Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,775
Binamu yangu aliolewa na kuishi na mume wake kwa raha, walijaliwa kupata watoto wawil, wa kwanza alikuwa wa kiume, na wakike. Wote wakikwa waajiriwa.
Weekend moja wakati binamu yangu anafua nguo za mume wake, akakuta barua inamjulisha yule mwaume mahitaji ya mtoto wake. Binamu alichanganyikiwa, aliamua kumaliza kufua, akalitafakari swala lile, mwisho akasubiri siku mumewe akiwa na raha sana ndiyo akamuuliza taratibu.
Jamaa akajieleza kuwa alipata mtoto lakini mazingira ya kuzaliwa mtoto mwenyewe hayakuandaliwa, na walikubaliana na mzazi mwenzake kuwa atakuwa anamtunza mtoto huko aliko.
Binamu yangu akaja kugundua yule mtoto na matoto wake wa kwanza wamepishana kama miaka miaka miwili hivi. Akamwambia mume wake, ni kheri watoto wajuane na walelewe pamoja ili tabia zao zisipishane pia wajenge upendo. Mama wa yule mtoto alikataa kumwachia mtoto wake ahamie pale na kulelewa na mama wa kambo. Binamu akamwambia yule mama hivyo utakuwa unamkosesha mtoto mapenzi ya baba yake. Basi mama alikubali mtoto awe anakuja likizo kwa baba yake.
Mazingira anayoishi yule mtoto ni tofauti ya wenzake, binamu akaanza kumfanyia mtoto shopping, kumnunulia games na toys, ect. Likizo ilipokwisha akanunuliwa vifaa vya shule na zawadi kwa mama yake.
Likizo iliyofuata mambo yalianza kubadilika ndani ya nyumba, baada ya yule mtoto kuja, Amani ndani ya nyumba ilipotea, ikawa binamu na mume wake kugombana. Binamu ni mwana maombi wa nguvu. Sasa siku moja ilikuwa Jmosi, akamkuta yule mtoto yuko jikoni peke yake, akamuuliza unafanya nini huku, watoto hawaruhusiwi jikoni bila kuwepo na mkubwa karibu? Kumchunguza mtoto alikuwa amewasha jiko anataka kuchoma unga unga ulikuwa kwenye karatasi.
Binamu akaanza kutetemeka, ndiyo mtoto kuulizwa kwa kirefu akajieleza kuwa ule unga alipewa na mama yake, akiuchoma basi Amani ipotee ndani ya nyumba na mwisho wa siku waachane ili mama aje kukaa yeye. Binamu ngachoka, ikaamuliwa matumizi ya yule mtoto yamfuate huko huko kwa mama yake.