Kwa hili la tokomeza Mh. Pinda anaonewa

Stabilaiza

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
1,843
2,000
Ninaamini kwa dhati kuwa Pinda anaonewa kutakiwa kujiuzulu kwa yaliyotokea katika utekelezaji wa operasheni tokameza. Pinda hatakiwi kujiuzulu wala kulazimishwa kujiuzulu. Anayetakiwa kujiuzulu ni rais Kikwete. Tukumbuke aliyosema rais Kikwete hivi karibuni wakati akilihutubia bunge kuhusu Afrika Mashariki. Alitetea oparesheni tokomeza akijitetea kuwa hata watangulizi wake kama hayati Baba wa taifa Mwl Nyerere waliwahi kuanzisha kampeni dhidi ya majangili ili kutunza maliasili.

Kama oparesheni tokameza inamkono wa Kikwete kwanini Pinda aonewe kwa kutakiwa kujiuzulu? Huu ni uonevu wa waziwazi kwake. Pinda alitakiwa kujiuzulu pale aliposema wapigwe tu, maana tumechoka, lakini siyo kwa suala hili la oparesheni tokomeza ambalo linamkono wa rais. Wanaotakiwa kujiuzuru ni JK na mawaziri wote waliotekeleza vibaya oparesheni hiyo. Umuhimu wa kujiuzulu JK na siyo Pinda unaongezewa nguvu na maelezo ya Mh. Msingwa aliyesema kuwa CCM imechakaa, kila atakayechaguliwa atafanya vilevile. Aliongezea kwa kusema kuwa tatizo ni CCM inayotakiwa kuondolewa madarakani ili kuwalinda rais wasiokuwa na hatia. Hivi karibuni Dr. Slaa pia amefafanua kuwa huwezi ukasema mawaziri ni mizigo ukaacha kumtaja aliyewateua ambaye ni Kikwete. Hivyo kwa suala hili la uparesheni tokomeza ni kumwonea Pinda kumwambia ajiuzulu.
 
Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,700
1,225
Rais hasimamii utendaji! Mtendaji ni Waziri Mkuu.., Tumia akili... Rais anawajibika tu kama alisema watekeleze hivyo!
 
oyaoya

JF-Expert Member
Mar 4, 2012
277
170
Hivi utaratibu wa kumwambia rais ajiuzulu unakuwaje, naiona point ya mleta mada kwa ukaribu sana...!?
 
Stabilaiza

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
1,843
2,000
Rais hasimamii utendaji! Mtendaji ni Waziri Mkuu.., Tumia akili... Rais anawajibika tu kama alisema watekeleze hivyo!

Siyo kweli. Anayeteua mawaziri ni rais. Pinda alishasema kuwa mwenye mamlaka ya kuwawajibisha mawaziri ni rais
 
Mwanamume

Senior Member
Jan 3, 2013
185
225
Nakubaliana na wewe. Lakini nadhani bunge linamtaka Pinda awajibike kwa kuwa ndiyo wigo wake wa kimamlaka unaishia kwake. Halafu kwa Tanzania yetu naona kama wabunge wanalalamika tu. Hawachukui hatua za kisheria kama vile kukusanya saini zao kwa lengo la kuwawajibisha hao wanao wataja.
 
Threesixteen Himself

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
8,206
2,000
!
!
umenikosha sana mkuu, sana yaani hapa wa kujiuzulu ni JK mwenyewe..................yule mzee wa watu na sura yake anaweza kumwaga chozi tena bungeni yakawa kama yale yale katika mauaji ya albinoNinaamini kwa dhati kuwa Pinda anaonewa kutakiwa kujiuzulu kwa yaliyotokea katika utekelezaji wa operasheni tokameza. Pinda hatakiwi kujiuzulu wala kulazimishwa kujiuzulu. Anayetakiwa kujiuzulu ni rais Kikwete. Tukumbuke aliyosema rais Kikwete hivi karibuni wakati akilihutubia bunge kuhusu Afrika Mashariki. Alitetea oparesheni tokomeza akijitetea kuwa hata watangulizi wake kama hayati Baba wa taifa Mwl Nyerere waliwahi kuanzisha kampeni dhidi ya majangili ili kutunza maliasili.

