Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 11,208
- 19,000
Nilisema wazi, kwamba kuna ajali nyingi sana na watu kufa nchini na sababu kubwa ni uzembe wa TANROADS, wala sio suala la madereva. Ndio kuna ajali zinazotokea kutokana na uzembe wa madereva, lakini si kila ajali inatokana na uzembe wa dereava. Dereva anaweza kuwa mzembe na kusababisha ajali katika sehemu ambayo TANROADS wamefanya uzembe, sehemu ambayo kama TANROADS wasingekuwa wamefanya uzembe, uzembe wa dereva usingesababisha ajali (TANROADS negligence compounded by driver's negligence).
Nilisisitiza sana kwamba Mfugale anafanya matumizi mabaya ya fedha ya kurekebisha barabara ambayo tunachangia kila tunaponunua mafuta (Road Maintenance Fund)
Ajali iliyoua watu 6 Dodoma: Wanaopaswa kukamatwa na kuwekwa ndani ni Mfugale na Meneja wa Dodoma wa TANROADS Dodoma, sio dereva wa lori
Mfugale awavimbia Waziri Mkuu na Waziri wa Ujenzi kwa kivuli cha Rais Magufuli?
Ndio maana nilisema;
Magufuli atoe amri kwa Mfugale kwamba kuanzia sasa sitaki kusikia ajali imetokea kwenye barabara kuu za lami za TANROADS na chanzo eti kulikuwa na gari ikikwepa shimo dereva aliloona ghafla katikati ya barabara, au daraja limekatika
Je Magufuli amesikia? Angalia hii clip.

- Kila meneja wa mkoa wa TANROADS, fanya ukaguzi wa kila wakati wa barabara kuu zote za lami na kuhakikisha eidha mashimo yamefukiwa permanently au kwa hatua za muda
- Shimo lolote lililofukiwa kwa hatua za muda sehemu hiyo iwekwe alama za tahadhali kwa madereva kuwaonya juu ya uwepo wa shimo kubwa barabarani. Kwa hiyo wakaguzi watembee na alama za onyo kuweka barabarani
- KIla mvua kubwa ikinyesha TANROADS wapite kufanya ukaguzi barabarani kuhakikisha hakuna vifusi vilivyuporomokea barabarani au madaraja kuathirika au kuwa na takataka zinazozuia maji.
- Kila Mkoa wa TANROADS uwe na kikosi cha kazi cha kurekebisha barabara kwa muda na kiwe on call masaa 24 kwa siku katika siku saba za juma
- TANROADS wawe na call centre ya road emergency na watoe namba za simu za emergency au watumie 112 ili madereva wanapoona hali mbaya barabarani wawapigie na watatue hilo tatizo mara moja. Namba hizi zitangazwe kikamili pamoja na kuwekwa kwenye stika za insurance ili watu wazione na kuzijua
Je Magufuli amesikia? Angalia hii clip.