Kwa hili inabidi tuwe na imani kali

Kwa hili inabidi tuwe na imani kali

Miaka 7. Yaani maisha haya mtoto wa miaka 7 unamfundisha kuwanga.
Kakichangamka kidogo kataanza kuruka na ungo.Binamu alikuwa na nia njema labda ambacho huyo mgombea mwenza hajui kuwa binamu ndo Mrs everything angejua kuwa huyo HB sio anae weka mkate mezani angeijutia pesa yake aliyompa matunge(mganga )
 
Binamu yangu aliolewa na kuishi na mume wake kwa raha, walijaliwa kupata watoto wawil, wa kwanza alikuwa wa kiume, na wakike. Wote wakikwa waajiriwa.

Weekend moja wakati binamu yangu anafua nguo za mume wake, akakuta barua inamjulisha yule mwaume mahitaji ya mtoto wake. Binamu alichanganyikiwa, aliamua kumaliza kufua, akalitafakari swala lile, mwisho akasubiri siku mumewe akiwa na raha sana ndiyo akamuuliza taratibu.
Jamaa akajieleza kuwa alipata mtoto lakini mazingira ya kuzaliwa mtoto mwenyewe hayakuandaliwa, na walikubaliana na mzazi mwenzake kuwa atakuwa anamtunza mtoto huko aliko.

Binamu yangu akaja kugundua yule mtoto na matoto wake wa kwanza wamepishana kama miaka miaka miwili hivi. Akamwambia mume wake, ni kheri watoto wajuane na walelewe pamoja ili tabia zao zisipishane pia wajenge upendo. Mama wa yule mtoto alikataa kumwachia mtoto wake ahamie pale na kulelewa na mama wa kambo. Binamu akamwambia yule mama hivyo utakuwa unamkosesha mtoto mapenzi ya baba yake. Basi mama alikubali mtoto awe anakuja likizo kwa baba yake.

Mazingira anayoishi yule mtoto ni tofauti ya wenzake, binamu akaanza kumfanyia mtoto shopping, kumnunulia games na toys, ect. Likizo ilipokwisha akanunuliwa vifaa vya shule na zawadi kwa mama yake.

Likizo iliyofuata mambo yalianza kubadilika ndani ya nyumba, baada ya yule mtoto kuja, Amani ndani ya nyumba ilipotea, ikawa binamu na mume wake kugombana. Binamu ni mwana maombi wa nguvu. Sasa siku moja ilikuwa Jmosi, akamkuta yule mtoto yuko jikoni peke yake, akamuuliza unafanya nini huku, watoto hawaruhusiwi jikoni bila kuwepo na mkubwa karibu? Kumchunguza mtoto alikuwa amewasha jiko anataka kuchoma unga unga ulikuwa kwenye karatasi.

Binamu akaanza kutetemeka, ndiyo mtoto kuulizwa kwa kirefu akajieleza kuwa ule unga alipewa na mama yake, akiuchoma basi Amani ipotee ndani ya nyumba na mwisho wa siku waachane ili mama aje kukaa yeye. Binamu ngachoka, ikaamuliwa matumizi ya yule mtoto yamfuate huko huko kwa mama yake.

Ooh Lord help us.. Open up our eyes to be more wide..in Jesus name.. Amen.. Thanks..
 
Si kupenda mama yngu kua mama wakmbo baada ya mzee kumjulsha alikua na binti amezaa inje mkubwa(20)......
Kiukweli tabia zinatofaut asikudanganye mtu....
Alimtangza vibya mama..
 
kuna kitu ni muhimu sana nimejifunza, mwanamke yeyote unaekutana nae kingono ni muhimu kutumia kinga, maana kiukweli kuna wanawake tunakutana nao unajuliza akikuambia ana mimba yako utafanyaje na ndo matokeo ya hawa watoto na wana changamoto kubwa sana, leo tunalalamika kuna majambazi, wanga, vibaka ukiangalia chimbuko hutawalaumu. mtoto katelekezwa na mama kwa baba, na baba kampeleka kwa mama yake, mtoto analelewa na bibi kipindi chote. kama huna mtoto hakikisha unampatia kwenye ndoa, na hapo tutakua tumetatua mzizi wa tatizo.
 
Asante sana kwa mawazo yako, binamu pia aliwaza hili, hivi baadae future ya huyu mtoto itakuwaje, mwisho wa siku atakuwa mzigo kwa wenzake, ni kheri nianze mapema kunyoosha maisha yake.
 
Asante sana kwa mawazo yako, binamu pia aliwaza hili, hivi baadae future ya huyu mtoto itakuwaje, mwisho wa siku atakuwa mzigo kwa wenzake, ni kheri nianze mapema kunyoosha maisha yake.
na ni mzigo sio kidogo. na bora angekuwa mzigo kwa vitu ambavyo ni rahisi kusaidia, vipi kama tatizo sasa ni tabia. kuna wakati ambao itabidi kuachana nae maana anaweza akawa chanzo cha kuvunjika amani tena na kipindi hiki ikashindikana ku solve.MUNGU amsaidie sana
 
I will raise a kid as God raise us,it doesnt matter tumezaliwa kwenye ndoa au la! Mkaribisheni Mungu atawale maisha yenu,hakuna nguvu ya kushindana na Mungu. Spread LOVE
 
I will raise a kid as God raise us,it doesnt matter tumezaliwa kwenye ndoa au la! Mkaribisheni Mungu atawale maisha yenu,hakuna nguvu ya kushindana na Mungu. Spread LOVE

Hakuna mtu anaechagua azaliwe kwenye mazingira gani lakini tunahitaji ku accept hali ilivyo na pia appreciate pale unapopewa msaada. Kikubwa ni kumtanguliza Mungu kama ulivyosema.
 
mwambie binamu azidishe imani sababu vita ndo kwanza inaanza, kwa nnavyo elewa mm hao watu wanaoamini ushirikina they dont just giveup kirahisi.
 
mwambie binamu azidishe imani sababu vita ndo kwanza inaanza, kwa nnavyo elewa mm hao watu wanaoamini ushirikina they dont just giveup kirahisi.

Maisha yangekuwa ya kheri na upendo kama hawa wanawake wawili wangeelewana, ingekuwa rahisi sana kwa mama mtoto kuleta zawadi kama appreciation ya yale anayofanyiwa mtoto wake. Katika vita mara nyingi hasara ni kubwa kuliko faida.
 
Back
Top Bottom