Kwa hili mbunge wangu umechemsha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili mbunge wangu umechemsha!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ziada Mwana, Jun 22, 2011.

 1. Ziada Mwana

  Ziada Mwana JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MBUNGE wa Jimbo la Dole, Sylvester Mabumba (CCM), amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuifuta Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kushindwa kazi na jukumu la kupambana na rushwa na kazi hiyo sasa ipewe Idara ya Usalama wa Taifa.

  Akichangia mjadala wa bajeti ya msimu ujao wa fedha bungeni mjini Dodoma, alisema Takukuru imeshindwa kazi kwa kuwa vitendo vya rushwa na ufisadi vinazidi kuongezeka kwa kasi.

  “Mheshimiwa Spika naomba sasa kazi ya kupambana na rushwa ikabidhiwe kwa Idara ya Usalama wa Taifa na Takukuru ivunjwe mara moja,” alisema Mabumba.

  Alisema kama hilo litakuwa gumu, basi ni vizuri kama Rais Kikwete ataagiza kazi hiyo ya kupambana na rushwa sasa ifanywe kwa pamoja baina ya Takukuru na Idara ya Usalama wa Taifa ili kuongeza tija na ufanisi kuliko ilivyo sasa.

  Alitaka Idara ya Usalama wa Taifa pia iwachunguze viongozi wanaoiongoza Takukuru na maofisa wapya wanaotaka kuajiriwa na taasisi hiyo ili kubaini uadilifu waliokuwa nao.

  Sakata la wabunge kuivaa Takukuru, limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika vikao vya Bunge, kwa wabunge wengi kulalamikia uwezo mdogo wa Takukuru katika udhibiti wa vitendo vya rushwa na ufisadi nchini.(HABARI LEO 22 JUNE 2011)

  HAPO MBUNGE WANGU UMECHEMKA SANA, TENA SANA, TAKUKURU NI WATU SI MLIMA, NI IDARA NYETI SANA SERIKALINI. UTAWEZAJE KUIVUNJA? USALAMA WA TAIFA PIA NI WATU NYETI SANA SI WA KUKIMBIZANA NA KUPIGANA NA WALA RUSHWA MITAANI, AU HUJUI JINSI TAKUKURU WANAVYOWEKA MITEGO YAO NA HATA KUFIKIA HATUA YA KUTOANA MACHO NA WALA RUSHWA? JE HAO USALAMA WA TAIFA UNAOTAKA WAINGIE MITAANI NA KUANZA KUPIGANA WATAKUWA WANA PERFOM VIPI HIZO KAZI ZA KI USALAMA? LABDA UNACHOWEZA KUSHAURI NI KWAMBA WATU WOTE WA USALAMA WA TAIFA SASA WAHAMIE TAKUKURU ILI WAANZE JUKUMU JIPYA NA WALE WA TAKUKURU WATAFUTIWE KWA KWENDA.

   
 2. C

  Chipoku Member

  #2
  Jun 22, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  NAUNGA MKONO HOJA , NO NEED OF TAKUKURU & HII KAZI WASIPEWA GSO ie USALAMA WA TAIFA EITHRE COZ WOTE HAWA NI WA HAPAHAPA! MBUNGE WAKO ANA POINT , WEWE POINTLESS !
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  takukuru ifutiliwe mbali haina unyeti wowote ule bali wanakula mshahara wa bure tuu. mbunge ana point kubwa sana hapo.
   
 4. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ifutwe kama inashindwa kesi zaidi ya robo tatu haina maana
   
 5. k

  kashwagala Senior Member

  #5
  Jun 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtoa thread umejichanganya,unapinga na kukubaliana na mbunge wako wakati huo huo,kimsingi sijakuelewa.Kwa maoni yangu Takukuru hawanishawishi kama wamefanikiwa kutimiza lengo la uwepo wake,kwa hiyo nakubaliana na mbunge.
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  what is the difference btn TAKUKURU na Usalama wa taifa ktk suala la rushwa?

  kazi ya kudeal na mafisadi wakabidhiwe vyama vya upinzani
   
 7. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  nimepita hapa.
   
 8. Dr-of-three-Phd

  Dr-of-three-Phd Senior Member

  #8
  Jun 22, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapa aliyechemka ni huyo mbunge ni wewe unayeona pafupi!

  TAKUKURU hawawezi kazi, la organ yenyewe iwe huru itokane na Bunge la mambo ni yale yale!

  Aluta Continua!

   
 9. Junior. Cux

  Junior. Cux JF-Expert Member

  #9
  Jun 22, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 5,305
  Likes Received: 1,226
  Trophy Points: 280
  nyie hamjui.!! Mtoa thread ni mfanyakazi wa takukuru sa mnafikiri ataenda wapi baada ya hapo.!? lazima atetee masilahi yake...
   
 10. p

  pat john JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi ya TAKUKURU & USALAMA WA TAIFA ni kulinda mafisadi. Hela za EPA, MELEMETA, DEEP GREEN FINANCE, KIWIRA, RADA, nk vilfanyika watu hao wakiwepo. Walichokkifanya ni kutetea Richmond na maovu mengine. Usalama wa Taifa marekani hufuatilia mwenendo wa hali ya dunia kila nyanja ili kulinda maslahi ya Tifa hilo. Hapa kwetu wanamagamba mafisadi wanalindwa na vyombo hivyo. Hakuna hata sababu ya kuwa navyo. Vyama vya upinzani vyaweza kugundua rushwa pamoja na vyombo vya habari. Polisi watapeleleza na kuwafikisha wahusika mahakamani. Takukuru haina maana ya kuwepo, na kama kuna haja ya kuwepo basi iwe chini ya BUNGE.
   
 11. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kuvunja takukuru si jawabu maana hata hao usalama wa taifa walishageuka na kuwa usalama wa matumbo yao. tofauti ni kwamba wao wanajua kuzima juu kwa juu issue zisitawanyike!
  kwa nini mjiulize maswali haya:-
  1. Lada kwa nini ilisafishwa hapa bongo mpaka waingereza wakakomalia nasi kwa kuondoa aibu tunajidai fedha lazima irudishwe?
  2. Skandinali ya Dowans mbona iliminywa mpaka walipodhulumiana ndiyo ikatoka? kwa nini zile za IPTL, Songas na nyingine hazikuwahi kunyooshewa kidole ilhali nature ni ileile
  3. Uchakachuaji wa kura mbona kila mwenye macho aliuona na hakuna mh!
  na orodha nyingine nyingi sana!
  Hapa cha msingi ni kueliimisha watanzania waache u-limbukeni. hicho ndiyo chanzo cha Rushwa!
   
 12. Ziada Mwana

  Ziada Mwana JF-Expert Member

  #12
  Jun 22, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  wapi nimejimix mzee wangu?
   
 13. Ziada Mwana

  Ziada Mwana JF-Expert Member

  #13
  Jun 22, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmmmmmm! mimi ni mkulima tu ndugu yangu,elimu yenyewe niliyonayo ndo ile ya umande. sifanyi kazi huko.
   
 14. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #14
  Jun 22, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kaka unagusa kazi za watu kuwa makini.
   
 15. oba

  oba JF-Expert Member

  #15
  Jun 22, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hapo ni kama kuruka mkojo na kukanyaga mavi, hao ni usalama wa taifa au usalama wa ccm, mali za taifa zinaibiwa mfano madini migodini, twiga mbugani n.k hatuoni hao usalama wa taifa wakifanya ujasusi wa kulinda mali hizo na wezi , wataweza hiyo ya takukuru?hakuna kitu hapo tumeliwa!fumua fumua kote kote, si usalama wala takukuru wenye sifa ya kutulinda na mafisadi kwa sasa!
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  just give me one advantage of takukuru... and compare with government expenses tulizokwisha ingia kama nchi

  my heart was broken during ccm primaries where the boys were really in for some colours
   
 17. Ziada Mwana

  Ziada Mwana JF-Expert Member

  #17
  Jun 22, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka, yeye ndio amegusa kazi za watu.awe makini.
   
Loading...