Kama oparesheni tokameza inamkono wa Kikwete kwanini Pinda aonewe kwa kutakiwa kujiuzulu? Huu ni uonevu wa waziwazi kwake. Pinda alitakiwa kujiuzulu pale aliposema wapigwe tu, maana tumechoka, lakini siyo kwa suala hili la oparesheni tokomeza ambalo linamkono wa rais. Wanaotakiwa kujiuzuru ni JK na mawaziri wote waliotekeleza vibaya oparesheni hiyo. Umuhimu wa kujiuzulu JK na siyo Pinda unaongezewa nguvu na maelezo ya Mh. Msingwa aliyesema kuwa CCM imechakaa, kila atakayechaguliwa atafanya vilevile. Aliongezea kwa kusema kuwa tatizo ni CCM inayotakiwa kuondolewa madarakani ili kuwalinda rais wasiokuwa na hatia. Hivi karibuni Dr. Slaa pia amefafanua kuwa huwezi ukasema mawaziri ni mizigo ukaacha kumtaja aliyewateua ambaye ni Kikwete. Hivyo kwa suala hili la uparesheni tokomeza ni kumwonea Pinda kumwambia ajiuzulu.
 
Stabilaiza

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
1,843
2,000
Nakubaliana na wewe. Lakini nadhani bunge linamtaka Pinda awajibike kwa kuwa ndiyo wigo wake wa kimamlaka unaishia kwake. Halafu kwa Tanzania yetu naona kama wabunge wanalalamika tu. Hawachukui hatua za kisheria kama vile kukusanya saini zao kwa lengo la kuwawajibisha hao wanao wataja.

Pinda hana mamlaka ya kuwawajisha mawaziri bali rais
 
MTIMBICHI

JF-Expert Member
Apr 15, 2013
947
225
Wamemfanya mbuzi wa kafara nchi nzima tumejua. Lkn hawataweza taratibu hotuba zao zinawataja kwa vyeo au chama tutawajua tuu
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
54,686
2,000
Amani Karume alishawahi kusema hawezi kumuwajibisha Waziri wake kwa kumuachisha kazi kwani hatuna utamaduni wa kuwajibika. That was a candid moment.

Na hata sasa hatajiuzulu mtu yeyote, kwa sababu hiyo hiyo.

Nyerere kama kafanya summary execution kwa sababu enzi zake hakukuwa na rule of law, vyama vingi, transparency, media coverage, internet etc, Kikwete naye aige hivyo hivyo?

Kwa sababu Nyerere alifanya tu?
 
data

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
22,792
2,000
pinda ilibidi afanye monitoring ya hiyo operation na atoe taarifa mapema... Haponi hapa.
 
Sokoine2

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
214
170
Nimependa mbunge mmoja amesema serikali yetu inanyanyasa wananchi wake kuliko hata wakoloni walivyokuwa wananyanyasa watumwa! Tena ni mbunge wa chama cha mizigo aliyesema hayo!
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,614
2,000
Walitegemea taarifa za kina mwema, chagonja, kova, advera, kamuhanda, ighondu n.k unadhani nini kitatokea.

Itakuwa ni hasara ccm kuendelea kuwepo, ingawa hivyo
Pangua pangua yoyote itaunufaisha upinzani.
 
wakuwaza

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
316
225
Pinda hana mamlaka ya kuwawajisha mawaziri bali rais

Uwezo anao, tena kwa namna fulani anao uwezo mkubwa kuliko Rais. Akijiuzulu tu yeye na baraza lote la mawaziri linavunjika dakika hiyo hiyo. Afanye hiyo Kama hakumrahisishia Rais kazi ya kuwawajibisha mawaziri.
 
The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
6,560
2,000
Ninaamini kwa dhati kuwa Pinda anaonewa kutakiwa kujiuzulu kwa yaliyotokea katika utekelezaji wa operasheni tokameza. Pinda hatakiwi kujiuzulu wala kulazimishwa kujiuzulu. Anayetakiwa kujiuzulu ni rais Kikwete. Tukumbuke aliyosema rais Kikwete hivi karibuni wakati akilihutubia bunge kuhusu Afrika Mashariki. Alitetea oparesheni tokomeza akijitetea kuwa hata watangulizi wake kama hayati Baba wa taifa Mwl Nyerere waliwahi kuanzisha kampeni dhidi ya majangili ili kutunza maliasili.

