Kwa hili dada zetu mmetuweza! - mnatufanya tuamini tumewachagua!

Yaani hiyo Avatar yako! mimi naaminigi ndiyo wewe na siku ukinitokea hata kama sura kama unakamuliwa jipu mimi nitakuwa navuta tu avatar yako ili mzuka unipande!
uzuri mimi situmii picha ya mtu huyo ndo mimi mkuu
 
kukubaliwa kwa mwanaume hvegemea hasa utangulizi wako ulikuwa vp.kama utangulizi ulikuwa mbaya unanyima nafasi ya kukubaliwa.
 
Jamani mimi nilimfukuzia msichana kwa miezi sita mpaka nikakata tamaa! siku nakutana na rafiki zake wananiambia eti picha zangu zilikuwa zimebandikwa chumba kizima! sasa sijui alikuwa ananikataa nini!
Ndio hapo hawa watu mimi huwa nawashangaa, anakusumbua kumbe alishakubaliana na wewe...
 
Ila wanawake wengine wanaudhi unamtongoza anakataa,lakini baadae ukishaamua kufuata mambo yako ndio yeye anjileta tena!
 
Kumbe wanaume tunajipaga moyo kweli kwamba tumetongoza na kukubaliwa; na wakati mwingine tunaamini kabisa kuwa sisi ndio tumemchagua mwanamke! Kumbe ukweli ni kuwa wanawake ndio wanatuchagua sisi kwanza kule kutongoza na kukubaliwa ni wao tu kutengenezea njia tu ya kuwafikia!

Mzee mwanakijiji, sielewi umewaza nini mpaka ukajikuta unawaza kwa sauti hivyo. Ila ni kweli, asipokupenda mwanamke utajua reaction yake kutoka mwanzo. lakini akikupenda pia utahisi lakini hutajua ukweli wote. Wengine wanajisogeza kupunguza makali waliyo nayo kwa kukutumia wewe bila hata kuwa na punje ya kukupenda. Akitokea ampendaye kweli anakutema kama utemavyo mabaki ya muwa uliyotafuna kwa sana tu. Si unajua, unaangalia litaanguakia wapi unapotema? Kipande cha muwa hutaki hata kidondoke au kuguswa na mtu au mdudu yeyote. Tamaa ya mwanamke iliandikiwa kuwa kwa mwanaume tangu enzi za Hawa wakati Mungu alipompa kila mtu kipande chake, Adam akaangukia michongoma, ndio maana tunabembeleza sana nao wanatusanifu tukijidhalilisha, na labda usipewe bado, ukibahatika unakufa na ahadi kibao zisizotimilika.."ntakupa, utapata, utapewa, subiri, mvumilivu hula mbivu, nikuzoee kwanza, .....n.k"


Wanawake wakiwa na kiu hiyo wanapagawa, ndio wale wasiosubiri ila wanatafuta muda kukuchomekea au kuelekea kwa watoto.
 
ni kweli mkuu.mimi nikimtamani mtu najigonga gonga wewe uzuri wanaume huwa mnaelewa mapema.mnasafisha njia
ni ngumu mwanaume from nowhere amtongoze mwanamke amkubalie ni ngumu sana
hata hapa jf nikitaka mtu anitongoze na mpm tu kumpa salamu asubuhi hadi jioni keshanipa mashairi

Dah kumpa salam tu anaanza kutongoza hahah huyu atakuwa ameshindakana..
 
ni kweli mkuu.mimi nikimtamani mtu najigonga gonga wewe uzuri wanaume huwa mnaelewa mapema.mnasafisha njia
ni ngumu mwanaume from nowhere amtongoze mwanamke amkubalie ni ngumu sana
hata hapa jf nikitaka mtu anitongoze na mpm tu kumpa salamu asubuhi hadi jioni keshanipa mashairi
ayaah!! kumbe nilipoteza bahati ile siku!! mimi nlijua salam tu..
 
Mkuu Mwanakijiji heshima kwako.

Nakubali ulichokisema kipo lakini sio kwa asilimia mia moja zote.
Mkuu wewe umeongea kama mwanaume anayewajua wanawake lkn mim naongea kama mwanamke ambaye ndiye ninayetongozwa.

Sio kweli kuwa wanawake wote tunatongozwa baada ya kuvutiwa na wanaume kisha kujilengesha kwao ili watutongoze.
Mim kama binti,nina uzoefu wa kutongozwa tokea niko shule,mim na rafiki zangu mara nyingi tu ilikua inatokea tunatongozwa na vijana ambao kamwe hatukuvutiwa nao na hivyo tuliwakataa.Tena unakuta wengine unajikuta unajenga kama kachuki au kahasira fulani juu yao sababu kila ukiwaambia haiwezekani tukawa pamoja wao wanazidi kukufuatilia,mara leo card mara kesho kampa mtu pesa akuletee,mara sijui kesho kafanya hivi jambo ambalo linageuka kero.

Sio kweli kwamba wanaume wote tulionao sisi ndio tumewachagua,asilimia kubwa wanaume ndio wanavutiwa na sisi kisha wanatuona bora kuliko wengine machoni mwao kutokana na muonekano wetu au kutokana na tabia zetu kuwavutia hivyo wanatuchagua na kututongoza.

Swali langu kwako mkuu ni kwamba,kama kweli sisi wanawake tunatongozwa baada ya kuwa tumevutiwa na wanaume na kuwajengea mazingira ya kututongoza KWANINI WAPO WANAUME WANAOTONGOZA NA KUKATALIWA?
Tena saa nyingine unakuta kuna mwanaume amezoea anakubaliwa na kila mwanamke anayemtongoza lkn ipo siku inatokea anatongoza msichana lakini huyo msichana anamkataa huyo kaka mwenye maujuzi yote ya kutongoza.
 
Back
Top Bottom