TANROADS waruhusu Malori yapite katikati kuanzia Kimara hadi Kibaha

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,305
12,969
Mimi naushauri TANROADS waruhusu malori yawe yanapita barabara ya katikati kabisa ambayo inaonekana imetengwa kwaajili ya mabasi ya mwendokasi.

Barabara ile ambayo ndiyo ilikuwa barabara kuu zamani kabla ya kuongezwa na kuwa njia nane imekuwa haitumiki kwa muda mrefu sasa bila shaka ni kutokana na ugumu wa mwendokasi kupakia na kushusha abiria ikiwa zitapita kule kwakuwa ili dereva aweze kushusha na kupakia abiria ni lazima akifika kituoni ahame kwenye njia yake halafu apangue njia tatu za kushoto ili aingie pembeni kabisa kituoni kushusha na kupakia na kisha akiondoka aanze tena kutafuta nafasi ya kurudi kwenye njia yake kwa kupangua njia tatu. Ikumbukwe wakati huo dereva anahangaika magari mengine katika njia tatu za kulia na kushoto yanakuwa yanapita.

Ni ngumu sana na ni hatari sana kiusalama kwakuwa sehemu kubwa atategemea fair ya wanaopita kushoto kwake wakati yeye yupo kulia. Kwa mazingira hayo napendekeza mwendokasi waendelee kutumia hizi lanes sita, tatu za kulia na tatu za kushoto n badala ya zile mbili za katikati labda mpaka watakapojenga vituo vya katikati kama ilivyo kuanzia Kimara kwenda Kariakoo.

Vile vile TANROADS iweke sheria za matumizi ya lanes sita zilizobaki. Iwe ni marufuku kwa bajaji, daladala na mwendokasi kupita lane ya kulia kabisa kwakuwa wao wanasimama mara kwa mara kila baada ya mita 500 Lane ya kulia kabisa katika zile tatu za kushoto na kulia iwe ni EXPRESS kwa magari yaendayo kasi iliwa ni pamoja na Ambulance ambayo mwendo wake iwe angalau 80kmph. Akionekana bajaji anaweka giza huko apigwe makofi na karatasi juu yake. Huwa najiuliza bajaji anatafuta nini kulia kabisa ambako unakuta mtu katoka mkoani na roli au basi kanyoosha mguu ghafla anakutana na kitenga mbele yake hata hakitembei wakati lanes mbili kulia kwake ziko wazi.

Naomba TANROADS ifanyie kazi haraka maoni yangu na kama yanafaa na wakatekeleza basi wasikose kunilipa kwaajili ya hati miliki ya maoni yangu ambayo nimeyatoa baada ya kufanya utafiti kwa miaka mitatu kwa gharama kubwa.
 
Wakifanyia kazi maoni yako mtakimbizana weee ghafla mnaenda kunasa Kimara njia mbili!

Kuna mdau alishauri humu jf ifike mahali double roads kwa high traffic areas iwe marufuku miji mikubwa; badala yake at least triple ways.

Kimsingi kwa uzoefu wa barabara mpya ya Kimara-Kibaha the third lane is important for overtaking. Ikikosekana ni mafoleni ya kijinga. Tanroads waachane na mazoea ya kizamani ya double roads ambazo hazipunguzi tatizo kwa kiwango kikubwa miji mikubwa!
 
Back
Top Bottom