Kama oparesheni tokameza inamkono wa Kikwete kwanini Pinda aonewe kwa kutakiwa kujiuzulu? Huu ni uonevu wa waziwazi kwake. Pinda alitakiwa kujiuzulu pale aliposema wapigwe tu, maana tumechoka, lakini siyo kwa suala hili la oparesheni tokomeza ambalo linamkono wa rais. Wanaotakiwa kujiuzuru ni JK na mawaziri wote waliotekeleza vibaya oparesheni hiyo. Umuhimu wa kujiuzulu JK na siyo Pinda unaongezewa nguvu na maelezo ya Mh. Msingwa aliyesema kuwa CCM imechakaa, kila atakayechaguliwa atafanya vilevile. Aliongezea kwa kusema kuwa tatizo ni CCM inayotakiwa kuondolewa madarakani ili kuwalinda rais wasiokuwa na hatia. Hivi karibuni Dr. Slaa pia amefafanua kuwa huwezi ukasema mawaziri ni mizigo ukaacha kumtaja aliyewateua ambaye ni Kikwete. Hivyo kwa suala hili la uparesheni tokomeza ni kumwonea Pinda kumwambia ajiuzulu.

Kwa hili mkuu hata wale walioanzisha movement hii wanatambua!!....Hapa kuna haya;

  1. Wabunge kamwe hataweza kumwajibisha Rais kwani uwepo wake,ndiyo uwepo wao at least hadi ile 2015 wavute mafao ya kutumia kwenye kampeni za kurejea mjengoni.
  2. Hili linatuleta kwenye la pili kwamba ni wazi wanampingia kengele Rais achukue hatua iwapo hatapenda kuadhirika tena kwa kubadili PM na Cabinet yote kwa mara ya (........?)
  3. Mwisho huyu jamaa JK ni kichwa maji na ni msanii wa ovyo kabisa,ni wazi anataka anataka kumtoa Pinda awe sadaka,na kwa hili hata mimi nasema anatolewa kama kondoo wa kafara kwa Maccm,na hili Pinda analijua kabisaaaa!. Mwenzie EL hili mwaka 2008 aliliona mapema na kwa hasira akajiuzuru kwa kuwaambia waliomwandama na kumwacha mzee wa kazi fisadi mkuu wa mpango mzima wa Richmond JK, kama ishu ni u-PM chukueni
 
Stabilaiza

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
1,843
2,000
pinda ilibidi afanye monitoring ya hiyo operation na atoe taarifa mapema... Haponi hapa.

Sasa hata kama alitoa taarifa, kama kampeni inamkono wa rais unadhani Pinda atafanya nini? Kiufupi mamlaka ya kuwawajibisha mawaziri ni rais na nivyo ilivyotokea.
 
Stabilaiza

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
1,843
2,000
Kwa hili mkuu hata wale walioanzisha movement hii wanatambua!!....Hapa kuna haya;

  1. Wabunge kamwe hataweza kumwajibisha Rais kwani uwepo wake,ndiyo uwepo wao at least hadi ile 2015 wavute mafao ya kutumia kwenye kampeni za kurejea mjengoni.
  2. Hili linatuleta kwenye la pili kwamba ni wazi wanampingia kengele Rais achukue hatua iwapo hatapenda kuadhirika tena kwa kubadili PM na Cabinet yote kwa mara ya (........?)
  3. Mwisho huyu jamaa JK ni kichwa maji na ni msanii wa ovyo kabisa,ni wazi anataka anataka kumtoa Pinda awe sadaka,na kwa hili hata mimi nasema anatolewa kama kondoo wa kafara kwa Maccm,na hili Pinda analijua kabisaaaa!. Mwenzie EL hili mwaka 2008 aliliona mapema na kwa hasira akajiuzuru kwa kuwaambia waliomwandama na kumwacha mzee wa kazi fisadi mkuu wa mpango mzima wa Richmond JK, kama ishu ni u-PM chukueni
Hapo umenena, lakini Pinda asionewe kwa hili.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom