini kuingilia ya ndoa ya binti sababu yeye ni baba huanzisha mikwaruzo amabyo inaweza kuepukika
 
Lakini pia kuna baadhi ya akina baba huwa ni kero katika familia za watoto wao!!
 
yaani hii haitaisha leo wala kesho, na sio kwetu tu ni dunia nzima, ushaona movie monster in law? unaweza elewa ni kwa nini wamama tunakuwa vile, ni ile hali ya kutokubali kwamba watoto wetu tuliopata shida kuwalea leo hii kupata msaada kwake lazima upitie kwa mkewe, and the more unamheshimu mkwe na kuwa rafiki yake thhe more utafaidi vya mtoto wako. ukijifanya kuleta mdomo hutapata hata upande wa khanga.
 
Back
Top Bottom