Kwa hili la tokomeza Mh. Pinda anaonewa

Amani Karume alishawahi kusema hawezi kumuwajibisha Waziri wake kwa kumuachisha kazi kwani hatuna utamaduni wa kuwajibika. That was a candid moment.

Na hata sasa hatajiuzulu mtu yeyote, kwa sababu hiyo hiyo.

Nyerere kama kafanya summary execution kwa sababu enzi zake hakukuwa na rule of law, vyama vingi, transparency, media coverage, internet etc, Kikwete naye aige hivyo hivyo?

Kwa sababu Nyerere alifanya tu?

Hapo sasa, lakini ndivyo alivyojitetea Kikwete wakati wa hotuba kwa Bunge
 
Yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na kauli ya mbiu ya wapigwe iliotolewa na PM!

Kama kuna kiongozi wa kwanza aliyepaswa kuwajibika ili kuonyesha mfano wa utawala bora ni PM.
 
Rais hasimamii utendaji! Mtendaji ni Waziri Mkuu.., Tumia akili... Rais anawajibika tu kama alisema watekeleze hivyo!
Kwa Tanzania waziri mkuu hana nguvu ya kuamua juu ya mawaziri, ni mamlaka ya rais
 
Yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na kauli ya mbiu ya wapigwe iliotolewa na PM!

Kama kuna kiongozi wa kwanza aliyepaswa kuwajibika ili kuonyesha mfano wa utawala bora ni PM.

Kwa kauli ya wakati ule kuwa wapinzani wapigwe tu alisitahili kujiuzulu, lakini siyo hii kampeni ya tokomeza ambayo inamkona wa rais, soma post ya uzi huu.
 
Ninaamini kwa dhati kuwa Pinda anaonewa kutakiwa kujiuzulu kwa yaliyotokea katika utekelezaji wa operasheni tokameza. Pinda hatakiwi kujiuzulu wala kulazimishwa kujiuzulu. Anayetakiwa kujiuzulu ni rais Kikwete. Tukumbuke aliyosema rais Kikwete hivi karibuni wakati akilihutubia bunge kuhusu Afrika Mashariki. Alitetea oparesheni tokomeza akijitetea kuwa hata watangulizi wake kama hayati Baba wa taifa Mwl Nyerere waliwahi kuanzisha kampeni dhidi ya majangili ili kutunza maliasili.

Kama oparesheni tokameza inamkono wa Kikwete kwanini Pinda aonewe kwa kutakiwa kujiuzulu? Huu ni uonevu wa waziwazi kwake. Pinda alitakiwa kujiuzulu pale aliposema wapigwe tu, maana tumechoka, lakini siyo kwa suala hili la oparesheni tokomeza ambalo linamkono wa rais. Wanaotakiwa kujiuzuru ni JK na mawaziri wote waliotekeleza vibaya oparesheni hiyo. Umuhimu wa kujiuzulu JK na siyo Pinda unaongezewa nguvu na maelezo ya Mh. Msingwa aliyesema kuwa CCM imechakaa, kila atakayechaguliwa atafanya vilevile. Aliongezea kwa kusema kuwa tatizo ni CCM inayotakiwa kuondolewa madarakani ili kuwalinda rais wasiokuwa na hatia. Hivi karibuni Dr. Slaa pia amefafanua kuwa huwezi ukasema mawaziri ni mizigo ukaacha kumtaja aliyewateua ambaye ni Kikwete. Hivyo kwa suala hili la uparesheni tokomeza ni kumwonea Pinda kumwambia ajiuzulu.

Pinda ni mkristo tunataka viongozi wote waislam
 
Back
Top Bottom