Stabilaiza
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 1,843
- 1,143
Ninaamini kwa dhati kuwa Pinda anaonewa kutakiwa kujiuzulu kwa yaliyotokea katika utekelezaji wa operasheni tokameza. Pinda hatakiwi kujiuzulu wala kulazimishwa kujiuzulu. Anayetakiwa kujiuzulu ni rais Kikwete. Tukumbuke aliyosema rais Kikwete hivi karibuni wakati akilihutubia bunge kuhusu Afrika Mashariki. Alitetea oparesheni tokomeza akijitetea kuwa hata watangulizi wake kama hayati Baba wa taifa Mwl Nyerere waliwahi kuanzisha kampeni dhidi ya majangili ili kutunza maliasili.
Kama oparesheni tokameza inamkono wa Kikwete kwanini Pinda aonewe kwa kutakiwa kujiuzulu? Huu ni uonevu wa waziwazi kwake. Pinda alitakiwa kujiuzulu pale aliposema wapigwe tu, maana tumechoka, lakini siyo kwa suala hili la oparesheni tokomeza ambalo linamkono wa rais. Wanaotakiwa kujiuzuru ni JK na mawaziri wote waliotekeleza vibaya oparesheni hiyo. Umuhimu wa kujiuzulu JK na siyo Pinda unaongezewa nguvu na maelezo ya Mh. Msingwa aliyesema kuwa CCM imechakaa, kila atakayechaguliwa atafanya vilevile. Aliongezea kwa kusema kuwa tatizo ni CCM inayotakiwa kuondolewa madarakani ili kuwalinda rais wasiokuwa na hatia. Hivi karibuni Dr. Slaa pia amefafanua kuwa huwezi ukasema mawaziri ni mizigo ukaacha kumtaja aliyewateua ambaye ni Kikwete. Hivyo kwa suala hili la uparesheni tokomeza ni kumwonea Pinda kumwambia ajiuzulu.