Kwa hili, Clatous Chama ajitafakari, hakupata ushauri mzuri

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,319
12,622
Kila mchezaji duniani kote ana ndoto na anaomba ajiunge na timu ambayo inashiriki mashindano ya kimataifa, ili acheze mechi za kimataifa kwa lengo la kujinadi kimataifa aonekane kimataifa ili apate timu zenye maslahi mazuri na mazingira bora ya kazi.

Ona mchezaji mkubwa Clatous Chama wa Simba, sasa hivi huku hayuko na kule hayuko, amebaki kuwa mtazamaji tu wa mechi za kimataifa kama wengine akina sisi. Yaani hachezi mechi za kimataifa za Simba wala za Berkane FC na umri unazidi kumtupa mkono.

Kufanya uamuzi wa aina hii kunahitaji ubongo uliovurugwa kabisa kiasi cha kuhitaji wataamu wa afya ya akili.

Ameamua kurudi kwenye ligi yenye changamoto nyingi sana za viwanja, waamuzi na management. Nadhani hakupata ushauri wa kutosha kabisa.
 
Ona mchezaji mkubwa Chama Sasa hivi huku hayuko na kule hayuko, amebaki kuwa mtazamaji TU wa mechi za kimataifa kama wengine akina sisi. Yaani hachezi mechi za kimataifa za Simba Wala za Berkane fc na umri unazidi kumtupa mkono...
Kwani ukipewa vitu viwili uchague, furaha + hela na kucheza, utachagua nini? Yeye amechagua furaha yake na ya familia yake, wewe ungechagua kucheza (ambako nako hujui)
 
Wachezaji wetu wote wakapimwe akili, wakili msomi hamna haja ya kumpima maana majibu yatakuwa kama wengi tunavyofikiria, Jonas tulitaka tumpeleke muhimbili kumpima ila mambo yakaingiliana, tutawapima wote mkuu wala usiwaze lazima tujihakikishie kuwa shida ni bangi au ndio akili zao zilivyo
 
Kilichomkuta chama kipo katika sheria ya mpira, kwa maana ya kwamba kingeweza kumkuta hata messi endapo angesajiliwa na simba
Kwani wakati anajiunga tena na Simba hakujua kama hatashiri mechi za kimataifa? Hapo ndipo panapohitaji upimaji wa akili. Umri alinaonao ni WA kushow case kimataifa, sio kurudi Manungu TU. Wenzake wanamcheka sana hata kama hawamwambii. Ni heri angekuwa mchezaji wa akiba kwenye timu yake ya Berkane kuliku alichofanya, mpuuzi kabisa wa soka.
 
Ona mchezaji mkubwa Chama Sasa hivi huku hayuko na kule hayuko, amebaki kuwa mtazamaji TU wa mechi za kimataifa kama wengine akina sisi. Yaani hachezi mechi za kimataifa za Simba Wala za Berkane fc na umri unazidi kumtupa mkono.
Kolo fulani hivi

1647166299705.png
 
Kwa namna hiyo wale wachazaji mliowasajili kwa kuwadanganya watacheza club bingwa Afrika wameenda kupima? Aucho au Bangala wamepimwa lini?
Walicheza kimataifa wakishindwa na wengine waliyakosa mashindano kwa sababu za transfer. Lakini Chama alihama wakati ule alifahamu wazi kuwa anakwenda kucheza Manungu complex TU.
 
Kwani ukipewa vitu viwili uchague, furaha + hela na kucheza, utachagua nini? Yeye amechagua furaha yake na ya familia yake, wewe ungechagua kucheza (ambako nako hujui)
Furaha!!!!! kufanya hivyo ndo sehemu ya ugonjwa wake wa akili. Yaani mchezaji kama yule hafanyi utafiti kabla ya kuamua?; yaani amekwenda kule bila kufahamu hali ya hewa ya kule, lugha, utamaduni, vyakula, afya yake nk. Hata mkimtazama Chama kwa makini sana kwa makini utagundua kuwa ana mapungufu fulani.
 
.... Hata mkimtazama Chama kwa makini sana kwa makini utagundua kuwa ana mapungufu fulani.
anaweza kuwa na mapungufu lakini akawa na furaha kuliko mtu asiye na mapungufu kabisa kama wewe. Yeye amefurahi kucheza Tanzania especially Simba, na ameiangalia zaidi familia yake. Wewe unaweza kuwa na vipaumbele vyako. Mfano, inawezekana ukakubali kufanyia kazi zako Mtwara huku mkeo yupo Bukoba na mambo ukayaona safi tu, wakati mtu mwingine kweke yeye akaona hiyo ni shida
 
Moja kati ya sheria ya kipumbavu ya FIFA ni hii ya kumzuia mchezaji kucheza mashindano fulani baada ya kuhama klabu. Hivi sababu ni nini hasa?
FIFA wako sahihi, Chama ndio mwenye shida kichwani. Mchezaji mkubwa kukosa mechi za kimataifa l bila sababu za maana ni nadra kuona.
 
Huwezi kujifunza kwa makosa yako mwenyewe, kabla ya kukubali kujiunga na Berkane alipaswa kufanya homework ya kuijua Morocco kwanza kabla ya kwenda huko. Wachezaji wakubwa wote wanafanya hivyo, Messi, Ronaldo, nk wanafanya kabla ya kukubali offer.
 
Usiwachukulie poa wachezaji au mawakala/ mameneja wao. Wakati mwingine ni michezo ya kupiga pesa. Fikiria Emmanuel Okwi alivyokuwa anazikomba hela za vilabu vingine (ikiwemo Yanga) halafu anarudi Simba kwa kisingizio cha 'kushindwa mazingira'. Unaweza ukasema ni mjinga, hafanyi utafiti, lakini kote huko alivunja mkataba akiwa na vitita vya fedha,

1647167857513.png
 
Walicheza kimataifa wakishindwa na wengine waliyakosa mashindano kwa sababu za transfer. Lakini Chama alihama wakati ule alifahamu wazi kuwa anakwenda kucheza Manungu complex TU.
Tunamweka na atakuja kutusaidia robo final au ww ulitaka acheze game gani uliyoona pengo lake?
 
FIFA wako sahihi, Chama ndio mwenye shida kichwani. Mchezaji mkubwa kukosa mechi za kimataifa l bila sababu za maana ni nadra kuona.
Mimi nimeongelea sheria wewe unamuongelea Chama kwani hii sheria inamhusu Chama tu? Unaleta ushabiki maandazi.
 
Moja kati ya sheria ya kipumbavu ya FIFA ni hii ya kumzuia mchezaji kucheza mashindano fulani baada ya kuhama klabu. Hivi sababu ni nini hasa?
Kuzuia mgongano wa kimaslahi hasa kwa vilabu ambavyo vina misuli mikubwa ya kifedha.
 
Kuzuia mgongano wa kimaslahi hasa kwa vilabu ambavyo vina misuli mikubwa ya kifedha.
Mbona ligi ya ndani wanaruhusu, yaani ndani ya msimu mmoja mchezaji anaweza kuhama kutoka Brentford na kuhamia Man u na akaendelea kucheza ligi, hapo imekaaje hamna mgongano wa kimaslahi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom