usiniguse
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 1,725
- 1,189
Ndugu wanabodi mie ni miongoni mwa waathirika wa watumishi ambao vyeti vyao vinatumika zaidi ya sehemu moja.
Jana nilikuwa baraza la mitihani tanzania nilifika saa 12:00 asubuhi nikiamini nimewahi lakini nilipata namba yakuanzia 70.Mida ya saa mbili akaja mtu wa baraza ,baada ya kuona nyomi ile akaamua kupunguza waliowahi na kutuingiza ukumbini kusubiria muda wa uhakiki.Huyu bwana ambae sikubahatika kujua jina lake alikuwa muungwana wa kutosha, kumbuka mvua ilikuwa inanyesha wakati huo.
Kikubwa alichotwambia baraza kwa sasa wanashughulikia matatizo matatu tu
Moja, vyeti vyenye utata kwa maana vinavyotumika zaidi ya mara moja
Mbili, vyeti ambavyo havikukamilika yaani incomplete kwa wale waliowasilisha baadhi ya vyeti
Tatu, wanaokata rufaa kupinga vyeti feki.
Muda ulipofika nilikabidhi vyeti vyangu vyote original ambavyo nimefanya mitihani ya baraza na kukabidhiwa fomu ya makabidhiano .
Jina langu nimetokea Halmashauri 3 yaani Halmashauri X,Y na Z.Mpaka mwaka 2015 nilikuwa mtumishi wa Halmashauri X nikapewa promotion kwa uteuzi wa katibu mkuu TAMISEMI kwenda Halmashauri Y ambayo imekuwa na hadhi ya Mji kutoka Halmashauri Z.
Zoezi la uhakiki lilipoanza ambalo kimsingi lilikuwa linaendeshwa na wakuu wa wilaya, lilijaa vitisho vingi kuhusu kufungiwa mshahara kama hutahakikiwa.Mpaka leo hii nimejaribu kuhamisha mshara kutoka Halmashauri X kuja Y bila mafanikio kwani mhusika wa kuhamisha mshahara ni Afisa Utumishi wa Halmashauri X na kazi hiyo kashaifanya ila Mhusika wa Wizara ya Utumishi anayetakiwa kuverify hajafanya kazi yake kuhamisha kunaonekana KUPO PENDING kwenye system.Kwahiyo uhakiki ulipoanza niliitwa kwenda kuhakiki Halmashauri X,baada ya mwezi Halmashauri Y nao wakapitisha uhakiki nikaambiwa nilazima nipeleke vyeti kwani mimi ni mtumishi wao ,kwakuwa Halmshauri hii imezaliwa kutoka Halmashauri z ,uhakiki ulifanyika pamoja kwani vyeti vilitakiwa vyote viende kwa RAS,nikatoa copy nikapeleka.Baada ya siku mbili Afisa utumsishi wetu akaja nakuniambia vyeti vyangu havijaonekana nikamwambia nimepeleka ,kwakuwa walikuwa kwenye harakati za kuondoka kuvipeleka wakaniomba nitoe copy nikatwapa,kumbe wakawa wamepeleka copy zote moja Halmashauri Y na nyingine Z,nDIYO maana nimetokea Halmashauri zote tatu.
Utumishi badala ya kukimbilia kukabidhi majina kama yalivyotoka Baraza walitakiwa wajithibitishie kama kweli majina haya yanapokea mshahara zaidi ya mmoja,na kama hili lingefanyika basi hiyo idadi ya vyeti vyenye utatata ingepungua sana kwani hapa idarani watumishi watatu tulioletwa kutoka Halmashauri tofauti wote tumekumbwa na tatizo hilo.
Wasiwasi wangu inavyoonesha Wizara ya utumishi hawajatimiza wajibu wao,nahofu ya kukosa mshahara wa mwezi huu kwani pamoja na uhakiki nilioufanya baraza nitathibitika ni mtumishi halali wa Halmashauri Y lakini mshahara wangu upo Halmshauri X ambao naamini wataufungia tu.